Mtangazaji na DJ wa East Africa Radio, Baba T atimiza miaka 81

Mara nyingi BabaT anatembea na miguu kutoka kwake Mbezi Africana nadra sana kupanda basi,si ajabu ndio maana ana umri mkubwa lakini ukimuona utadhani yupo miaka kati ya 55 na 60
 
Mwalimu Nyerere aliwaalika hata Wamarekani weusi na wengi wapo Kigamboni wengine wana mashamba ya kahawa Mbozi na wapo hadi leo,pale Kimara Mwisho kulikuwa na bucha moja maarufu na kisasa ilikuwa ikiitwa Little John ,hiyo bucha ilikuwa ya Mmarekani mweusi na washwahili washirika walimfanyia hila na akaamuriwa aondoke nchini,bucha ,ardhi na mali nyingine zikakombwa na waliokuwa washirika zake ambao walishindwa kuindesha bucha hiyo akina Sunday ,Rich Mlowo,
 
Hongera sana umejitunza vyema Mwenyezi Mungu akubariki sana
 
Inawezekana Tegeta ilikuwa ngome ya Rastafarian kwa mwendo huu ...
Yeah kila Jumamosi wanakutana kule Tegeta.

Yule Prof kwa sasa Marehemu.

Nadhani alikuja enzi za akina Prof. Walter Rodney.

Pale UDSM ukisoma mambo ya Development Studuies lazima usome kitabu cha Walter Rodney kinaitwa "How Europe Underdeveloped Africa".
Jamaa alikuwa na akili sana alipata PHD akiwa na miaka 24. Kazi yake iliyompa PHD ni hicho kitabu nilichokitaja hapo juu.

Waswahili hawaja anza majungu siku hizi!!
Hiyo dhambi itawatafuna tu.
 
Hbd rasta, Baba T anaheshimika sana huko kwao Jamaica, bday yake mwaka juzi konshen alimuimbia wimbo

Mbona nasikia Baba T ni Mchagga aisee....au nililishwa tango pori?Hebu tupeni verification..huyu ni mtu muhimu sana TZ hii.
 
Mbona nasikia Baba T ni Mchagga aisee....au nililishwa tango pori?Hebu tupeni verification..huyu ni mtu muhimu sana TZ hii.
Mkuu Baba T ni mjamaica alikuja na wenzie miaka ya 80 kuna wengine walisettle morogoro na wengine walienda kigoma, mwalimu aliwapa ardhi kubwa wafanyie shughuri zao, baadhi walirudi kwao baadae, hivi karibuni nilipata taarifa kuwa lile eneo lao la kigoma lilitaifishwa.
 
Mara ya mwisho naonana naye alikuwa anatimiza 80. Lakini nikijilinganisha naye najiona tayari nimeshajichokea wakati yeye ni mkubwa kuliko father wangu.
 

Duh..basi kuna kilaza mmoja aliniaminisha Baba T ni pure Mchagga....Hiyo story ya Wajamaica kuja TZ miaka hiyo naifahamu,kumbe na Baba T alikua mmoja wapo.Very interesting story!
 
Hivi nifanyeje kuwa vegetarian maana kuna wakati huwa nasiki mwili unataka ka nyama japo sipendi nyama ila samaki napenda sana
 
ulaji wa nyama sana na ngono za mara kwa mara zinachosha sana,mwili unatumia calories nyingi sana ku digest nyama mpaka iwe rahisi kuwa absorbable kuliko samaki na mbogamboga
Basi hapa nitaondoa nyama ila samaki nitaendelea nayo
 
Hahaha hiyo ya vipande vya nazi na chocolate itakuwa kuna kitu ameking'amua ndani ya eneo la kazi labda vijana wamekuwa hawako makini kwenda na wakati
 
Hii ya kuwagawia wanawake biskuti za chocolate na wanaume vipande vya nazi imekaaje hii? Mmeshawahi kumuuliza maana ya jambo hili? Au anamaanisha wanawake wakila hizo biskuti ndio wanakuwa watamu zaidi?
Mkuu huyu rasta anajua vyakula ambavyo ni dawa.

Nazi inaongeza libido kwa wanaume huna haja ya kula miti shamba mingi au dawa za hospital kuongeza nguvu za kiume.

Chocolate pia inatokana na nuts huongeza libido, sema hii ukila yenye sukari nyingi huongeza mwili kitu ambacho sio kizuri kwa mwanaume.
 
Mkuu

Media zetu zinashangaza sana
 
Mkuu

Acha nichume mlenda,kwanza nyama vyuma vimekaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…