Uchaguzi 2020 Mtanzania amka: Wasanii kazi yao ni usanii, Kampeni za Uchaguzi Mkuu si usanii, hatuhitaji maigizo wala kukatiwa mauno!

Safi sana.nchi bado iko na shida nyingi sana zakijamii lakini hazisemwi tumekalia kuzungumzia mambo makubwa makubwa wakati madogo yakijamii tumeshindwa kuyafanya.safi sana kijana.
 
Dogo ahamishiwe kwenye team ya campaini ya raisi
 
Duuuh hadi mwili unasisimka. Lissu upgrade this boy and let him be in your campaign team .
 
Dogo yuko vizuri mno...Anajua kuongea na hadhira
 
Ameongea vyema lakini tatizo la vijana dizaini hii wa CHADEMA huwa hawakawii kununuliwa na kugeuka wanapokuwa "approached" na mawakala wa Magufuli.
 
Jukwaa ni sehemu ya kufafanua utatizi sio kuonyesha mauno Abarikiwe kijana wa Mwanza aunganishwe kwenye ziara ya Lisu
 

Ukitaka kujua uandishi kioja ndio huu. Kwamba huyo kijana wa CHADEMA katoa hotuba iliyobora kabisa! Kwa Sera zipi? Hivi, CHADEMA ina Sera wanazozinadi kwenye kampeni zaidi ya kudharilisha viongozi?

Aluu Mkuu Missile of the Nation ati kutembea na wasanii ni kuwasaulisha wapiga kura matatizo yao kupitia burudani. Du, yaani kwa uzoefu wako hujui nguvu ya wasanii kufikisha ujumbe kwa jamii? Pole sana.
 
Safi sana.nchi bado iko na shida nyingi sana zakijamii lakini hazisemwi tumekalia kuzungumzia mambo makubwa makubwa wakati madogo yakijamii tumeshindwa kuyafanya.safi sana kijana.
Ebu eleza mikakati ya kutatua shida zote za jamii pasipo kuwa na uchumi imara? Mtu kama wewe ndiye uota kuwa na ghorofa wakati hata mlo wa siku moja ni wa kubaghaiza.

Kwa kweli wafuasi wa CHADEMA humu JF ndiyo maana mwaitwa nyumbu. Kutwa kushabikia mada za kipuuzi zinazohusu watu na matukio.
 
Mpe masikini burudani asahau shida zake au vipi?
 
Hii ndiyo hotuba bora kabisa kutolewa tangu kampeni zianze
Aisee! Amenifikirisha! Hivi VIUNO VYA DIAMOND ndio utatuzi wa matatizo yetu? Halafu cha kufurahisha, wamewasajirisha wasani woooooooote maarufu, ili upande wa pili wasiwapate!
Ila kuna mmoja, KIBA naona pamoja na kutoa burudani, yeye kakataa KUVAA JEZI.
 
Huyu dogo ni msomi aliyeaumizwa na sera za CCM. Ana hasira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…