Msumbiji: Inasemekana Magaidi wamevamia Msafara wa Wanajeshi wa Tanzania na Lesotho

Hakuna nchi imewahi kujitosheleza kiulinzi juu ya magaidi.
Tatizo gaidi hatambuliki kwani anajichanganya na raia
 
Endelea kuamini ni propaganda sisi tuliopo huku mpakani tunaona kwa macho yetu hayo mambo ndugu yetu kipanya alichinjwa akatolewa kichwa na hao magaidi na wakasambaza picha za tukio hilo pale kitaya
Uko maeneo gani mkuu?
 
Hivi wanajeshi wetu wakiwa kwenye mission za kimataifa huwa wanatumia magari yenye namba za JWTZ? Siyo kwamba wanatuamia namba za mission iliyowapeleka kama SADC ama UN!! Najiuliza tu kwa sauti kubwa!! Nisaidieni wajuzi.
 
AK 47 haijawahi kuwa outdated mkuu..
Utachekwa.
AK-47 hata sights za kuweka infrared scope uitumie usiku haina. Ikifika usiku unapigana kama mpuuzi tu wa Boko Haram wakati wewe ni mwanajeshi wa taifa. Huwezi funga sight ya kupima umbali na kulenga shabaha, inategemea uwezo binafsi wa kulenga na uzoefu wa mwanajeshi. Kama unadhani Tanzania ina wanajeshi exceptional kiuwezo basi hujui kulinganisha majeshi au unapumbazwa na uzalendo feki ule unaoamini kujikweza ndio kuipenda nchi.

Hamza pale Salender unajua walimrushia risasi ngapi kabla ya kumuua, wakati ni bonge nyanya refu, kijana mzembe wa familia ya kitajiri hata rifle ukute alikuwa anaziona kwenye movie na aliuwawa barabarani. Sasa angekuwa ni trained terrorist kwa zile AK-47 na SMG unamuua saa ngapi.

Hawa ni Botswana wanazo kama FN FAL na SAR 21

Hawa ni Kenya nao wana hizi na AK-47 bado zipo nyingi

Hawa ni Russia standard rifle yao kijeshi kwa sasa ni AK-12 ambayo ni derivative ya AK-47 ila ya kisasa ingawa characteristics ni zilezile. Na hii ndio iko very simplified na basic. Waasisi wake wanaziacha kama sio outdated kwa nini

Hawa ni China na QBZ-191 ambayo ndio standard rifle. JW niliwaona na kitu kama QBZ-95 mwaka jana/juzi walipopigwa ambush na hawa magaidi ikakamatwa APC ya Kichina. Wachina walikuwa na SMG zao na copycat ya AK-47 wanaita Type 56 wakaziacha. Kama sio outdated kulikuwa na haja gani

Bunduki design ya 1947 haiwezi tumiwa na taifa serious kujilinda. Hiyo ni very cheap ila hata effective range yake ndogo kiasi, accuracy ndio kwa standard za sasa ni ndogo na sights hamna. Hizo bunduki nilizotaja wala sio expensive, sio lazima ziwe hizi. Wajerumani ndio wana bunduki nyingi hatuwezi afford
 
Endelea kuamini ni propaganda sisi tuliopo huku mpakani tunaona kwa macho yetu hayo mambo ndugu yetu kipanya alichinjwa akatolewa kichwa na hao magaidi na wakasambaza picha za tukio hilo pale kitaya
Naaaamini umefungua ID mpya kwa ajili ya Kutuma habari za Ugaidi huko Kusini Mkuu.
 
ka ni kweli soon taanza sikia mtwara vurugu vuruguu za wale wanaovuka mto na kuja kusumbua vijiji jirani
 
Hakuna nchi imewahi kujitosheleza kiulinzi juu ya magaidi.
Tatizo gaidi hatambuliki kwani anajichanganya na raia
Kipindi mauaji ya rufuji..kituo chao kikuu ilikua ikwiriri..hao jamaa bila kuwa na inteligensi kali huwezi kuwamaliza...mana ni raia kama raia tu unakula nao unacheka nao.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kipindi mauaji ya rufuji..kituo chao kikuu ilikua ikwiriri..hao jamaa bila kuwa na inteligensi kali huwezi kuwamaliza...mana ni raia kama raia tu unakula nao unacheka nao.

#MaendeleoHayanaChama
Sahihi
 
Duuh Nimeumia kuaona vifaa vya jesh letu vimeangukia kwa hao magaidi sijajua hali za hao askari wetu kama wako salama au wamekufa.
Yale yanayoikumba Russia huko Ukraine ya kudhalilishwa kwenye mitandao Mapicha ya magari na vifaru vikiibiwa na matrekta ya wakulima ndio Yanayotaka kulikumba Jeshi letu.
MUNGU TULINDE aibu hii ipite na isijirudie tena .

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Kinachofanyika ni kuziba barabara na kusimamisha magari na pikipiki na kuanza kuuliza vitambulisho ukipoza 5000 unapita bila shida vijiji vya karibu na mpaka,
Aisee sijui ndio intelijensia yenyewe yaani mjeshi in AK47 inakuuliza kitambulisho tu
 
Dude kama hilo ni bei gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…