Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Za asubuh mkuu.... nina mpango wa kufuga kuku elfu 1 kwenye eneo moja.... wa kienyeji.

Naomba ushauri mkuu wa kitaalamu... vitu gani vya kuzingatia katika ukuaji na utagaji wao....

Na eneo ukubwa gani kitaalamu wanatosha.
Na chanzo gani muhimu na rahisi kwa woote kujikinga na magonjwa....?

Sent from "La -Vista"
 
Kuna ugonjwa wa kuku unafahamuka kama coryoza na pia huu mwingine unajulikana kama Chronic Respiratory Disease (CRD) ... ni nini kinga pamoja na chanjo na tiba ya magonjwa haya?
 
Ng"ombe basha huyoo
 
Nshukuru ngombe ameamka baada ya siku 14! It was hard work and despair! Kazi kubwa niliyonayo ni kurudisha afya yake. Doctor, nimlishe vipi aweze ku gain weight haraka. asante sana kwa ushauri wako. santetena.
 
Wote wana umri mmoja miaka mitatu mkuu!
Mkuu samahani kuingilia. Lakini nina swali/maoni kwanini usifanye uhamilishaji kwa chupa (Artificial Insermination) tu kuliko kufuga dume kwa gharama na bado hafanyi kazi.

Mbegu bora ni cheap na process nzima itakayo guarantee offspring uitakayo ni rahisi tu.

Daktari atanisaidia kama nimekosea mahali
 
Ndugu nina swali nisaidie kumuuliza huyu rafiki yako mfugaji.

Je
1. Anazingatia malisho kwa kilograms? Au anawajaza tu kila waliapo?
2. anawapa concetrates?
3. Anawapa japo nafasi ya kufanya mazoezi au ni 100% zero grazing?
4. Amewawekea lile jiwe la chumvi?
5. Vitu kama makiliki(sifahamu spellings zake) anawapa kuongeza joto?
6. Ratiba ya muda wa ukamuaji inazingatiwa?
7. Mlishi na mkamuaji wana uniforms? Hapa utajiuliza kwanini lakini naamini Dokta atakuelewesha zaidi ni kwanini, na wafugaji wengi wanafeli hapa ng'ombe anakata maziwa na wengine kuugua mastitis
8. Usafi wa mwili na malazi ya mifugo hayo yako?

Mkuu hayo yanachangia sana kwa mfugo huyo kutoku perform anavyotakiwa kuperform

Daktari nisaidie nilichosahau au nilichotia chumvi
 
Shukran kwa wazo zuri mkuu. Mm nafuga kuku wa kienyeji, ila kuna ugonjwa wa vifaranga kutokwa na vidonda mdomoni unanimalizia sana vifaranga wangu sana.

Kuna batch fulani waliugua huo ugonjwa nikamuona dr akaniambia unasababishwa na virus na hakuna tiba zaidi ya chanjo, ikanibidi batch iliyofuata nikapiga chanjo lakini vifaranga vyote vilikufa. Sasa sielewi nifanye nini na hivi karibuni kuku atatotoa vifaranga wengine. Je nini ushauri wako na tiba kabla ya hao wengine nnaotarajia kuwapata.
 
Ahsante Dokta kwa utayari wako kutuelimisha. Naomba kuuliza: Je, vifaranga wanatakiwa wakae siku ngapi ili wapate chanjo baada ya kutotolewa?, Je ni aina gani ya chanjo inafaa? (kuku wa kienyeji).
 
Kuna ugonjwa wa kuku unafahamuka kama coryoza na pia huu mwingine unajulikana kama Chronic Respiratory Disease (CRD) ... ni nini kinga pamoja na chanjo na tiba ya magonjwa haya?
Magonjwa hayo yote husababishwa na bacteria na yote husambulia mfumo mzima wa upuaji yaani respiratory system..

Coryza husababishwa na Haemophilus paragallinarum na bacteria huyu huenezwa kwa njia ya direct contact kupitia kuku anaeumwa ugonjwa huu na kuku ambao hawana ugonjwa huu or Indirect kupitia vyombo vya usafi vyenye bakteria hao...

Chronic respiratory disease ugonjwa huu Husababishwa na Mycoplasma gallisepticum huenezwa kwa njia ya transiovarian route kutoka kwa mama kwenda kwa vifaranga kupitia mayai na hii yaweza kupelekea wewe kununua vifaranga wenye huo ugonjwa na pia kwa wakubwa ni kupitia njia ya direct contact kama nilivyokwisha elezea hapo mwanzo....

Tiba yake ni kwa kutumia Antibiotic na pia kwa CRD yakupasa kununua vifaranga vilivyopewa chanjo ya kuzuia ugonjwa huo na vilevile hakikisha suala zima la management linazingatiwa vilivyo katika banda lako mkuu
 
Ahsante Dokta kwa utayari wako kutuelimisha. Naomba kuuliza: Je, vifaranga wanatakiwa wakae siku ngapi ili wapate chanjo baada ya kutotolewa?, Je ni aina gani ya chanjo inafaa? (kuku wa kienyeji).
Mkuu kwa day 1 old chick chanjo zinazotakiwa kuwakinga vifaranga wako dhidi ya magonjwa hatari ya bacteria na virus ni kama ifuatavyo ; Chanjo dhidi ya Chronic respiratory disease, salmonellosis, avian leukosis, avian encephalomyelitis na avian influenza thou kwa local breed wetu ni nadra sana kupata magonjwa hayo but kama uko ki commercial zaidi ni vyema ukawakinga mkuu coz siku zote wanakuambia Kinga ni nzuri zaidi kuliko tiba.... kila la kheri mkuu
 
labda ungeniambia unatumia system gani ya ufugaji mkuu.... either free range system or intensive system na ukiacha hiyo dalili ya vifaranga kutoka vidonda mdomoni ni dalili nyingine ipi wanaonesha tena mkuu? tuanzie kwanza hapo
 
Vipi magonjw ya bata mzinga ni yapi
Mkuu yapo magonjwa mengi tu kama vile Newcastle, typhoid, coryza, hemorrhagic enteritis, avian encephalomyelitis na infectious bursa disease....

sasa sijajua ulikuwa unataka maelezo ya ugonjwa gani hapo juu mkuu....
 
mkuu swali lako liko ki upana zaidi waweza nicheki pm for more detail
 
Mkuu hizi ni chanjo ama dawa ya kuwapa wakiwa na day1. Mimi navyojua chanjo ya Day 1ni Malek, then zingine zinafuata wiki kwa wiki ( Gombolo na Newcastle);

Kama ni chanjo je zinapatikana wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…