Mtaalam wa kuwekeza kwenye kuku tayari ameshawaliza

Mtaalam wa kuwekeza kwenye kuku tayari ameshawaliza

Mkuu umenikumbusha shule ya msingi tulikuwa tunaweka nyoya la tausi katikati ya daftari tukiamini atakua ndege mzima! Kumbe zile akili kuna watu wamekua nazo!
Hahaha
 
Miaka ya nyuma ziliuzwa hisa za benki ya DCB, nikanunua za tshs 50k baada ya miaka kama mitano gawio 9k,nikajua hapa kuna ujinga sana kwenye maswala ya hisa, zilipotangazwa za voda, nikakaa pembeni nacheka tu, watu wakazivamia balaa, leo wanauza kwa hasara na bado!
Umenikumbusha jambo ambalo kidogo nigombane na wife kuhusu hisa za voda baada ya Kung,ang,ania tununue hisa nikakataa. Maendeleo yake yakoje kiongozi ili nirudishie mrejesho kwa wife
 
Deci kama deci.

Watanzania hatujifunzi. Kila siku deci inakuja kwa jina lingine.

Pyramid au Ponzi scheme ina sura na rangi nyingi.
 
Miaka ya nyuma ziliuzwa hisa za benki ya DCB, nikanunua za tshs 50k baada ya miaka kama mitano gawio 9k,nikajua hapa kuna ujinga sana kwenye maswala ya hisa, zilipotangazwa za voda, nikakaa pembeni nacheka tu, watu wakazivamia balaa, leo wanauza kwa hasara na bado!
Hisa za voda zimenipa somo kubwa sana. Yaani 1M inakuzalishia gawio la elfu 20 kwa mwaka mzima!!!
 
Corona iliposhamiri nikajua obvious hiyo project itakwama , nilikuwa na study mama chanja anavohangaika na soko la kuku wake na ye ni mfugaji wa small scalle.

On a serious note , sijaelewa kwa nini watanzania tunakuwa addicted kwenye kupata pesa kirahisi na tunaishia kupigwa pesa , project haikuwa tofauti na deci yet watu wa kupigwa wamepatikana .
Sent
Mkuu sisi ni wavivu, wazembe na tusiopenda kujishughulisha!

Ndiyo maana akitokea mtu, akasema atatufanyia kazi fulani sisi tutoe pesa tu then tutagawana faida, huwa hatuwezi kureason kabisa kwa sababu ya uvivu

Sent from my SM-J105H using JamiiForums mobile app
 
Niliwahi kupigwa kijinga sana, tena nilishawishiwa na vitoto vya Chuo... kwa jeuri na kuonesha utofauti basi nikajitupia 800k.

Niliambulia 40k tu, ambayo alinigawia aliyeniingiza kama nusu ya kamisheni yake.

Nilijifunza kwa ada kubwa, sitarudia tena ujinga.

Rise Africa, maanina zao!

Ilikua inadeal na Nini? Alafu wanajuaga na majina yeny mvuto😄
 
Nilivyo sikia tu eti account inashikiliwa na watu wa PCCB,sijui vibari vimekamatwa..nikajua kuna watu washapingwa huko..
Mkuu
Hebu Mwagika Vema Tuwafute Machozi Waliopigwa
 
Mkuu sisi ni wavivu, wazembe na tusiopenda kujishughulisha!

Ndiyo maana akitokea mtu, akasema atatufanyia kazi fulani sisi tutoe pesa tu then tutagawana faida, huwa hatuwezi kureason kabisa kwa sababu ya uvivu

Sent from my SM-J105H using JamiiForums mobile app
Rejea uwekezaji wa boda boda, sijabahatika katika watu wangu wa karibu kuona aliyefanikiwa, wengine waliwekeza moja wengine mbili, na mmoja aliwekeza boda tatu sehemu tatu tofauti, kabla ya miezi sita zilirudi zote mbovu na hajarudisha hata nusu ya hela,pmbav!
 
Na ujue kabisa unanunua hisa kwa malengo gani?Ya muda mfupi au muda mrefu.

Maana huko duniani kuna Ma co. Kama Ya kina Warren Buffet(Mmiliki wa Coca-cola na biashara nyingine nyingi) wao sera zao ni hakuna kulipa dividends(gawio)wakipata faida kwny biashara yao hizo pesa wanazi-retain na kuzirudisha kwny biashara zao so wewe kama mwana hisa faida yako unayopata ni hiza zako kuongezeka thamani na ukitaka kuuza hisa zako utapiga pesa kwny Capital gains.

Daah sijui hata kama nimeeleweka mazee.
Nimekuelewa sana mazee!
 
Mkuu, hisa nimenunua 2017 lkn hadi leo hii sijawahi pokea gawio zaidi ya elfu 30 kwa mwaka. Hisa nilizonunua ni za shilingi milioni moja. You can imagine, kweli milioni inazalisha faida ya elfu ishirini tu kwa mwaka mzima? It means mtu aliyenunua hisa za milioni kumi aliambulia gawio la laki mbili tu! Ni ajabu sana. Gawio la kwanza nilipata kama elfu 12, gawio la pili nilipata elfu 20 hivi na gawio la tatu sikumbuki lkn ni hizo hizo za elfu 10 hadi 30 hapo.

Mimi nadhani hisa za voda zilikuwa overpriced ukilinganisha na uhalisia ndio maana profit per share imekuwa ndogo mno hadi unajiuliza hv ni kweli voda wapo Tz kwa ajili ya kuzalisha elfu 20 kwenye milioni moja kwa mwaka mzima. This is ridiculous! Au pengine voda hawakuwa na haja ya kuongeza mtaji bali walilazimishwa hivyo walikusanya mtaji ambao hawakuwa wanauhitaji na hivyo hautumiki kuzalisha faida. May be kampuni inaweza kuwa ilikuwa imefika maxmum level of growth Kwa hivyo mtaji mpya haujatumika kufanya ukuzaji wowote wa biashara, ikiwa na maana pesa imeenda pasipohitajika
 
Mkuu umenikumbusha shule ya msingi tulikuwa tunaweka nyoya la tausi katikati ya daftari tukiamini atakua ndege mzima! Kumbe zile akili kuna watu wamekua nazo!
Na Chakula Chake ilikuwa Vumbi Za Chaki Baada Ya Mwalimu Kutoka Tunagombania Ule Unga Pale Chini ya Ubao Tuwalishe Tausi Wetu Wazidi Kunenepa.

Sasa Uache Daftari Watu Waje Wamuibe Tausi Unaeza Kugeuza Darasa.

Tukija Kwa Wale Wafanya Biashara Walokua Wanatuuzia, Wanatupanga Foleni na Wanauza Uku Wanaringa Ela Ya Kula Inaishia Kwa Mabawa Ya Tausi.
 
Back
Top Bottom