TANZIA Mtanzania apigwa risasi na kufariki Afrika Kusini

TANZIA Mtanzania apigwa risasi na kufariki Afrika Kusini

Familia moja ya Kigogo, Dar es Salaam, inaomboleza kifo cha mtoto wao nchini Afrika Kusini. Ericky Ismael Ngobei, 22, aliuawa kwa kupigwa risasi Alhamisi iliyopita usiku katika eneo la biashara lenye watu wengi baada ya kuzozana na washambuliaji.

Ndugu wa marehemu amesema kuwa shambulio hilo lilitokea mwendo wa saa 11 jioni lakini hakuweza kubainisha ni katika mji gani. Kwa mujibu wa chanzo cha familia, kijana huyo alihamia Afrika Kusini hivi karibuni ambako aliajiriwa kama muuza duka.

Saa 11 jioni siku ya Alhamisi akiwa kazini, marehemu alikabiliwa na watu watatu ambao walitaka kuhudumiwa mara moja. Hata hivyo, Ngobei aliwaambia wawe na subira kwani alikuwa akiwahudumia wateja wengine katika eneo la biashara lililojaa watu.

"Katika ugomvi uliofuata, mmoja wao alichomoa bunduki na kumpiga risasi tumboni na kukimbia," jamaa wa karibu wa familia hiyo alisema. Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu inaratibiwa na wanajumuiya ya Watanzania nchini Afrika Kusini.

Very sad aise, hao waarabu ni makatili sana, walichomfanyia mwafrika mwenzetu sio kabisa.
 
Hata Kama watu wadogo ila fursa zipo nyingi sn pale.
_namibian dola na South Africa rand's ni thamani sawa.
_ kazi za kubangaiza mitaani zipo.

Hata mafundi cherehani pia wanapiga pesa.
Mafundi machenics.
Nk.
Raia wanapenda wageni.
Police wao sio wasumbufu.
Amani tupu pale.

Yote ya South Africa yapo pale.. watanzania wachache waliopo pale wanapiga pesa sn.
Mbona we huendi huko Namibia?
 
Nikajua Panyaroad wamehamia SA dooh pole sana marehemu astarehe kwa amani.,
Pole sana majeruhi, wafiwa, wazazi, ndugu, jamaa, marafiki na taifa kwa ujumla

Wallailai walailai walai rajun
Bwana alitoa bwana ametwaa
Jina lake lihimidiwe
Mwanga wa milele umpe ee bwana
Astarehe kwa Amana..
Wallailai walailai walai[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ignorance
Ignorance
Ignorance
Kufuata mkumbo
Kufuata mkumbo
Kufuata mkumbo
Ushamba
Ushamba
Ushamba
Note: ujinga ndio the biggest factor/reason inayowafanya wabongo waamini S.A inamaisha bora zaid yaTz, kama wasouth wangeikimbia hiyo nchi nani angewajengea? Ata mkoloni angeikimbia iyo South baada ya utumwa kuisha nan angeijenga? Resources ziko nyingi lkn wajinga hawaachi kuzikimbia nchi zao,

Elimu ndiyo mkombozi pekee kwa vichwa vya hawa wajinga waliokosa uzalendo
Columbus alikua mjinga?
Vasco Da Gama alikua mjinga? Hao makaburu wenyewe vipi? Maisha yanatafutwa popote ndugu yangu juzi kati mdada watu kauawa na vibaka kawe mzimuni tena nyumbani kwao tusiwakatishe tamaa explorers wetu
 
Familia moja ya Kigogo, Dar es Salaam, inaomboleza kifo cha mtoto wao nchini Afrika Kusini. Ericky Ismael Ngobei, 22, aliuawa kwa kupigwa risasi Alhamisi iliyopita usiku katika eneo la biashara lenye watu wengi baada ya kuzozana na washambuliaji.

Ndugu wa marehemu amesema kuwa shambulio hilo lilitokea mwendo wa saa 11 jioni lakini hakuweza kubainisha ni katika mji gani. Kwa mujibu wa chanzo cha familia, kijana huyo alihamia Afrika Kusini hivi karibuni ambako aliajiriwa kama muuza duka.

Saa 11 jioni siku ya Alhamisi akiwa kazini, marehemu alikabiliwa na watu watatu ambao walitaka kuhudumiwa mara moja. Hata hivyo, Ngobei aliwaambia wawe na subira kwani alikuwa akiwahudumia wateja wengine katika eneo la biashara lililojaa watu.

"Katika ugomvi uliofuata, mmoja wao alichomoa bunduki na kumpiga risasi tumboni na kukimbia," jamaa wa karibu wa familia hiyo alisema. Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu inaratibiwa na wanajumuiya ya Watanzania nchini Afrika Kusini.
Tokea nisome Ripoti Moja kuwa India na Afrika Kusini kila baada ya dakika Nne ( 4 ) kuna Tukio la Kiuhalifu na hata Mauwaji kutokea ( hutokea ) wala sijashangaa sana kwa hili na hii Taarifa kwani ni Kawaida na limeshazoeleka pia.
 
Hii nchi iko poa ila naambiwa maisha yake yapo juu sana ni kweli hama niliyemsikia alikuwa na porojo!.
Porojo tu ,,

South African's Rand na Namibian dollar zipo sawa.

Kuna fursa nyingi sana pale.

Population ya watu ni ndogo sana,
Inchi kubwa.
Wanapenda sn wageni.
 
Porojo tu ,,

South African's Rand na Namibian dollar zipo sawa.

Kuna fursa nyingi sana pale.
Population ya watu ni ndogo sana,
Inchi kubwa.
Wanapenda sn wageni.
Kabla ya yote; kama uliwahi kwenda ni vipi utaratibu wa Visa na getini (mnaita border) kwa wageni?.
 
Back
Top Bottom