Mtangazaji mpira Azam Tv anaboa sana

Sasa si uombe kazi ili ukatangaze wewe! Haya makasiriko yako yanakusaidia nini ndugu!!
 
Povu hilo,kama vipi kaombe hiyo kazi utangaze wewe maana una hasira sana
 
Hakuna mtangazaji anayependwa kama Nazareth upete na nurdin . Bongo ukiwa unatangaza kama unasoma risala Hakuna mtu wa kusikiliza watu wanapenda uweke na historia kidogo maneno maneno hio ndio nature ya wabongo vitu wanavyopenda kuvisikia
 
Sasa si uombe kazi ili ukatangaze wewe! Haya makasiriko yako yanakusaidia nini ndugu!!
Mmezoea porojo tu. And this is one of the weakness of Kiswahili language. Ni lugha maneno meeeengi halafu kilichomo hakijai hata kijiko, yaani ni kama furushi la pamba wakati uzito ni robo.
Hata vikao vinavyoendeshwa kwa kiswahili huchukua muda mrefu sana wakati agenda ni mbili tu. Fuatilia hata mijadala ya Bunge letu.

Nadhani hata ahadi za kujenga barabara, maji na Umeme huenda zingeshafaniwa kazi kama tu hizo ahadi zingetolewa kwa Lugha ya Kizungu

Kwa hiyo hata nyie watangazaji mnaotumia muda mwingi kupiga porojo msamehewe tu
 
Labda kama unashida na tune yake... Lakin ukija upande wa historia hata watangazaji wakubwa huko ulaya wanatabia za kutoa historia za wachezaji na binafsi navutiwa sana na inaonesha kuwa mtangazaji kabla ya Mechi kafanya homework yake vizuri
Tatizo wabongo english inatupiga chenga kwahiyo wakati tunaangalia epl au uefa tunakuwa hatuelewi kama kati kati ya utangazaji kuna kuongelea historia za wachezaji ndo maana tunawashangaa kina Nurdin maana wanatumia lugha yetu
 
Yote tisa,kumi ni mtangazaji wa Azam anayetangaza matangazo mubashara ya ligi kuu NBC wanamuita Pascal Kabombe (sijui kapombe) .Aisee jamaa huwa ananiboa sana ,hajui kutangaza na mipasho huwa mingi kuliko mpira anaoutangaza.
 
Halafu wanapenda kiingereza cha kachumbari huku hawakijui. Mara back left sijui back right
 
Sasa Bosi wangu mimi na utangazaji wapi na wapi! Mimi nimekushauri tu upunguze hasira.
 
Atakuwa mtu wa pwani au visiwani
 
Nurdin ukizingua tunakusema tu
 

Wale watangazaji wa mpira kwa lugha ya Kiingereza huwa unawasikiliza na kuwaelewa wakitangaza mathalani Premier League, WC, AFCON n.k?

Maana hata wao kuna muda huwa wanapiga soga kuhusu mchezaji au jambo lolote linalohusiana na mchezo/wachezaji husika...
 
Dah haya unayasema nimetoka kuyasikia jana usiku kwenye mechi ya DRC Congo vs Guinea. Yaani ni style ya kijinga haswa sijui kaipendea nini.
 
Nurdin Seleman anajua vizuri historia ya wachezaji,lakini swala la kutangaza kama anaimba kwangu naona jau.
 
Wanaboa Sana. Sema hawajui Kama wanaboa. Tangaza mpira achana na mambo mengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…