Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Ushauri utategemeana na namna ulivyoipata hiyo million kumi, Kama umeipata kwa mkupuo baada ya kuuza au zali, unastahili kuendeleza maada, Kama hiyo million kumi ni imeanza 01-10 wewe Leta mawazo ya biashara hapa upo vizuri
 
Wazo lilifaa mwaka 2005
 
Fungua duka la reja reja
Fungua mgahawa wa chakula
Fungua stationery
Fungua duka la dawa
Fungua duka la spea za pikipiki
Fungua duka la nafaka.
 
Napenda kuokoa pesa (saving money) nimeweza kufikisha kiasi cha shiling milion 8. Sasa napata wakati mgumu ni biashara gani naweza kuifanya kwa mtaji huu wa pesa.

Nahitaji kuwekeza huko kwenye biashara . Naombeni msaada wenu tusaidieni wengine.

Ahsanteni

======
Michango ya wadau

 

Ungeangalia kwanza unapenda nini kufanya biashara gani ukifanya utaifanya kwa moyo
 
Ungeangalia kwanza unapend nini kufanya biashara gani ukifanya utaifanya kwa moyo
Sawa ndugu nimekupata. Ila ninaamini kuna biashara ambayo naweza kunufaika nayo japo kwa mtaji kama wangu, nikiifanyia research na kuona inalipa nais ntaweza kubadilisha maisha kwa namna moja ama nyingine
 
Hapa ndio huwa changamoto mwenye pesa hajui biashara gani ya kufanya mwenye wazo la biashara hana mtaji wa kuanzia anyway! angalia ni kitu gani unachofikira kwa haraka na ukipendacho kufanya, biashara ziko nyingi depends na ww umefocus nini zaidi.Milion 8 ni nyingi kwenye biashara za kati lakini inaweza potea pia usipokuwa na malengo bora

IDEAS
1.Duka la nguo au vyombo
2.Kuuza matofali, kokoto na mchanga
3.Pub
4. Ufundi wa kushona nguo za kike na suti za kiume unanunua machine unaajiri mafundi wazuri.
5.Saloon ya kike au kiume standard kali tu
6.Car wash
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…