Uchaguzi 2020 Mtanzania amka: Wasanii kazi yao ni usanii, Kampeni za Uchaguzi Mkuu si usanii, hatuhitaji maigizo wala kukatiwa mauno!

Uchaguzi 2020 Mtanzania amka: Wasanii kazi yao ni usanii, Kampeni za Uchaguzi Mkuu si usanii, hatuhitaji maigizo wala kukatiwa mauno!

Kweli huyu kijana ametoa hotuba yenye hisia kali na yenye ujumbe mzito sana naweza kukubaliana na mleta uzi kuwa ni hotuba bora kabisa kutolewa katika kampeni za mwaka huu kwakweli. Kijana anajitambua sana
 
Chadema ni zaidi ya chuo kikuu!
Hakika CHADEMA kina watu wenye uwezo wa kujenga na kutetea hoja, ccm waendelee kuwahadaa watanzania tu, maana mtaji wao ni ujinga wa watanzania
 
Katika kinyang'anyiro cha ugombea ubunge, wagombea wengi sana wametoa hotuba zao.

Katika hotuba zote, iliyobora kabisa ni hotuba iliyotolewa na mpiga debe wa mgombea ubunge wa Chadema huko Mwanza katika Jimbo la Nyamagana huko Mwanza.

Kijana huyo amewakumbusha wapiga kura wake kuhusu umuhimu wa uchaguzi huu, amewaasa wote wanaodhani kuwa uchaguzi ni ama vile ushabiki wa mpira wa Simba na Yanga. Amewaambia kuwa uchaguzi unahusu ajira zao, pensheni zao n. k

Pia amewaasa wananchi kuwa Magufuli hana sera za kuwaambia wananchi ndiyo maana anazunguuka na wasanii ili kuwasahaulisha matatizo yao kupitia burudani. Akahoji kuwa kwani mauno ya Diamond yanasaidiaje kwa mfano wazee wetu kupata pensheni zao?

Kwa kweli inafurahisha kuwa TZ tuna baadhi ya wagombea vichwa, ambao naamini kama wakiingia bungeni watakuwa na mchango mzuri sana wa mawazo

Kwa taarifa zaidi angalia hotuba yenyewe hapa


Huyo ndugu anayeimba haya mashairi ni mtata sana... yafaa team Lissu wazungeke naye, kwa kweli mashairi yake yametulia sana.
 
Chadema ni chama makini sana.. wote vichwa.
Kiuhalisia CDM ni chama makini na wanachama wake karibia wote ni watu wenye akili timamu na wanaojitambua bila kujalisha umri au elimu yao.Wazalendo kweli kweli tofauti na CCM ambayo ni kokoro hasa,hata wenye akili nao wakiingia humo wanaondolewa kiungo muhimu-akili.
 
Wasije waka mu Alfonse mawazo huyokijana maana ccm hawachelewi kurusha mawe wakishindwa hoja
 
Mpe masikini burudani asahau shida zake au vipi?
Jibu ni kioja maana hapo ulipo husikiliza nyimbo za wasanii (injili, bongo flava, zuku, taarabu, singeli, nk) siyo tu kwa mziki wenyewe bali ujumbe uliomo kwenye tungo za wimbo, au?
 
Hot
Katika kinyang'anyiro cha ugombea ubunge, wagombea wengi sana wametoa hotuba zao.

Katika hotuba zote, iliyobora kabisa ni hotuba iliyotolewa na mpiga debe wa mgombea ubunge wa Chadema huko Mwanza katika Jimbo la Nyamagana huko Mwanza.

Kijana huyo amewakumbusha wapiga kura wake kuhusu umuhimu wa uchaguzi huu, amewaasa wote wanaodhani kuwa uchaguzi ni kama vile ushabiki wa mpira wa Simba na Yanga. Amewaambia kuwa uchaguzi unahusu ajira zao, pensheni zao n. k

Pia amewaasa wananchi kuwa Magufuli hana sera za kuwaambia wananchi ndiyo maana anazunguuka na wasanii ili kuwasahaulisha matatizo yao kupitia burudani. Akahoji kuwa kwani mauno ya Diamond yanasaidiaje kwa mfano wazee wetu kupata pensheni zao?

Kwa kweli inafurahisha kuwa TZ tuna baadhi ya vijana vichwa, ambao naamini kama wakiingia bungeni watakuwa na mchango mzuri sana wa mawazo

Kwa taarifa zaidi angalia hotuba yenyewe hapa


Kijana Yuko vizuri
 
Ngoja tuwasubiri waje kujibu hoja kama walivyoagizwa Na katibu wao
Nadhani twende zaidi ya hotuba i.e. maongezi /maneno twende kwenye kutenda. Tuliwachagua wapinzani wengi badala ya kutetea maslahi ya Nchi wanagombania ruzuku, uteuzi wa upendeleo (viti maalum), wameshindwa kuonyeshwa mfano wa uwazi wa mapato ya chama chao sembuse Nchi. Wanataka tujifungie ndani kwa ajili ya COVID-19 kwa kuwa mabeberu wanataka hivyo, ili mimi niwaamini waambie leo wajifungie kwa ajili ya KORONA! Maneno lazima yaendane na matendo vinginevyo ni makelele tu!
 
..Dr.Bashiru alisema mambo kama haya hayatakuwepo wakati wa kampeni.

..alisema wasanii wanaoimba na kughani kwa namna ambayo itawachoma mabeberu.

..sasa sijui kama " mauno mauno " ndiyo kuwachoma mabeberu.
 
😂😂 tafuteni kura sio kasoro chama kipi malaika nipisheni mie
 
Kuna jamaa yangu yupo kwenye timu ya kampeni za CCM kanda ya ziwa, ananiambia mpaka sasa ameshafukunyua pisi kama 15 hivi.

Na wanawake wote wapo kwenye kampeni, anawalamba tu, kwa ufupi kampeni za CCM sio salama kabisa,kuna uchafu mwingi sana
 
mala.ya sidhani kama watamsaidia jpm, ajitathimin abadili utaratibu.
 
Back
Top Bottom