Mtaalam wa ndege CNN: Watu 26 kati ya 43 kuokolewa ni nzuri sana kwa ajali ya ndege

Mary Schiavo ameshika nafasi mbalimbali Marekani ikiwemo mkurugenzi mkuu wa idara ya usafirishaji Marekani na kwasasa ni mchambuzi wa usafiri wa anga kwenye kituo cha CNN.

Kuhusu ndege iliyopata ajali, Mary kasema ndege za ATR ziliacha kutumika nchini Marekani kwa sababu ya ajali za mara kwa mara hivyo kutolewa kwenye huduma.

Mary pia amemuongelea Pilot na kumpa kongole kwa kuishusha ndege kwenye maji bila kuigonga(Landing instead of crash). Mary amesema ndege hazifanyi boti na ikidondoka majini huzama.

Amemaliza kwa kusema watu 26 kupona kwenye 43 ni takwimu nzuri sana kwenye ajali za sekta ya anga.

Nami namaliza, inachukua dakika 4-6 kwa binadamu aliyezama majini bila kuibuka kufariki. Labda changamoto iwe mawasiliano, kinyume na hapo tushukuru waliowahi lakini kwa nchi nyingi idadi ya vifo ingebaki kama ilivyo na ile inabaki kuwa ajali.

View attachment 2410063
Idadi ya walionusurika ingelikuwa kubwa zaidi ya hiyo endapo waokozi wangelifanya kazi zao sawasawa badala ya kumuachia mvuvi.
 
Mary Schiavo ameshika nafasi mbalimbali Marekani ikiwemo mkurugenzi mkuu wa idara ya usafirishaji Marekani na kwasasa ni mchambuzi wa usafiri wa anga kwenye kituo cha CNN.

Kuhusu ndege iliyopata ajali, Mary kasema ndege za ATR ziliacha kutumika nchini Marekani kwa sababu ya ajali za mara kwa mara hivyo kutolewa kwenye huduma.

Mary pia amemuongelea Pilot na kumpa kongole kwa kuishusha ndege kwenye maji bila kuigonga(Landing instead of crash). Mary amesema ndege hazifanyi boti na ikidondoka majini huzama.

Amemaliza kwa kusema watu 26 kupona kwenye 43 ni takwimu nzuri sana kwenye ajali za sekta ya anga.

Nami namaliza, inachukua dakika 4-6 kwa binadamu aliyezama majini bila kuibuka kufariki. Labda changamoto iwe mawasiliano, kinyume na hapo tushukuru waliowahi lakini kwa nchi nyingi idadi ya vifo ingebaki kama ilivyo na ile inabaki kuwa ajali.

View attachment 2410063
Daah
 
Kuna wahuni kule ista wameweka namba ya kumchangia mvuvi majaliwa,watu wabongo sio watu.
 
Mary Schiavo ameshika nafasi mbalimbali Marekani ikiwemo mkurugenzi mkuu wa idara ya usafirishaji Marekani na kwasasa ni mchambuzi wa usafiri wa anga kwenye kituo cha CNN.

Kuhusu ndege iliyopata ajali, Mary kasema ndege za ATR ziliacha kutumika nchini Marekani kwa sababu ya ajali za mara kwa mara hivyo kutolewa kwenye huduma.

Mary pia amemuongelea Pilot na kumpa kongole kwa kuishusha ndege kwenye maji bila kuigonga(Landing instead of crash). Mary amesema ndege hazifanyi boti na ikidondoka majini huzama.

Amemaliza kwa kusema watu 26 kupona kwenye 43 ni takwimu nzuri sana kwenye ajali za sekta ya anga.

Nami namaliza, inachukua dakika 4-6 kwa binadamu aliyezama majini bila kuibuka kufariki. Labda changamoto iwe mawasiliano, kinyume na hapo tushukuru waliowahi lakini kwa nchi nyingi idadi ya vifo ingebaki kama ilivyo na ile inabaki kuwa ajali.

View attachment 2410063
Hajaambiwa majaliwa ndiye akaokoa ,amuite kwa USA army Navy seal command faster apewe green card na bado kijana bado mbichi kabisa yaani bado kabisa. Akiingia huko anafanya maendeleo home kwao mpaka dingi yake anakuja kujiliza kwake kuwa hamjali. Ataomba arudiane na mama yake Mana hayuko mbali sema tu Ni masuala ya kindoa. Eti Ni ya kifamilia kisa pesa jamani Ila njaa haina adabu
 
"Dakika 4 kwa mtu kufa akiwa ndani ya maji kwa kukosa hewa"
Sawa!
Swali kwako Replica !

Je!
Yule kijana #Majaliwa alitumia muda gani kufika hadi kwenye Ndege,huku akitumia mtumbwi wa kasia na kukuta bado watu wakiwa hai?

Je!
Unaweza kutuonyesha clip ya hata,askari mmoja wa kikosi cha uokoaji cha serikali aliyekuwa sambamba na wavuvi wale on time?

Je!
Kama mkuu wa mkoa wa Kagera alifika eneo la tukio,na kuuthibitishia Umma kupitia vyombo vya habari.
Kwamba ameweza kuongea na walioko ndani ya ndege,hiyo yote ilikuwa ni ndani ya hizo dakika nne zako?

Hapa tunajiuliza na kutathmini u-haraka wa kuweza kufika eneo la tukio na kufanya kinachowezekana kwa wakati!

Huyo mzungu wa CNN,ametoa maoni yake kuhusiana na "Rapid response emergency landing capability of the pilot"

Hakutoa maoni kuhusu umbali wa tukio kutoka pwani ya ziwa na kingo za uwanja wa ndege.

Suala la umri na uchakavu wa ndege,linabaki kuwa technical faults,sisi tunaongelea uzembe wa serikali katika uokozi wa majanga.

Sijui wewe umetumwa kumtetea nani?

Ni CCM au Kutetea Serikali?
Alamsikhi!
10101.
Haya ndiyo maswali ya msingi ambayo wasingependa tujadili.
 
Kama hatuna makomando na kambi za kijeshi ENEO la mkoa wa kagera na ni mpakani bas we are not the state anymore!tena kagera mkoa wa mpakani wa uganda kabisa!!!

Fikiria upya!
Si ajabu mabeberu wanatugeuzageuza wapendavyo kama chapati za unga wa Azam.
 
Back
Top Bottom