issakwisa6810
JF-Expert Member
- Sep 5, 2014
- 309
- 84
Sijui kama in kawaida mbona hutokea Mara kwa Mara Ila ngozi iko hawaidaNi mwasho tu? je ngozi inaonekanaje?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijui kama in kawaida mbona hutokea Mara kwa Mara Ila ngozi iko hawaidaNi mwasho tu? je ngozi inaonekanaje?
Sijui kama in kawaida mbona hutokea Mara kwa Mara Ila ngozi iko hawaida
Habari wakuu,
Nakaribisha maswali yoyote kuhusu magonjwa, dawa, tiba na afya kwa ujumla. Kama una maswali kuhusu ugonjwa wowote, vipi kuishi na magonjwa, kufanya mabadiliko kwenye maisha baada yakupata ugonjwa, matibabu, matumizi ya dawa, matumizi ya dawa pamoja na dawa nyingine au athari zake.
Karibuni sana.
View attachment 361607
Kama umejibiwa maswali na mtu mwingine na haijakufaa ni kosa lako.
Mimi nitajibu maswali zote mwenyewe kama Daktari.
Elimika Juu ya Afya: Bofya Hapa
asante docta kwa ushauriMkuu, ushatumia dawa nyingi sana. Ushauri wangu ni huu:
1. Inaweza kuwa una allergy inayoleta shida hili, Ni vizuri nyumba unaoishi isikuwe na vumbi sana. Isafishwe na kupigwa deki ili kuondo vumbi.
2. Jaribu kuto lala chini ya pangaboi au A/C, inawezekana unapata tatizo hili kutokana na kupulizwa na hewa baridi usoni.
3. Tumia dawa hii: Fexofenadine 60mg kutwa mara mbili kwa muda wa wiki mbili. Alafu nipe mrejesho.
Asante.
Dawa za kushusha pressure za asili tafadhali
Hapa patanifaa siku zijazo.
Ebu ngoja ni subscribe huu uzi
Mimi sijajibiwa mpaka leo swali langu.. docta angalia posti za juu..
Mke wangu ana tatizo la watoto kufia tumboni..mimba ya kwanza ilifika miezi nane na pili ikafika miezi saba..pia akiwa mjamzito mtoto huwa hachezi tumboni.. pia hukosa hamu ya kula kwa muda mwingi wa ujauzito...mimba ya kwanza ilipoharibika aliambiwa kuwa tatizo halitaweza kujirudia, mimba ya pili akazalishwa mtoto mapema baada ya mimba kufika miezi nane.. mimba ya tatu ilipofika miezi saba mtoto akafia tumboni..je tatizo hilo litaishaje??
mkuu kuna dawa yoyote ya kuondoa uvimbe? au ni mpaka operesheni
Duh, hio hatari ...Ni wiki sasa,naskia kelele kwenye sikio la upande wa kulia tatizo linazidi sana muda wa usiku..lakini haliumi.
Dr. Sajjad Fazel mimi nina tatizo la kuwa na meno yenye rangi ya njano, hii sio asili ya meno yangu kwasababu miaka ya zamani meno yangu yalikuwa yana rangi nyeupe, kuna wakati nilikwenda kliniki ya meno kuyasafisha yakawa meupe kiasi, naomba unisaidie kama ipo dawa ya kusukutua mara kwa mara ambayo nitakuwa naitumia kuyafanya meno yangu kuwa meupe siku zote? Kuna wadau humu jamii forums walisema ukitumia baking powder inayotengenezeaga maandazi kwa kusukutua inasaidia kusafisha meno na kuwa meupe.
Dr. Sajjad Fazel mi nina tatizo la kuota "kijinyama" kati ya maungio ya mguu wa kulia na sehemu za siri(korodani). Hakiumi ila ukikibana na vidole ndo na sense maumivu yake.
Mwanzo nilikipuuza ila naona kadri siku zinavyosonga kinazidi kurefuka!
Je, hii ni hali ya kawaida tu?
Nifanyeje ili kipotee make huwa nafikiria siku moja nikikate na wembe lakini nahofia pengine naweza kutokwa na damu nyingi au kusababisha tatizo jingine kubwa zaidi.
Msaada tafadhari!