Mtangazaji Paul James 'PJ' arejea Clouds FM

Mtangazaji Paul James 'PJ' arejea Clouds FM

Nilikua nawasikiliza kupitia tunein lakini kwanzia jana sikumsikia.... Hivi kwanini hamna misimamo nyie watu lkn? Kwahiyo Gerald nae karudi?
 
Mbona wazee wa mji tushajua EFM wamemnyakua Millard Ayo...hiyo inaitwa weka ugoko niweke jiwe.
 
Yawezekana ni ushamba wangu au umri, binafsi baadhi ya vipindi vingi vya Clouds FM sioni maudhui yake na faida chanya za kuijenga jamii yetu na kwa maendeleo ya taifa. Nadhani wangepewa nafasi ya kupromoti sanaa tuu, vingine waachie wengine

Endelea TBC taifa upate maudhui, maisha ya leo wanashida nyingi na wakati mwingine wanapenda vitu vya kipuuzi ili kuondoa stress. Neno lako la umri kuntu, ukiona hata mziki unachukia hujue ndio bye bye tena manake binadamu anaamini Zaidi alivyozoea.
 
Wakuu salamu.

Inasemekana PJ n Hando wamerudi tena Clouds fm. Waliondoka kwa mbwe mbwe sana kwenda Efm japo kwa maoni yangu hawakufanikiwa kufanya kile nilichotarajia! Lakini leo asubihi katika nyapia nyapia zangu pale Efm inasemekana PJ amekabidhi barua ya kuacha kazi na leo asubuhi ameonekana Clouds fm.

Hoja yangu ya msingi je Radio za Tanzania zimekosa kabisa kutengeneza damu mpyaa hadi kugombania watangazaji wale wale ambao kimsingi hawana jipya?

Niliona usajili wa Gadner pale Clouds kutoka Efm nao haukuleta jambo jipya sana kwenye jahazi! Ukiangalia kitakwimu bado Ubaoni ya Efm ndio yenye wasikilizaji wengi kwa mujibu GO nyakati za jioni. Ilitosha kwa Clouds kujifunza hilo kwamba sasa wanapaswa kuamini damu mpya.

Kingine cha kusikitisha kwenye radio hizi zimebakia kugombania watu maarufu na huku wenye taaluma hii wakiwa mtaani hawana kazi mfano mtu kama Gigy Money anakuwa mtangazaji kwa elimu ipi na kwa taaluma ipi?

Radio zetu hizi kubwa za Dar zinapaswa kuwaamini na kuwapandisha madaraja watangazaji wa Mikoani ambao ni wazuri kuliko hawa mjini wanao wasumbuaa.

Nimejiuliza sana mikataba ya hawa watu ipoje kama PJ ameweza rudi Clouds kijanja janja hivi na hata miaka miwili haijaisha.

.....Mwache arud lkn mi binafsi hata kama watangazaji wote wa Efm waende clouds kama siwez kuisikiliza hio radio...bora nisisikilize radio kuliko kusikiliza clouds...Pj nae kajishusha uthaman anakua kama "mtu yule" wa buguruni
 
kama wamerudi itakuwa poa mile kipindi kilipwaya sana Masood hana uelewa mpana Sizya mleta magazenga anamfunika
 
Yawezekana ni ushamba wangu au umri, binafsi baadhi ya vipindi vingi vya Clouds FM sioni maudhui yake na faida chanya za kuijenga jamii yetu na kwa maendeleo ya taifa. Nadhani wangepewa nafasi ya kupromoti sanaa tuu, vingine waachie wengine

Mimi sioni ulazima wa vipindi vya burudani kuwa na faida "chanya za kuijenga jamii yetu na kwa maendeleo ya taifa".

Hicho kituo [Clouds] ni cha kiburudani zaidi. Si kituo cha kujenga maadili kwenye jamii.

Na burudani pia ina nafasi yake katika jamii. Tupo tunaopenda kusahau kwa muda changamoto za maisha kwa kuburudika na mambo mbalimbali.
 
Kuanzia kesho nitabeba redio niendenayo kazini nikasikilize pb kwa sababu PJ is back again
 
Haya ndio matatizo ya kuwekeza kwa watu badala ya kuwekeza kwenye kipindi..Clouds walitakiwa kuwaamini watu hasa walio wakabidhi kipindi na wangewapa muda kuliko kuhangaika name mtu mmoja..! Walitakiwa kuwaamini wanao soma magazeti na ikiwezekana wawafundishe si lazima wafanye kama PJ lakini wanaweza fundishwa jinsi ya kusoma magazeti na kuchambua..

Media zinaangaishwa na mtangazaji mmoja badala ya kukuza walio nao ili kesho kama Fulani hayupo basi mwingine anachukua nafasi.

Mimi naamini baadhi ya media zinapaswa kujifunza kwa IPP maana wao wanawekeza kwenye vipindi zaidi na wanajua kuamini watu na kuwapa nafasi ndio maana tunaona wengi wanachukua watangazaji toka kwao maana wanajua kukuza vipaji na hawaamini kipindi kinaweza kufa kisa fulani kaondoka....nop.
 
Mimi sioni ulazima wa vipindi vya burudani kuwa na faida "chanya za kuijenga jamii yetu na kwa maendeleo ya taifa".

Hicho kituo [Clouds] ni cha kiburudani zaidi. Si kituo cha kujenga maadili kwenye jamii.

Na burudani pia ina nafasi yake katika jamii. Tupo tunaopenda kusahau kwa muda changamoto za maisha kwa kuburudika na mambo mbalimbali.
Inashangaza mtu anapotegemea Clouds Fm iwe kama TBC Fm.......Clouds TV iwe kama CNN.
 
Mimi naamini baadhi ya media zinapaswa kujifunza kwa IPP maana wao wanawekeza kwenye vipindi zaidi na wanajua kuamini watu na kuwapa nafasi ndio maana tunaona wengi wanachukua watangazaji toka kwao maana wanajua kukuza vipaji na hawaamini kipindi kinaweza kufa kisa fulani kaondoka....nop.
Daaah
We jamaa umeongea jambo la maana sana
Huwa najiuliza kwani hao EA radio huwa wana wezaje
Yaani kinatoka kitu kina ingia kitu
Ni suala la work ethics hasa hasa hapo nadhani
Na kipindi kikisha kuwa na producer mkali hata nikienda mimi ana nitengeneza ni fit na pindi lina songa
 
Back
Top Bottom