Uchaguzi 2020 Mtani wangu Tundu Lissu pokea huu 'Ukweli' wangu japo najua hujaambiwa na unaweza ukawauma Wakupendao

Uchaguzi 2020 Mtani wangu Tundu Lissu pokea huu 'Ukweli' wangu japo najua hujaambiwa na unaweza ukawauma Wakupendao

Watakaompigia kura Lisu ni wafuatao-
1.Wafanyakazi waliokosa nyongeza ya mishahara kwa miaka 5 ilihali gharama za maisha zineongezeka maradufu...
Walivyojaa msongo wa mawazo labda hata kujiandikisha hawakujiandikisha labda unadhani unaenda tu kupiga kura bila kujiandikisha?
 
Tayari CCM walishafanya 'Utafiti' wao wa ndani tena 'Kiumakini' kabisa na 'Kujiridhisha' kuwa wana uhakika wa Kura 8,000,000 ( Milioni Nane ) kutokana na 'Wanachama' wao
75% ya hao wanaccm mil 8 wameichoka ccm na wako tayari kumpigia Lisu kura.
 
Hili la msingi sana. Kulaumu tuuu na kulialia kwamba alipigwa risasi 85% ya speech ni wastage ya time.

Watu wana kiu kubwa kusikia kitu tofauti CHADEMA itafanya tofauti na CCM ya JPM. Muda wa kurekebisha bado upo though
Hakuna Jipya mkuu wataishia kufukuza Wana habari kwenye mikutano yao wakijiona wamesha chukua nchi
 
Nchi hii bana kwa kweli Ina Mambo mengi sana na watu wa aina yake.NEC wanatuambia Kuna wapiga kura 29milioni waliojiandikisha kupiga kura mwaka huu. CCMkwa mujibu wa pole pole inawanachama Kama 14 milioni,Je hao 15 milioni ni akina nani?
Ni wewe na wenzako
 
Mi nimejiandikisha mwaka huu sikuwa na kitambulisho cha kusajilia line ila sasa kura yangu inaenda chadema hata asiposhinda lisu sio mbaya
 
Leo wanafungua kampeni zao lakini wameshindwa kabisa kusema watafanya nini wakichaguliwa. Muda wote wanalaumu tu

Sasa watachaguliwaje kama wanaenguliwa hivo ni bora wameahirisha uzinduzi kutokana na hiyo engua engua ya wagombea wao
 
Kuna watu hawataki kwa makusudi kusikia maoni ya ushauri kutoka kwa wengine hapa JF.

Nilileta mada hapa inahusu kuwataka waanze kuzungumzia ilani yao ya uchaguzi wakakataa.

Nimekuwa naongelea jinsi upinzani unavyokosa mikakati na mipango ya jinsi ya kukabiliana na CCM bila kutusiana wala kutafutiana makosa ya kiuchochezi lakini imekuwa ni ngumu kueleweka.

Hili la mikakati, mbinu na mipango nimekuwa nikilipigia kelele kwa muda mrefu lakini nimekuwa sieleweki.

Upinzani hauwezi kuitoa CCM madarakani kirahisi kama mnavyojiaminisha.

Nimesema haya kama maoni ya kiuchambuzi lakini mtaniita wa Lumumba.

Upinzani uwe tayari kusikiliza ushauri na maoni mbadala.
Ungeleta na uzi wa namna gani wataweza kufanya siasa huku tume ya uchaguzi ikishiriki kuwahujumu.
 
Hivi niliposema kuwa CCM tayari walikuwa na Wanachama wao 8,000,000 ( Milioni Nane ) 'Kibindoni' na kwamba waliendelea tena 'Kuwatafuta' wengine hivyo ni 'obvious' kuwa kwa 'Mikakati' yao watakuwa 'wameongezeka' ulinielewa? Kuna Watu hapa kutokana na 'Upumbavu' wenu na Kupenda 'Kukurupuka' katika Kusoma 'Threads' zangu huwa mnanilazimisha niwe nawajibuni 'hovyo' tu. Kama huna 'Akili' usifungue 'Uzi' wagu.
sasa Kama wapiga kura wote tayari wanao kampeni wanafanya za nini? Je mwaka huu malori hayatahusika kubeba watu?
 
Na hilo ndio tatizo kubwa,mimi nakumbuka kuna wakati watu walikata tamaa ya mass exodus wabunge wa upinzani hasa Chadema wakihamia CCM.
Kitendo hicho kilikatisha tamaa wapiga kura wapya hawakuhamasishwa kisawa sawa.
Lakini kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi.
Kama watu hawakujiandikisha tume ya uchaguzi imewezaje kuandikisha watanzania wote wenye sifa za kupiga kura ?
 
Tupo pamoja Mkuu na siwalazimishi waufuate ila wauheshimu kama Mtazamo wangu Kwake na Kwao kama Chama Kikuu cha Upinzani hapa nchini.
Kama watu hawakujiandikisha tume imepata wapi wapiga kura million 29 ambayo ni nusu ya watanzania wote ?
 
Milioni 8 ni costant! Piga ua hiyo ipo ya wanachama kindakindaki,sasa chadema hawawezi kuipita hiyo hata wafanyaje.watabaki wanachama mil 6 kati ya 14,hao tutapata nusu,nusu watakuwa na vinyongo vya kuenguliwa.jumla mil 11.zitabaki kura 18 za wananchi kati ya milioni 29 za wapiga kura wote.hapo sasa ccm watavuna 90% ya wapiga kura mil18 ambayo ni kama mil16 na laki 2, ukijumlisha ccm watapata kura milion 27 .2.[emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji112][emoji112][emoji112]
Unachukua takwimu magumashi za 2015,hao 8M kamali wa 2015 Mkapa na Rwakatale Getrude ni sehemu yao? Au replacement yao imefanyika tayari?
 
Unachukua takwimu magumashi za 2015,hao 8M kamali wa 2015 Mkapa na Rwakatale Getrude ni sehemu yao? Au replacement yao imefanyika tayari?
Imefanyika na inaweza kuzidi hapo.anyway niwape pole,uzinduzi wa kampeni zenu umeingia dosari,mwanzo mbaya,mrekebishe makosa mapema,mnaweza kosa kura hata laki 5.
 
Hivi niliposema kuwa CCM tayari walikuwa na Wanachama wao 8,000,000 ( Milioni Nane ) 'Kibindoni' na kwamba waliendelea tena 'Kuwatafuta' wengine hivyo ni 'obvious' kuwa kwa 'Mikakati' yao watakuwa 'wameongezeka' ulinielewa? Kuna Watu hapa kutokana na 'Upumbavu' wenu na Kupenda 'Kukurupuka' katika Kusoma 'Threads' zangu huwa mnanilazimisha niwe nawajibuni 'hovyo' tu. Kama huna 'Akili' usifungue 'Uzi' wagu.
Please Genta umeeleweka vyema na uko very objective kwenye thread, usiichafue kwa kujibu vibaya.
 
Yeah ile hali ilikatisha wengi tamaa na kuona kupiga kura nikupoteza muda,na muda ule wa kwenda kujiandikisha ilionekana ni kupoteza tu muda,nikweli wapiga kura unaweza kuwabadilisha kwa muda mfupi ila ingependeza zaidi kungekuwa na kamtaji ka kuanzia
Lile ndio kosa,na events za mwaka huu nazo zilikuwa ngumu,mara corona,mara mass exodus mara upungufu wa ajira,upungufu wa pesa mifukoni,tumbua tumbua.
 
Back
Top Bottom