Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?


Mkuu km hayo maelezo hayalipiwi si uyaeke hapa tu
 

Kumbe cow nazo mpango mzima eeh? Ila vp kuhusu soko la hayo maziwa,,huwa yanaisha yote? Na vp kuhusu hzo cow kuugua na madawa yake?
 

Breweries wananunua zabibu? Wananunuaje?
 

Blue --- crystal clear ..... this is a real fact in any successful business

Red ----- sound not very far from reality .... 2m/10mx100 = 20% profit .....

mkuu 1701 ... please advice the forum members about your business idea
 
Last edited by a moderator:
Nenda pwani kanunue shamba heka tano is around laki 3 kwa heka jumla 1.5 utaspend utasafisha msitu kwa m1 kwa hizo heka tano then utalima kwa kila heka elfu45 kwa tr3ka then panda matikiti .Gharama jumla utatumia milioni 4.5 then utabakiwa na hakiba .Nenda mkuranga au kibaha.
 
kijana hebu leta pesa hiyo niiombee. baada ya hapo utapokea miujiza isiyo ya kawaida ya pesa!
 

mkuu kweli kazi za kusupply ugumu wake.lazima uwe na network..pili cash flow..tatu ukubali cheleweshewa malipo sometimes unaweza kuto lipwa hadi miezi miwili.wengi wameamua kuachana na mikataba ya Gpsa maana mtu mwaka mzima hana kazi
 
hao ng'ombe wenye mimba miezi sita wanapatikana wapi aisee kwa walioko dsm
 

Unamaanisha Cattering au nini?
Heb nishawishi nione
 
wanajamvi mimi nina milioni kumi nataka kuanzisha mradi wa kufuga kuku wa kienyeji nipo dodoma mjini kama una softcopy itakuwa vizuri zaidi
 
kiongozi business plan huwa inatofautiana kutokana na ainanya biashara au mradi mtu alio nao. Business plan ya mradi wa kuku ni tofauti ni plan ya mazao ya kilimo au mradi wa ujenzi jengo la biashara.
Na kutokana na umuhimu wa mpango wa biashara katika mradi wako itakuwa sio busara ukaokota mpangobwa biashara toka mtaani maana athari zake katika mradi wako ni kubwa.

Ni nini kifanyike basi.
waone wataalamu wa maswala ya business and financial consultancy. ukae nae uwaelezeebkwa kina ni nini unataka kufanya. wao watakuandikia mpango wa biashara utakaoendana na mazingira uliyonayo.

ukihitaji maelezo zaidi au mtaalamu unaweza ukapiga namba 0755815174
 
Reactions: Mbu
Wazo linguine la nyongeza mkuu ni hili, uko nje ulipo, angalia yafuatayo,

1.viwanda vya kutengeneza vyakula vya kuku-kama wanaweza kununua dagaa kutoka Tanzania.
2.Viwanda vyakutengeneza vyakula vya mifugo, na dawa za viatu kama kiw-ulizia kama wanaweza kununua mashudu ya alizeti kutoka tanzania
3. Viwanda vya kutengeneza viatu, mikoba, mikanda n.k- ulizia kama unaweza kuwa uzia ngozi za wanyama kama ngombe.
4. Viwanda vya kutengeneza taa za umeme, balb- ulizia kama wanaweza kununua kwato na pembe za ngombe.

Ukisha pata soko lake la uhakika, rudi jamvini kuomba watu wa kushirikiana nao ili kuongeza mtaji.bidhaa zote nilizo eleza kwa apa Tanzania zinapatikana sana. hivyo ukiomba watu wa kushirikiana nao uenda ukawapata na mimi naweza kuwa mmoja wapo kwa kuongeza zingine 10milion. na hivyo ukapeleka hata kwa kuanzia angalau contena moja.

ndo hayo tu mkuu. ubarikiwe
 
Reactions: Mbu
Mi mchango wangu ni huu ufuatao:
Kwanza nawashukuru wote mliochangia na pia mtoa mada.
Kwa hiyo million 10 unaweza kufanya biashara ya bajaji kwa miji kama mbeya, Iringa na Bukoba ni biashara inayolipa pia competition yake ipo chini...Mimi nimewahi kufanya kama dereva wa bajaji by mwaka 2012 niliona jinsi hiyo kitu ilivyo ila inahitaji usimamizi na kwa mtaji wako inabidi uchanganye wakati wa kununua hizo bajaji yaan nununua baadhi used na baadhi mpya hata ukianza na bajaji tatu si mbaya pesa itarudi
Pia kuna idea ya kufungua hizi college za masomo ya biashara na social studies pia kibongobongo naona it is a high rate growing business na watu wanazipenda coz we mwenyewe ni shaid jins wazazi wanavyosumbuka na watoto baada ya kumaliza form 4 na 6 na kukosa sifa au nafasi vyuoni...angalizo usifanye Hii kitu Dar competition ni kubwa mno coz kuna utitili wa colleges ila mikoani huku mambo safi kabisa
Mwisho kama utaipenda hiyo idea ya pili na kutaka kuifanya mi sina mtaji ila niko tayari kuisimamia na kukupa mwongozo na eneo na returns zake na jinsi ya kuiendesha najua una shaka na walimu hao very cheap tunawapata na mi ni mmoja wa walimu wazuri kwenye issue za business admin..
Mawazo yangu ni hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…