Kwenye UTI kuna kundi mbili. UTI "complicated" na UTI "uncomplicated". Kwa ajili ya wanaume inakua complicated, yaani tunatizama kama vimelea wamefika kwenye figo pia.
Ni vizuri kwa madaktari wachukuwe sampuli ya mkojo ilikutizama vimelea wanasugu na dawa gani. Kama mtu anatatizo kwenye mirija yakukojoa, hilo ni tatizo lingine na matibabu yake nitofauti kabisa.
Matibabu ya kwanza ni dawa yakuua viemlea. Kuna dawa aina nyingi zinazotumika. Septrin na Ciprofloxacin huwa inatumika sana na ndiyo maana siku hizi vimelea vimejenga sugu juu ya dawa hizi. Kunywa maji na juisi ya cranberry huwa inasaidia kwa kiwango pia. Hii ni kwasababu maji inapunguza idadi ya vimelea. Kwa wale wagonjwa waliokuwa na tatizo hili kwa kila mara, antibiotic za sindano (Ampicillin pamoja na Gentamicin) inashauriwa.
Wagonjwa wengi siku hizi wakitumia Amoxiclav 500mg inawasaidia kwakutosha. lakini kuna antibiotic nyingi yanaoweza kutumika kwa wale waliokuwa na vimelea vyenye sugu.