Mimi alipo ondoka hapo Clouds nilipata wasaha wakusikiliza Clouds FM hasa kwenye uchambuzi wa magazeti kwakweli sijaona sababu ya kumrudisha zaidi ya kuona tuu wanashindwa kuwaamini watangazaji wao..jamaa walio kuwepo walikuwa wanafanya vyema tuu na wanachambua vizuri..
Kinacho waponza Clouds na E FM wamejikita kuwekeza kwenye witu kuliko kuwekeza zaidi kwenye content ya vipindi na maudhui.
lazima media zibadilike na ziwe na utaratibu wa kuandaa witu wao na kuwaamini.
Mimi nimekuwa nikiwatolea mfano IPP kwakuwa ni ukweli wamekuwa wakitoa nafasi kwa watangazaji wao bila kujali ana jina au lah..
waliondoka Kennedy na mamy baby lakini kipindi hakikufa..kaja binti anaitwa queen fif kipindi kimerudi kwenye moto...
juzi nilikuwa naangalia e-news kuna binti wamemuweka unaitwa Suzy hakika nikaamini wanajua kutoa nafasi..yule binti anajua sana...
ukisikiza e-drive kuna binti anaitwa scola ana kipaji balaa na kipindi kina contents nzuri sana..
media zimeendekeza ushamba wa Kugombea watangazaji baada ya kuwezesha walio nao na ndio maana wana walingia na kuwasumbua..