Mtaji wa 46M faida 540,000, pia mtaji wa 45M faida 576,000

Mkuu kama ndio unaanza biashara basi huo ni mwanzo mzuri sana
Hapo unapata darasa na uzoefu na discipline ya hela..... HONGERA

Hizi ndio biashara aina nzuri za kuanza kujifunzia biashara kwasababu risk ya kupata hasara ni ndogo japokuwa faida yake ni ndogo pia.

Usihamie kwenye biashara nyingine haraka haraka bila kufanya utafiti wa kina kwasababu umeambiwa ina faida kubwa, unaweza kwenda kuzika hela yako yote.

Kwa uzoefu unaoupata naamini utapata biashara nzuri na utakua na uzoefu.
 
Si bora ununue mashamba na kukata viwanja yaani hiyo M 45 utaidouble ndani ya miezi 3
 
Namashaka na wewe. Wewe sio mfanya biashara. Utakuwa umesikia story vijiweni. Biashara unayozungumzia hapo ni biashara ya jumla. (Whole sale) na biashara ya jumla huwezi kuuza mifuko 600 kwa miezi miwili. Huo ni uongo kabisa.

Biashara yoyote ya jumla ina faida ndogo ila ni pesa nyingi. Dukani kunakuwa ma bidha kama hizi kwa mfano.
1. Sukari kg 50 na kg 25
2. Ngano kg 50 na kg 25
3. Mafuta ya kula lita 20 na lita 10
4. Sabuni za unga packege za ujazo tofauti
5. Sabuni za miche makampuni tofauti
6. Dawa za meno. Colgate, whitedent mls tofauti tofauti
7. Bidhaa nyingine zote zinazopatikana kwenye maduka ya rejareja almaarufu maduka ya mangi.
Sasa huyu wa duka la jumla anauza bidhaa hizi kwa wateja wa duka la reja reja. Mteja akija kwa mfano ataandiksha vitu vifuatavyo.
1. Sukari kg 50 pc 1
2. Mafuta ya kula lt 20 pc 1
3. ngano kg 50 pc 1
4. Colgate gm 250 dozan 2
5. Majani ya chai gm 125 dozani 3
6. Omo sabuni za unga catton 2
7. Sigara bomba 1 sawa packet 10 moja
8. Pipi, big G, juice, pc 10 kila moja
9. Nk.
Huyu mteja mmoja akija hapa lazima amwachie huyu jamaa wa duka la jumla wastani wa tshs 10-15k kama faida. Akiwauzia wateja 25 tu kwa siku anapata wastani wa tshs 300k +. Unasemaje hapo hakuna faida?
Wewe mleta mada hujui chochote kuhusu biashara. Biashara kwa taarifa yako ina faida ndogo lakini pesa ni nyingi.

Ukija kwa hawa wa maduka ya rejareja. Akiwa na duka la kuuza wastani wa shilingi 300k wa siku, huyu jamaa kama atakuwa msimamizi mzuri baada ya miaka miwili, my friend humgusi.
Naandika kama mzoefu kwenye hili eneo. Nimewahi kuwa na duka la rejareja na ni mzoefu kwenda kununua kwenye haya maduka ya jumla.
 
Nikweli faida ni ndogo,
Ila kama huna nyingine endelea kufanya hiyo mpk upate nyingine
 
Uzoefu unaonyesha mfanya biashara msomi huwa anapata tabu sana kuendesha hizi biashara za kitaa. Sababu kubwa ni ujuaji wa kisomi. Unasema eti upeleke mchele tani 20 upate faida 1000000 huo ni ujua kama sio uwehu!!!
Mtu kama huyo na mimi mmoja wao pia najiwekea malengo. Kila tani 10 ya mchele nipate wastani wa shilingi 1,500,000. Na natakiwa niuze tani 40 ya mchele kwa mwezi. Hii ni kwa jumla na rejareja. Unakuta mtu ana store hapo dsm. Labda mbezi au kimara au Kule tegeta. Gongolamboto au kiwalani. Hapo sitaji mbagala wala tandika.

Kila wiki anapakia tani kumi. Mchele wa viwango tofauti. Kwa hiyo hapa lazima apate faida isiyopungua 6mls kama atapata 150 kwa kila kgm1. Mchele super huwa kupata faida ya kuanzia 300 kwa kg 1 ni jambo la kawaida kabisa. Hiyo sie tunaita ziada.
Huyu mtu unakuta sio msomi.kajiajiri. anapata milioni 6 kwa mwezi anakuwa amekosa nini?
Sasa msomi akija hapa anagundua ametumia jumla ya shilingi milioni 80 kwenye biashara na anapata 6mls kwa mwezi. Anaona ndogo....
Wakuu hamnaga pesa ndogo. Pesa inakuwa ndogo pale inaposhindwa kufanya jambo unalokusudia kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…