Mtaji wa 46M faida 540,000, pia mtaji wa 45M faida 576,000

Mkuu hii biashara nimeifanya sana, sio rahisi kama unavyotaka kuwaambia watu hapa!! Kwa soko letu hapa uniambie eti kilo moja upate net profit ya tsh. 300!!tena kwa mwezi uuze tani 40!!labda kama una tenda sehemu!! Lakini hii ya kupeleka kwenye ma store ya watu, hapana!! Faida ya mchele kama wewe ni risk taker, kachukue pesa DRC, kule hata tani 30 unaweza kuziuza ndani ya siku 3!!
 
Iko hivi. Nina wateja wangu. Ambao mara nyingi siwauzii mzigo kwa cash. Ninawapa mzigo wanauza kila baada ya siku 7 mpaka 10 wananilipa pesa. Hapa unatakiwa kuwa na mitaji miwili. Naongea nao kabisa. Unakuta mtu anakupa order ya magunia labda 9. Anakuambia niwekee mchele super gunia mbili, mzuri 3 ma mchele wa chini gunia 4. Kazi yangu ni kumtafutia. So nachukua order kwa wateja wangu wote. Kitendo tu cha kupakia tayari nishauza 85% ya mzigo. Unaobakia unashuka store. Kijana yupo pale anauza. Na ndie anayepokea mzigo na kuwasambazia wateja.

Mzee unashangaa mtu kupata faida ya 300 kwa kg kwa mchele super? hiyo iko wazi sana. Kwa super ni kawaida kabisa. Sema hii mingine ni kuanzia 100 ukipata sana 150.

Hapo kibaha kuna watu wanachapa kazj acha kabisa.
 
Kwa hivyo sawa!! Ila ndio hapo mitaji lazima uwe nayo miwili,
 
Acha nitumie ujuaji wa kisomi nawewe tumia ukilaza wako kila mtu ajivunie alichonacho.
Huo mchele unaotamka 80M unahitaji uanze na mtaji mkubwa ndio upate faida, ukianza na sijui milioni 15 unapata faida ndogo ambavyo ni muda mrefu kukua na risks zikija unaumia sana. Na sijaona mchele unaopata faida ya shilingi 300 kwa kilo, sanasana mara nyingi nimeona faida ambayo ni guaranteed ni shilingi 50 kama unataka ushushe gari mzigo uishe kabla haujaingia store. Au ukikaa kidogo ni 100 au 150, kuanzia 200 hiyo ni super profit ambayo haitokei muda wote. Ukitaka faida kubwa kuna usumbufu mkali na maandalizi mara ununue mpunga sijui uweke stock, umiliki gari lako. Hiyo ni ngumu na mtaji wake inabidi uanze mkubwa.

Meanwhile nilipoacha hiyo nikaja hii biashara, ukiwa na 80M unayosema hapa na ukapata net profit ya 6M kwa mwezi hata kama ni mara yako ya kwanza huna uzoefu wowote unastahili uchapwe viboko kwa uzembe. Na haisumbui kama mchele.
 
Unaona sasa. Hapa haukuanza biashara hapohapo unakopesha, ulitumia muda kwenye soko na ulianza kupata hizo faida baada ya kuwa na mitaji miwili. Mimi kwenye mchele nilipungukiwa mtaji nilioingia nao, nikaacha. Ni ama uje na mtaji mkubwa na sometimes usifanye cash deal, ama ugange njaa na mtaji mdogo.

Ukikopesha mtu unamnyima bargaining power unaongeza risk na faida. Ukiuza cash unapata faida ndogo, last time mchele nilokuja nao walitaka kununua bei sawa na niliyonunua mkoani nikakopesha maduka nikarudisha hela yangu nikaachana na mchele.
 
Hiyo hela mkuu ukienda nayo china ukanunua bidha ndani ya miezi miwili unapata hiyohiyo 46m so mtaji wako unazaa faida ya 46m njoo dm
 
malembeka18 kama una passport muda na huo mtaji Kuna safari ya wafanyabiashara imeandaliwa mwez April kwenda Canton fair china kama upo tayari njoo tujiset
 
Mkuu huko nifuate biashara ipi Sasa boss
Biashara n nyingi Mzee Kuna nguo, viatu, saa, heren, bangili, michezo ya watoto, vyombo, vipodozi, spea za pikipiki na magari, decoration za nyumbani na magari, nguo za ndani, mtumba hvyo vyote Mzee ukininua hata hapa bongo unapata zaidi ya 30% kama faida kwenye mtaji wako baada ya kutoa Kila kitu pia hapo Kuna bidhaa zingine ukiweka sh unapata sh Kuna machimho yapo hapa hapa East Africa.


Muhimu kujikaza na kujitoa akili pesa ipo sema ndio hvyo watu wana🔚🔜↔️
 
Nimesikia habari za ufuta huko Lindi
Ikifika mwenzi wa Sita.. nitafute Mzee nikuonyeshe chaka Uone watu wanavyokusanya pesa kwenye ufuta huku kusini. Utatamani kuiacha. Hizi siyo zama za magufuli za kuhulizana hii milion 200 kwenye account umeipata wapi?...nchi imefunguka hii watu wanapiga pesa hatari.
 
Wewe ndo unajua biashara sasa. Wasomi wanasahau sana kama 10 ilianza na 1.
 
Mimi pia nimesuspect hicho hicho. Yaani hio faida kwa hela anayowekeza ni lazima awe mtu ambaye hajui biashara. 46M kwa mtaji wa duka la jumla, ana double capital kwa mwaka tu. Hii ni speaking from experience kabisa.
 
Yaani mfuko wa sukari kg 25 faida iwe 900.?
Sasa anayeuza rejareja atapata sh ngapi.?

Huu ni uongo, labla kama sijaelewa mada.
Biashara ya jumla Ina faida kidogo kuliko ya rejareja.

Kinachofanya iwe nzuri ni kama kutakuwa na mzunguko mkubwa.
 
pole
 
We umesikia story kijiweni ukaja humu kupost uongo,huwezi ukawa na Mataji wa 46 mill na ukaleta mifuko 600,alafu uwe unauza mifuko 10 Kwa siku,kama ni kweli basi upo sehemu mbaya sana kibiashara na unatakiwa uhame hapo ulipo,wenzio wenye mtaji kama huo wanamaliza mzigo within a week,pia faida ya sukari Kwa Sasa ni kubwa sana,mfano mi Kwa Sasa sukari kg 25 naipata Kwa 70000 naiuza jumla 75000,tuache kusikia story tukajua ni kweli,Chamsingi ingia Kwa game
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…