Mtaji wa biashara zangu umeanza kukua, sasa naombeni mnisaidie jambo hili

Bado mtaji haujakuwa mzee. Wewe kama umeweza kufanya nao zikafika ml2 fanya nao zikue angalau ufike 10 hivyo hivyo. Kumbuka ukishaenda kufuata mwenyewe unapoteza ule uteja wenu unakuwa mshindan. Sasa kwa hiyo hela bado huna nguvu ya kushindana jipange kwanza usiwaonyeshe uwezo mapema
 
Mkuu ubarikiwe sana.

Huyo jamaa yako wa usafiri anaweza akawa anasafirisha kutoka madukani kupeleka Melini??
Yes. Kazi yake n kubeba mizigo kwa bajaji.
Kwaio hayo maduka yooote anayajua maana hua anapaki mitaaa hyo. So kazi yako n kulipia mzigo then ye atakuja aufuate anapeleka hadi hapo kwenye meli unasafiri na mzigo wako
 
Bei ya kiwandani ikoje mkuu na niwe na mtaji kiasi gani
Airtel pic moja ya Tsh 500 ni Tsh 470.....inamaana apo wewe unaweza ukawauzia watu wengine wa jumla kwa 478 au 490....kwa bei ya rejareja unauza 500

....ili uione faid andaa 3Ml adi 4Ml,uweze kuchkua pic zaid ya 10,000 [470×10,000] 4,700,000 apo kwa bei ya rejareja faida 300,000
 
Yes. Kazi yake n kubeba mizigo kwa bajaji.
Kwaio hayo maduka yooote anayajua maana hua anapaki mitaaa hyo. So kazi yako n kulipia mzigo then ye atakuja aufuate anapeleka hadi hapo kwenye meli unasafiri na mzigo wako
Kama hautojali, naomba mawasiliano yake pm for future use
 
Asante kwa ushauri wako mkuu.
Mimi nataka nichukue mzigo mwanza lakini nitakuja kuuza kwa reja reja, sijafikia kiwango cha kuuza jumla mkuu.

Asante
 
Kaka wazo zuri sana na hapo ndio faida utaiona... Mim nina kibanda tu nachukua mzigo takribani wa mil 1 kwa wiki yan, vocha, sigara, pombe kali, maji na visoda vya jambo ila unajikamua wiki nzima. Unaambulia faida laki tu
Laki kwa wiki au kwa mwezi?
 
Mi namshauri afanye vyote aendelee kununua kwa hao jamaa halafu kimya kimya awe ananunua mzigo mwingine mwanza
 
Mi namshauri afanye vyote aendelee kununua kwa hao jamaa halafu kimya kimya awe ananunua mzigo mwingine mwanza
Hujui principal za biashara Chief. Wakishagundua na watagundua tu kuwa kuna toleo jipya jiandae hata pale ulipokuwa unachukua mali kauli inakata. So kama umeweza kupandisha mtaji kwa muda mfupi piga kimya kimya ikifika Wakat wa kubadilika unakuta hata wakikubadilikia unakuwa uko salama kimtaji.
 
Pia uchunge matapeli wameshasoma mahitaji yako hapa hivyo watakutokea
 
Ni kweli, biashara huwa na mafuriko na kiangazi pia. Hivyo lazima uwe mtu wa research mara kwa mara uweze kupata njia ya ku escape wanapoku suprise.
 
Acha uoga. Kama anaweza kuchukua mzigo mwanza na akaongeza faida afanye hivyo. Kwenye biashara kinachoangaliwa ni kuongeza faida na kupunguza gharama. Hayo mambo ya kuogopa watu ni enzi za Nuhu huko. Na hata kama ukiwa mwema vipi lazima kuna watu wakuone nuksi tu. Huyu jamaa cha muhimu asivunje sheria za jamhuri na za Mungu.
 
Sina uoga mkuu mi nimetoa mawazo na tahadhari. Mi niko kwenye biashara miaka 30 hiv sasa. Nachosema hiyo kasi ya upandaji wa mtaji alitakiwa apande nayo kimya kimya maana bado hakuna kikwazo. Kuwajulisha watu ushalingana nao huku ukijua hujajipanga na matokeo yake ni kujiharibia. Ila haya mawazo sio sheria mi naongea kwa uzoefu wangu sio wake. Biashara sio kuuza na kununua tu ni pamoja na mazingira endelevu ya kuaminika. So kabla hujachukua hatua za juu zaid jipange usiwe na haraka. maana biashara kubwa zaid ni kuaminika kuwa mwaminifu.
 
Mkuu comment yako imejaa busara za hali ya juu ila mimi ninaona kama hana madeni kwa hao suppliers wake wa sasa hakuna madhara yoyote akiagiza Mwanza. Ila kama kuna ambao humpatia mzigo kwa mali kauli anaweza kuanza kutulia kwanza kwa muda kama ulivyosema. Milioni 2 bado ni hela ndogo.
 
Point hiyo au anza kubadilika kidogo kidogo unakuwa unachukua baadhi ya vitu mwanza vingne unachukua kwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…