TANZIA Mtanzania afariki kwa kupigwa risasi South Africa

TANZIA Mtanzania afariki kwa kupigwa risasi South Africa

Daa sema dizonga kwa chuma dakika tu Rest easy brother..
Yaani Dizonga hakuna tofauti na USA kwa vyuma, utofauti wake kule utasikia mtu kavamia Mall au sehemu yoyote ya alaiki kaanza kutembeza chuma na Dizonga mtu mmoja mmoja wanarambana vyuma.
 
Africa Kusini sio mahali pa mtu kwenda kuishi, imekuwa nchi ya hovyo sana.
Mkuu tunao ndugu watanzania wanayoishi South kwa zaidi ya miaka 15 sasa na hatujawahi kusikia Jambo lolote limewatokea na wanaishi vizuri mpaka Sasa. Wengine wameoa huko na wengine wanarudi kuziona familia zao na kuwaletea dhawadi kedekede.
Kama alivyosema mdau mmoja, vijana wengi wa kibongo kule wanaojihusisha na issues illegally mpaka kupelekea kuuwawa. Sasa kwa mdau kama huyu (pichani) mwonekano wake na hata mahali alipopiga hiyo picha inakupa tafsiri gani?
 
Utashanga kusikia wabongo wenzake wanahusika!..wabongo wengi wanafanya mishe ambazo sio halali.
 
Na ni ujinga tu , wanapewa mzigo wanaambiwa kabisa e bana dola 5000 hiyo ulete anaitikia sawa.
Anauza anaanza kutumia km zake.
Siku jamaa wanarudi hela aah blah blah.
Analipa nusu nyingine katumia.
Wanamwambia kabisa tunarudi siku fulani.
Utupe hele iliyobaki au mzigo.
Wanarudi hadithi tena.
Sasa hapo wakiondoka wakirudi ni kukuchapa shaba tu.
Anakuwemo dereva na shubshooter ndani ya gari
Wanajua kijiwe chako
Na vinauliwa vinakuaga vitoto 20-25 year
Inasikitisha sana na wengi ni vijana wa Kizanzibari na Kitanga (Vitoto vya masheikh)
 
Mkiambiwa msiende south hamsikii
Kwani hata hapa watu hawauani mkuu. Unaweza ukafa ukiwa ndani mwako umelala ama upo sebuleni. Acha kuwapa wanaume hofu ya kutoenda kutafuta maisha waonapo ndipo mahala sahihi kwao kiutafutaji. Unajua welder wa bongo na sauzi,ama masonry unadhani mnafanana ama mnalipwa kwa rate sawa.
Wewe kaa Hapa hapa kijijini kwenu sijui mnapaita dar na ndio mnajiona Kama Ni mji na huku Ni kijijini Kama panakufaa sio kwa wote. Mtu akazaliwa dar akaishi mpaka akamaliza six Yuko dar anaziona balozi kibao unadhani atakosa nguvu ya kuwaza nje
 
Mwendo wa kuwatembezaa tu south sio bongo mazee kuishi kunahitaji mahesabu na utulivu wa hali ya juu..
 
😭😭TANZIA TANZIA TANZIA 😭😭

Ndugu zangu ninawaletea taarifa ya msiba mwingine.

Tumempoteza ndugu yetu Mtanzania mwenzetu bwana Mohammed Ramadhani aliyekuwa akiishi South Africa katika jiji la Cape Town jimbo la Fley.

Ndugu yetu Mohammed amefariki usiku wa jana huko Cape Town kwa kupigwa risasi na mtu asiyejulikana. Kwa Tanzania anatokea mkoa wa Tanga.

Mbele yake nyuma yetu.
🙏🙏🙏View attachment 2624595
Muuza Ngada
 
Back
Top Bottom