TANZIA Mtanzania afariki kwa kupigwa risasi South Africa

TANZIA Mtanzania afariki kwa kupigwa risasi South Africa

😭😭TANZIA TANZIA TANZIA 😭😭

Ndugu zangu ninawaletea taarifa ya msiba mwingine.

Tumempoteza ndugu yetu Mtanzania mwenzetu bwana MOHAMMED RAMADHANI aliyekuwa akiishi South Africa katika jiji la Cape Town jimbo la FLEY.

Ndugu yetu MOHAMMED amefariki usiku wa jana huko Cape Town kwa kupigwa risasi na mtu asiyejulikana. Kwa Tanzania anatokea mkoa wa Tanga.

Mbele yake nyuma yetu.
🙏🙏🙏
Anamuonekano wa kinunda alikuwa mwizi hiyo bila shaka
 
Africa Kusini sio mahali pa mtu kwenda kuishi, imekuwa nchi ya hovyo sana.
 
Ukienda nchi za watu jitahidi sana kuishi kwa umakini coz uki-mess up kidogo tu, unarudishwa kwenye ndege ya cargo.
Wao wenyewe kwa wenyewe wanapigana vyuma sana tu, hivi karibuni tu kuna rapa maarufu kapigwa risasi.
 
South tamu, na hizo hamsha hamsha za bunduki ndiyo zinafanya iwe sweeter.
Juzi namsoma jamaa mmoja, kapiga vita Yemen,then kaenda Afghanistan mwaka 2019 alipigwa risasi kidogo afe. baada Biden kuwatoa wanajeshi uko akarudi US, akaoa but Ndoa haikwenda vizuri, akaachana na mke wake. Mara vuuu Bakhmut hiyo, akaamua kubeba mabegi yake kwenda kutulia uko,hadi sasa yuko huko Bakhmut anawindana na warusi.
Anasema maisha ya vita kwake ni raha sana kuliko kitu kingine.
Haaa haaaa vita ni Raha ukiwa umeshawahi pigana mara kadhaa
Wewe
 
South tamu, na hizo hamsha hamsha za bunduki ndiyo zinafanya iwe sweeter.
Juzi namsoma jamaa mmoja, kapiga vita Yemen,then kaenda Afghanistan mwaka 2019 alipigwa risasi kidogo afe. baada Biden kuwatoa wanajeshi uko akarudi US, akaoa but Ndoa haikwenda vizuri, akaachana na mke wake. Mara vuuu Bakhmut hiyo, akaamua kubeba mabegi yake kwenda kutulia uko,hadi sasa yuko huko Bakhmut anawindana na warusi.
Anasema maisha ya vita kwake ni raha sana kuliko kitu kingine.
Huyo kamanda kama atachomoka hapo Bakhmut hafi tena vitani
 
South kwa sasa usalama mdogo sana. Kitendo cha kuonekana umeenda tu ATM ni hatari ya kifo. Ila wabongo wengi wanaoenda huko wana tabia mbaya. Wengi wao huku TZ walikuwa vibaka. Nawajua vijana kadhaa wa Mburahati & Kigogo waliokuwa vibaka hatari kwa sasa wanaishi South Afrika. Vijana kama wale nikisikia wamepigwa risasi sitashangaa kwasababu hata hapa Tanzania kilichowakimbiza ni kutafutwa na polisi.
 
Nilibahatika kuwepo hapo Cape Town mwaka mzima ( 2004 ) nikiwa nakaa jirani na aliyekuwa Mchezaji wa Santos FC Mkenya Musa Otieno.

Nilichokibaini hasa hapo Cape Town ukisikia Mtanzania Kauwawa / Kauliwa jua sababu Kuu moja wapo ni kati ya zifuatazo......

1. Kutembea / Kutia hovyo Wake za Makaburu ( Wazungu )

2. Kujiunga na Wauza Dawa za Kulevya kisha Kudhulumiana

3. Tabia ya Udokozi / Uwizi inayosifika kwa Wabongo wengi

Naitakia Kila la Kheri Yanga SC Kesho.
Tumeshapoteza SHABIKI mmoja wa kutushangilia!
 
Huyu bwana marehemu hiyo ishara tu aliyoionyesha kwenye picha inaashiria alikuwa ni mtu wa namna gani hiyo bila shaka ni Gang sign hivyo alikuwa ni Gang member
 
Yani mtu aisende kisa kuuliwa unaweza kufa umekaa bora kwenda tu
 
[emoji24][emoji24]TANZIA TANZIA TANZIA [emoji24][emoji24]

Ndugu zangu ninawaletea taarifa ya msiba mwingine.

Tumempoteza ndugu yetu Mtanzania mwenzetu bwana MOHAMMED RAMADHANI aliyekuwa akiishi South Africa katika jiji la Cape Town jimbo la FLEY.

Ndugu yetu MOHAMMED amefariki usiku wa jana huko Cape Town kwa kupigwa risasi na mtu asiyejulikana. Kwa Tanzania anatokea mkoa wa Tanga.

Mbele yake nyuma yetu.
[emoji120][emoji120][emoji120]View attachment 2624595
Jamii Forum mumeanza kukera. Kwa nini hamuoneshi picha kama zamani. Mnaleta habari nusu nusu!?
 
Back
Top Bottom