TANZIA Mtangazaji nguli, Baba T wa East Africa Radio afariki dunia

TANZIA Mtangazaji nguli, Baba T wa East Africa Radio afariki dunia

Huyu ni mbongo mbona naonaga Kama ni mjamaika kutokana na ngeli yake
Ni mjamaika alikuja na wajamaika wenzake miaka ya Nyerere na waziri mkuu Michael Manley wa Jamaika walipokuwa wauumini wazuri wa Pan africanism, kipindi hicho hata wamarekani weusi wengi walihamia nchini,kuna walimu kama Walter Rodney, Prof Joshua Mkhululi , ndio akina Baba T na wenzake nawakumbuka hawa walikuwa na mgari wao kama wa kijeshi walikuwa wanaishi Mbezi Beach enzi hizo ikiwa pori na pia walikuwa na kikundi cha muziki wa reggea hawa waliwahamasisha Watanzania wengi kuwa marasta na pia walikuwa na falsafa ya kujitegemea na kuishi maisha ya kawaida sana, na walikuwa na uafrika ndani yao,hawa ndio waliofanya hata vijana marasta wa madale kuanzisha kijiji chao Madale na baadae wakahamia kijiji cha Mbigiri Morogoro kufanya shughuli za kilimo. Kule mbozi bado kuna wamarekani weusi, kule Kimara kulikuwa pia na wamrekani weusi kama Little John wa Kimara mwisho huyu alikuwa na bucha kubwa na ya kisasa sana lakini washwahili waliokuwa wafanyakazi wake wakamchomea utambi kwa mamlaka ili waitwae bucha yake na wakafanikiwa lakini kama ilivyo kwa washwahili wao kwa wao wakaanza kugombana na bucha ikafa na mali kupotea.
 
Mwanamajumui wa Afrika.....

Inna lillahi wainna illayhi rrajiuun!

Barukh atah Adonai Eloheinu melekh ha'olam dayan ha'emet 🙏🙏🙏
Hizi lugha za jangwani zinatamalaki sana siku hizi. Serikali inabidi liangalie hili swala kwa jicho la tatu ma kuingilia kati kwa kulishinikiza bunge itunge sheria ya dharura haraka sana kudhibiti hizi lugha before it's too late!

Dalmine kahtaan
 
Ujinga mzigo.....

Hivi unakuwaje na balozi wako aliye uarabuni asiyejua kiarabu?!!!😳

Hivi unakuwaje na balozi wako aliye Israel asiyejua Yiddish ?!!! 😳😳🤣🤣

Duuh yaani ndio akili zetu hizi?!!! 🤣🤣🤣

SIEMPRE JMT
 
Back
Top Bottom