guda masta
New Member
- Feb 4, 2024
- 1
- 0
Mtaa wa Nzasa, eneo lililo karibu na nyumba za walimu wa UDSM, kuanzia Barabara ya Kitambaa Cheupe hadi kwa Mama Ngoma, unakabiliwa na tatizo la mara kwa mara la mifumo ya maji taka kuziba na chemba kujaa.
Hali hii imekuwa kero kubwa kwa wakazi, hasa ikizingatiwa kuwa watoto hupita katika njia hiyo. Maji machafu ya vyooni hutiririka kwa wingi kama vile yanasukumwa na pampu, jambo linalohatarisha afya ya wakazi na linaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko.
Tunaomba mamlaka husika zichukue hatua za haraka kutatua tatizo hili.