Uchaguzi 2020 Mtani wangu Tundu Lissu pokea huu 'Ukweli' wangu japo najua hujaambiwa na unaweza ukawauma Wakupendao

Watakaompigia kura Lisu ni wafuatao-
1.Wafanyakazi waliokosa nyongeza ya mishahara kwa miaka 5 ilihali gharama za maisha zineongezeka maradufu...
Walivyojaa msongo wa mawazo labda hata kujiandikisha hawakujiandikisha labda unadhani unaenda tu kupiga kura bila kujiandikisha?
 
Tayari CCM walishafanya 'Utafiti' wao wa ndani tena 'Kiumakini' kabisa na 'Kujiridhisha' kuwa wana uhakika wa Kura 8,000,000 ( Milioni Nane ) kutokana na 'Wanachama' wao
75% ya hao wanaccm mil 8 wameichoka ccm na wako tayari kumpigia Lisu kura.
 
Hili la msingi sana. Kulaumu tuuu na kulialia kwamba alipigwa risasi 85% ya speech ni wastage ya time.

Watu wana kiu kubwa kusikia kitu tofauti CHADEMA itafanya tofauti na CCM ya JPM. Muda wa kurekebisha bado upo though
Hakuna Jipya mkuu wataishia kufukuza Wana habari kwenye mikutano yao wakijiona wamesha chukua nchi
 
Sasa huo utafiti upo hivyo mbona wanakata wagombea? Huo utafiti ndio uli conclue ukiwa Mwana CCM lazima upigie kura CCM ?
Ila ukiwa Chadema uipigie Chadema? Hovyo
 
Nchi hii bana kwa kweli Ina Mambo mengi sana na watu wa aina yake.NEC wanatuambia Kuna wapiga kura 29milioni waliojiandikisha kupiga kura mwaka huu. CCMkwa mujibu wa pole pole inawanachama Kama 14 milioni,Je hao 15 milioni ni akina nani?
Ni wewe na wenzako
 
Mi nimejiandikisha mwaka huu sikuwa na kitambulisho cha kusajilia line ila sasa kura yangu inaenda chadema hata asiposhinda lisu sio mbaya
 
Leo wanafungua kampeni zao lakini wameshindwa kabisa kusema watafanya nini wakichaguliwa. Muda wote wanalaumu tu

Sasa watachaguliwaje kama wanaenguliwa hivo ni bora wameahirisha uzinduzi kutokana na hiyo engua engua ya wagombea wao
 
Bwashee nakubaliana na wewe mengi uliyosema ila naomba ufafanuzi zaidi pale ulipoandika " sana sana lissu atafanikiwa kuwajaza chuki na unafiki wafuasi wake" je ni chuki gani na unafiki upi uliomanisha?
 
Ungeleta na uzi wa namna gani wataweza kufanya siasa huku tume ya uchaguzi ikishiriki kuwahujumu.
 
sasa Kama wapiga kura wote tayari wanao kampeni wanafanya za nini? Je mwaka huu malori hayatahusika kubeba watu?
 
Kama watu hawakujiandikisha tume ya uchaguzi imewezaje kuandikisha watanzania wote wenye sifa za kupiga kura ?
 
Tupo pamoja Mkuu na siwalazimishi waufuate ila wauheshimu kama Mtazamo wangu Kwake na Kwao kama Chama Kikuu cha Upinzani hapa nchini.
Kama watu hawakujiandikisha tume imepata wapi wapiga kura million 29 ambayo ni nusu ya watanzania wote ?
 
Unachukua takwimu magumashi za 2015,hao 8M kamali wa 2015 Mkapa na Rwakatale Getrude ni sehemu yao? Au replacement yao imefanyika tayari?
 
Unachukua takwimu magumashi za 2015,hao 8M kamali wa 2015 Mkapa na Rwakatale Getrude ni sehemu yao? Au replacement yao imefanyika tayari?
Imefanyika na inaweza kuzidi hapo.anyway niwape pole,uzinduzi wa kampeni zenu umeingia dosari,mwanzo mbaya,mrekebishe makosa mapema,mnaweza kosa kura hata laki 5.
 
Please Genta umeeleweka vyema na uko very objective kwenye thread, usiichafue kwa kujibu vibaya.
 
Lile ndio kosa,na events za mwaka huu nazo zilikuwa ngumu,mara corona,mara mass exodus mara upungufu wa ajira,upungufu wa pesa mifukoni,tumbua tumbua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…