Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Kwanini usianze na millioni tano hiyo tano, nyingine ikae pembeni uone mzunguko upoje.
Sawa. Lakini niliwaza kuweka yote kwa sababu ni mtaji usihitaji kununua kitu zaidi ya kulipa kodi na marekebisho ya ofisi tu.. kwa maana hata kama hakuna mzunguko kwa miezi 6 niliyolipa kodi kama uliweka 9m itabaki vile vile, kama sijakutana na wale matapeli
 
Fanya biashara ya kuuza vipuri vya pikipiki,bajaji,guta e.t.c utakuja kunishukuru
Biashara hii inahitaji angalau mtaji wa sh ngapi na return yake ikoje kwa mtaji utakaoupendekeza? Ikiwa tayar umeshalipia frem na kuiandaa
 
Biashara hii inahitaji angalau mtaji wa sh ngapi na return yake ikoje kwa mtaji utakaoupendekeza? Ikiwa tayar umeshalipia frem na kuiandaa
Milioni 10 mtaji, utavuna 1M to 1.5M kwa mwezi kama utakaa golini mwenyewe. Kama utaweka mfanyakazi toa gharama zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…