Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Dr. Natoka kiasi kikubwa cha ute mweupe kama karatasi ukeni, hautoe harufu, nawashwa kiasi kidogo na sisikii maumivu. Nimepima UTI na fungus nimeambiwa sina mambukizi hayo. Ute huo huongezeka zaidi nikikaribia siku zangu. Ni ute mwingi mpaka nguo ya ndani inalowa sana. Huu ni mwaka wa tatu sasa kila nikipima wanasema hawaoni fungus.

Kwa dalili hizo linaweza kuwa mambo mengi. Ningekushauri umuuone Gynecologist. Hawa ni daktari bingwa juu ya swala hilo.

Asante.
 
Dr. Uso wangu una mafuta mengi sana mpaka natamani niyauze..

Nimejaribu kutumia cosmetics mbali mbali za kufanya skin kuwa dry lakini hazijasaidia..

Unanisaidiaje niweze kuondokana na hali hii?

Maanake nikiwa juani usoo una ng'aa kweli kama sentimila ya ISUZU na mimi sipendi mng'ao huo.

Tumia Dawa hii yakupakaa; Retin A Cream. Alafu niambie unaendeleaje.

Asante
 
Dr. TB kwa uelewa wangu mdogo wanasema huwa inakuwa na dalili za kukohoa kikohozi kikavu kwa muda mrefu (wiki 2), Mimi sina kikohozi cha namna hii. na sikohoi kabisa. labda kuna zaidi ya hilo katika TB??

Kuna TB aina nyingi. Unachosema wewe ni Kifua Kikuu TB ya mapafu lakini nachosema mimi ni TB ya mgongo. Pia wiki ijayo unaweza kuelimika juu ya TB kwa kutazama video hii: Afya Yako with Dr. Sajjad Fazel
 
Dr. SF,
Samahani Dr. niulizia kuwa kuna njia ya kusafisha au kuondoa ukoko,ukoko ndani ya Urinary bladder !! au haina haja... japo kuwa hakuna sumptoms zozote!!
 
Kuna TB aina nyingi. Unachosema wewe ni Kifua Kikuu TB ya mapafu lakini nachosema mimi ni TB ya mgongo. Pia wiki ijayo unaweza kuelimika juu ya TB kwa kutazama video hii: Afya Yako with Dr. Sajjad Fazel
Thanks a lot! sasa nimekuelewa. Hii video naitazama kupitia wapi??? TV ama hapa hapa?

Naweza kupata apointment ya kukuona kwa uchunguzi zaidi kama uko tanzania???
 
Thanks a lot! sasa nimekuelewa. Hii video naitazama kupitia wapi??? TV ama hapa hapa?

Naweza kupata apointment ya kukuona kwa uchunguzi zaidi kama uko tanzania???

Kwa sasa hivi nipo mamlaka ya chakula na dawa.
Unaweza kuiona kwenye tovuti hilo. Kuna kipindi moja juu ya Kifua Kikuu nilifanya na Clouds Tv.
Unaweza kuiona hapa chini:
 
Habari mkuu
Mimi nasumbuliwa sa na miguu huwa inawaka moto mpaka nashindwa kulala, nimetumia baadhi ya dawa lakini tatizo bado liko pale pale zaidi sana nimepima sukari na presure ziko nomal wamenipa dawa za neves lakini wapi bado inachoma choma. Naomba unisaidie nitumie dawa gani nateseka sana dr, na je utakuwa ni ugonjwa gani unasababishwa na nini? Asante
 
ninasumbuliwa na pua kuziba sana baada ya muda ina badili kutoka pua moja na kwenda nyingine na mafua ya Mara kwa Mara yananipata nimeenda hospital tofauti nimeambiwa Nina allerg katika Tiba zao sikufanikiwa kupata nafuu je ninaweza kufanyaje nipate nafuu
 
Habari mkuu.
Tumbo linakata sana hasa nikishamaliza kula na kunywa kimiminika chochote, maumivu yanakua makali sàna kushoto na kulia karibu na kiuna,

Pia naomba unijuze dawa ya tumbo kujaa gesi.

Asante.

Tumia Pantoprazole 40mg kila siku kwa wiki mbili.
 
Asante...

Lakini hiyo Retin A ni lotion kama zilivyo lotion zingine i.e Nivea,Cocoa au ina tofauti?
maanake kma ni lotion nilishaga zitumia sana lakin hakuna impact

Hii siyo lotion kama vipodozi zingine. Hii cream ni dawa.
 
Back
Top Bottom