Yawezekana ni ushamba wangu au umri, binafsi baadhi ya vipindi vingi vya Clouds FM sioni maudhui yake na faida chanya za kuijenga jamii yetu na kwa maendeleo ya taifa. Nadhani wangepewa nafasi ya kupromoti sanaa tuu, vingine waachie wengine
Usiwe unasikiliza.Clouds
Leo Tena
XXL
Jahazi
Makele matupu tangu mwanzo mpaka mwisho,hakuna content yoyote
.....Mwache arud lkn mi binafsi hata kama watangazaji wote wa Efm waende clouds kama siwez kuisikiliza hio radio...bora nisisikilize radio kuliko kusikiliza clouds...Pj nae kajishusha uthaman anakua kama "mtu yule" wa buguruniWakuu salamu.
Inasemekana PJ n Hando wamerudi tena Clouds fm. Waliondoka kwa mbwe mbwe sana kwenda Efm japo kwa maoni yangu hawakufanikiwa kufanya kile nilichotarajia! Lakini leo asubihi katika nyapia nyapia zangu pale Efm inasemekana PJ amekabidhi barua ya kuacha kazi na leo asubuhi ameonekana Clouds fm.
Hoja yangu ya msingi je Radio za Tanzania zimekosa kabisa kutengeneza damu mpyaa hadi kugombania watangazaji wale wale ambao kimsingi hawana jipya?
Niliona usajili wa Gadner pale Clouds kutoka Efm nao haukuleta jambo jipya sana kwenye jahazi! Ukiangalia kitakwimu bado Ubaoni ya Efm ndio yenye wasikilizaji wengi kwa mujibu GO nyakati za jioni. Ilitosha kwa Clouds kujifunza hilo kwamba sasa wanapaswa kuamini damu mpya.
Kingine cha kusikitisha kwenye radio hizi zimebakia kugombania watu maarufu na huku wenye taaluma hii wakiwa mtaani hawana kazi mfano mtu kama Gigy Money anakuwa mtangazaji kwa elimu ipi na kwa taaluma ipi?
Radio zetu hizi kubwa za Dar zinapaswa kuwaamini na kuwapandisha madaraja watangazaji wa Mikoani ambao ni wazuri kuliko hawa mjini wanao wasumbuaa.
Nimejiuliza sana mikataba ya hawa watu ipoje kama PJ ameweza rudi Clouds kijanja janja hivi na hata miaka miwili haijaisha.
Hata Mpoki ni Bonge la msanii sio wa kumfananisha na Gigy Money.Zembwela anajua anachokifanya ni moja kati ya watangazaj wanaojitambua huwez kumweka level za kina gigy
Nshaa acha baada ya kugundua hiloUsiwe unasikiliza.
Yawezekana ni ushamba wangu au umri, binafsi baadhi ya vipindi vingi vya Clouds FM sioni maudhui yake na faida chanya za kuijenga jamii yetu na kwa maendeleo ya taifa. Nadhani wangepewa nafasi ya kupromoti sanaa tuu, vingine waachie wengine
Umefanya vyema coz haipendezi kusikiliza makelele cku nzima wkt kuna radio nyingi nchi hiiNshaa acha baada ya kugundua hilo
Inashangaza mtu anapotegemea Clouds Fm iwe kama TBC Fm.......Clouds TV iwe kama CNN.Mimi sioni ulazima wa vipindi vya burudani kuwa na faida "chanya za kuijenga jamii yetu na kwa maendeleo ya taifa".
Hicho kituo [Clouds] ni cha kiburudani zaidi. Si kituo cha kujenga maadili kwenye jamii.
Na burudani pia ina nafasi yake katika jamii. Tupo tunaopenda kusahau kwa muda changamoto za maisha kwa kuburudika na mambo mbalimbali.
DaaahMimi naamini baadhi ya media zinapaswa kujifunza kwa IPP maana wao wanawekeza kwenye vipindi zaidi na wanajua kuamini watu na kuwapa nafasi ndio maana tunaona wengi wanachukua watangazaji toka kwao maana wanajua kukuza vipaji na hawaamini kipindi kinaweza kufa kisa fulani kaondoka....nop.