Msumbiji: Inasemekana Magaidi wamevamia Msafara wa Wanajeshi wa Tanzania na Lesotho

Msumbiji: Inasemekana Magaidi wamevamia Msafara wa Wanajeshi wa Tanzania na Lesotho

Mode naomba ufutwe huu uzi si kila taarifa ina hitaji jamii kujua. Mtoa mada unasafari ya kujifunza juu ya ulinzi n aman ya nchi yako
Acha ujinga wako, kwamba hizo taarifa apewe nani?
 
Hata kama naishi kwa dada yangu bado ukweli utabaki vilevile kuwa kazi ya jeshi ni ya kijinga.
Unaishi kwa amri mpaka unastaafu.
Hata CDF anaishi kwa amri, je hawa ma junior!!
We jamaa una akili gani wewe!!!! Sasa si ndo majukumu yao unadhani kila mtu akiwa na akili kama zako nchi itakuwa na jeshi????
 
Jamani Hawa IS si watu wazuri
Kuna jamaa anatengeneza maboti pale Slipway boat yard mwarabu wa Mombasa naskia nae ni member inabidi achunguzwe maana siku chache zilizopita ulizuka moto Slipway
V8 ya 2022 namba A naiwasha sasahivi naenda hapo, kabla hawajaleta ya west_gate hapa, maana hawa kwa revenge hawapo nyuma
 
Hata kama naishi kwa dada yangu bado ukweli utabaki vilevile kuwa kazi ya jeshi ni ya kijinga.
Unaishi kwa amri mpaka unastaafu.
Hata CDF anaishi kwa amri, je hawa ma junior!!
Hapo una mchumu na unapita hivi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
JamiiForums914395227.jpg
 
Ndio maana unaambiwa huna akili, kumbe ni kweli!
Wewe mwenye akili zimekupa utajiri kiasi gani? Umezifanyia nini hizo akili ulizonazo zaidi ya kubishana na mimi unaesema sina akili au ndio mwisho wa uwezo wako wa kufikiri? Alafu unabishana na mimi huku unasema sina akili hivi unadhani nani anaeonekana hana akili? Jipimie ila usipimane na mimi, JF kumbe kumejaa WAJINGA hivi
 
Sisi wabongo ujuaji mwingi sana alafu hatujui mambo mbaya zaidi hatutaki wala hatupo tayari kujifunza. Sisi tumekalia kula na kulala kumbe kuna mambo mengi huko yanaendelea na hatuyajui kabisa ndio maana Kigwangala alituchana ukweli kwamba sisi watanzania shida yetu ni chakula tu. Watu walimjia juu sana ila ndio ukweli wenyewe
Nashangaa sana Watanzania hawajabisha. Miaka miwili nyuma hapa ningesema hivi wangeniita sio mzalendo, niko kwa shemeji nalala wakati watu wananilinda misituni, jeshi letu ni imara sana. Kuna wale hamna kitu kabisa wanadiriki kusema sisi jeshi la ardhini ni wa kwanza Afrika, wengine wanakwambia jeshi ni uzalendo as if ukivamiwa na adui uzalendo ndio mbadala wa silaha.

Wengine hushangilia na kusifia maonyesho ya makomandoo kwenye sherehe za uhuru wakijua ndio uwezo wa kijeshi. Zile gears wanazokuwa nazo sijawahi zikubali kabisa, show za ukakamavu sizipingi ila haiondoi udhaifu wa kutokuwa na zana bora.

Changamoto ni kwa serikali, jeshi halina tatizo lolote. Specifically tatizo ni umaskini na mikakati. Tusiombe kudhibitisha ninachomaanisha, navy ipo Kigamboni ila siku itokee kivuko kimepata changamoto kwenye maji unayoona pande zote mbili kwa macho utashangaa performance ya jeshi.

Na zana ninazosema hapa sio hizi za kupigana na taifa jirani.
Nasema zana chache kufanya missions dhidi ya magaidi, majangili, maharamia na kufanya uokoaji maana zana huwa na dual use. Pale ajari ya ndege Bukoba wangekuwepo sailors na divers wa navy wangesaidia. Sasa ushindwe kuokoa watu 30 ajari ya 150 meters kutoka ufukweni sembuse ajari ya meli yenye mamia ya watu kilomita ngapi ziwani ambapo raia wema hawatokuwepo
 
Kwenye masuala haya huwa najifunza mengi sana kupitia wewe, mkuu hivi wewe ni soja?
Hiyo ni Maxxpro na silaha za Magharibi ni za bei kidogo. Tunaweza chukua za South Africa (tunazo kadhaa, Kenya wanazo, Uganda wanazo na wana assembly line walijenga, West Africa ndio zimejazana). Tunaweza chukua za Uturuki na Chinese. Russia zile BTR na BMP ni heavy sana hazifai kupigana na magaidi na sio za kisasa kivile kwa leo, kwanza sio MRAP zile. Ujue silaha ukinunua utakaa nayo miaka 30 uko, sasa ukinunua silaha ya 1970 leo ni hasara. Kwa Russia ile Tigr nayo ni nzuri.

Kenya mwaka jana waliagiza Katmerciler Hiriz kutoka Uturuki kama ile niliyosema wanazo Chad. Mtengenezaji anaweza kukupa configuration tofauti kama command & control vehicle, CBRN vehicle, weapon carrier, ambulance, border-security vehicle au reconnaissance vehicle. Kutokana na configuration na bei inatofautiana ila Kenya iliagiza magari 118 kwa bei inayokadiriwa kuwa ni $70 million. Sio expensive kivile Waturuki hawana bei ya kukomoaView attachment 2423733

Ni 4×4 ina Allison system kwenye uendeshaji, magari kama haya hayatakiwi kupinduka wanajeshi ndani wasijigonge kuvunjika au kupata brain damage likikanyaga bomu
 
Habari za Kina

Kuvamia doria ya pamoja ya majeshi ya Msumbiji na Tanzania na kuchoma magari 3 katika shambulio la wapiganaji wa Islamic State kaskazini mwa Msumbiji.

SHIRIKA LA HABARI LA AMAQ

3944 JW22

Moja ya gari lililokamatwa na wapiganaji wa Islamic State baada ya kuvizia karibu na kijiji cha "Vondanhar" -

Msumbiji - Cabo Delgado - Shirika la Habari la Amaq: Doria ya pamoja ya majeshi ya Msumbiji na Tanzania yalipata hasara ya mali katika shambulio la wapiganaji wa Islamic State katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado.

mashariki mwa Msumbiji. Vyanzo vya usalama vililiambia shirika la "Amaq" kuwa wapiganaji wa Dola ya Kiislamu walianzisha mashambulizi ya kuvizia yenye silaha, Jumanne iliyopita, kwa ajili ya doria ya pamoja ya majeshi ya Msumbiji na Tanzania yaliyokuwa yakisafiri katika moja ya barabara kati ya eneo la "Ningad" na kijiji cha Fundanhar. katika mkoa wa "Palma".

Habari hizo zimeongeza kuwa, shambulizi hilo la kuvizia lilisababisha kukamatwa kwa magari 3 na kuyachoma moto baada ya askari hao kuwakimbia, pamoja na kukamata silaha na risasi. Vyanzo vya habari vilithibitisha kujiondoa kwa wapiganaji wa Islamic State kwenye nafasi zao baada ya shambulio hilo.

Novemba 18, 2022
 
Back
Top Bottom