Nashangaa sana Watanzania hawajabisha. Miaka miwili nyuma hapa ningesema hivi wangeniita sio mzalendo, niko kwa shemeji nalala wakati watu wananilinda misituni, jeshi letu ni imara sana. Kuna wale hamna kitu kabisa wanadiriki kusema sisi jeshi la ardhini ni wa kwanza Afrika, wengine wanakwambia jeshi ni uzalendo as if ukivamiwa na adui uzalendo ndio mbadala wa silaha.
Wengine hushangilia na kusifia maonyesho ya makomandoo kwenye sherehe za uhuru wakijua ndio uwezo wa kijeshi. Zile gears wanazokuwa nazo sijawahi zikubali kabisa, show za ukakamavu sizipingi ila haiondoi udhaifu wa kutokuwa na zana bora.
Changamoto ni kwa serikali, jeshi halina tatizo lolote. Specifically tatizo ni umaskini na mikakati. Tusiombe kudhibitisha ninachomaanisha, navy ipo Kigamboni ila siku itokee kivuko kimepata changamoto kwenye maji unayoona pande zote mbili kwa macho utashangaa performance ya jeshi.
Na zana ninazosema hapa sio hizi za kupigana na taifa jirani.
Nasema zana chache kufanya missions dhidi ya magaidi, majangili, maharamia na kufanya uokoaji maana zana huwa na dual use. Pale ajari ya ndege Bukoba wangekuwepo sailors na divers wa navy wangesaidia. Sasa ushindwe kuokoa watu 30 ajari ya 150 meters kutoka ufukweni sembuse ajari ya meli yenye mamia ya watu kilomita ngapi ziwani ambapo raia wema hawatokuwepo