Kama ni wewe nakushauri unapotangaza mpira jaribu kukaza sauti, pia focus kwenye mchezo uwanjani na sio kuanza story za na maneno ya MIPASHO. Jifunze kwa manguli kama Chales Hilary. Pia fuatilia watangazaji wa ligi kubwa kama EPL au Laliga uone wenzako wanapojikita na yanayoendelea kwenye pitch.
Eti mtangazaji unatangaza mpira unaanza kusema " huyu Keita anazuia pale na kumuambia wewe siwezi kukuruhusu kirahisi unipite, kwanza hujui mimi ni kisiki cha mpingo waulize wenzako, mimi nimeaga kwetu na taifa linanitegemea kwahiyo hapa ni ngome ya vifaru na mizinga, huyu keita ni mzaliwa wa .... ni baba wa watoto watatu japo hii ni ndoa yake ya pili, pia kijiji Chao kinaitwa.....alikuwa kwa tabu sana huyu".
Imagine umbea wote huo anaoeleza wakati huo game inaendelea na haizungumzii. Halafu anarudi tena kwa mchezaji mwingine anaitwa labda Koulbaly utasikia " Koulbaly anapiga chenga pale anamuambia beki utanijua mimi ni nani, huyu ni mzaliwa wa kijiji kinachoitwa.... alianza mpira kwa kupelekwa academy na mjomba wake ambaye alikuwa na wanawake wanne"