KWELI Mtanzania Bara huruhusiwi kuendesha gari Zanzibar bila kuwa na kibali maalum

KWELI Mtanzania Bara huruhusiwi kuendesha gari Zanzibar bila kuwa na kibali maalum

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.

Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.

Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.

Huu Muungano ni wa kishenzi sana.

Bilikundi.jpg

Tunachokijua
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa Aprili 26, 1964 ikiwa ni Muungano wa Mataifa mawili huru ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo yaliingia mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964 huko Zanzibar.

images

Picha: Mwalimu Julius Nyerere (kushoto) na Sheikh Abeid Amani Karume (kulia) wakibadilishana Hati za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili, 1964.
Sababu ya Muungano
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwepo kutokana na sababu mbalimbali kama vile kuwepo kwa mahusiano ya karibu na ya kihistoria baina ya Tanganyika na Zanzibar katika nyanja mbalimbali kama vile undugu wa damu, biashara, utamaduni, lugha na mahusiano ya karibu kisiasa hususan baina ya vyama vya TANU na ASP.

Pamoja na kuwepo muungano lakini Tanganyika na Zanzibar hazikuungana kwenye kila jambo bali kwa baadhi ya mambo tu, hivyo kuwepo kwa mambo yahusuyo Muungano na ambayo hayahusu Muungano hivyo kila upande huyashughulikia bila kuhusisha Muungano.

Je, Mtu wa Tanzania bara anaruhusiwa kuendesha gari Zanzibar kwa kutumia leseni yake aliyopewa na TRA?

JamiiForums Imezungumza na Kamanda wa Polisi Ramadhani Ng'azi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, ambaye amekiri kuwa:

"Ni kweli mtu hawezi kutumia leseni yake aliyopewa na mamlaka ya Mapato Tanzania( TRA) kwasababu Mamlaka ya utoaji wa leseni sio jambo la kimuungano hivyo Mamlaka za utoaji wa Leseni kati ya Tanzania bara na Zanzibar zipo tofauti.

Tanzania bara Mamlaka inayotoa leseni ni TRA, baada ya kupata uthibitisho kutoka jeshi la Polisi kuwa mtu huyo amesomea udereva na amepitia mitihani ya polisi au utahini wa polisi na kupewa hati maalum ya kufaulu na kwamba mtu huyo anatakiwa kupatiwa daraja fulani la leseni.

Baada ya TRA kupokea taarifa ya uthibitisho kutoka Polisi hutoa leseni kulingana na maelekezo ya jeshi la polisi kikosi cha usalama Barabarani.

Lakini Zanzibar wao wana mamlaka yao ya utoaji leseni ambayo ni tofauti na huku Bara na ndio maana wameweka utaratibu mtu akitoka huku kwenda kule ataomba kibali maalum kwa kuwa mamlaka ya utoaji leseni siyo jambo la kimuungano.

Hivyo
mtu akienda Zanzibar ataomba kibali maalum na vivyo ivyo mtu akitoka Zanzibar kuja bara ataomba kibali maalum ili aweze kuendesha gari".

Pia, JamiiForums imezungumza na Abubakar Nassor Ali Mkuu wa Divisheni ya Upasishaji Madereva, Mamlaka ya usafiri na usalama barabarani Zanzibar, ambaye amesema kuwa:

"Kimsingi tunapozungumzia suala la usafirishaji, Tanzania tuna sheria 2 tofauti, zikiwa na lengo moja la udhibiti wa usalama barabarani. Huko bara mna sheria ile namba 30, ya mwaka 1973 (Road Traffic Act) lakini Zanzibar tuna sheria namba 7 ya mwaka 2003 kwa ivyo ni sheria 2 tofauti ila lengo ni moja la shughuli za usafirishaji.Na hii kutokana na jambo hili kutokuwa la kimuunano.

Kwa maana Zanzibar tuna sheria yetu, sheria hiyo ndio inashughulika na mambo mbalimbali ya leseni, na inamtaka dereva yeyote awe na leseni.

Sheria yetu inatuambia mtu yoyote ambaye atatoka nje ya nchi, inamtaka mwenye leseni ya udereva mbali na ile iliyotolewa na Msimamizi Mkuu wa usafiri barabarani( Mkurugenzi wa mamlaka na usalama Barabarani) kwenda kufanya jaribio au kuangalia afya au kufanya mtihani ili kupima uwezo wake wa uendeshaji chombo cha moto akiwa ndani ya nchi.

Kwa maana hiyo mtu yoyote ambaye atakuwa na leseni ya nje ya nchi( nje ya nchi hapa ni pamoja na Tanzania bara)
anatakiwa kukata permit, kwa hiyo kwetu mtu yoyote ambaye atakuwa anatokea bara maana yake anatokea nje ya nchi, na anatakiwa kukata Permit (kibali maalum) ambapo kwa sasa gharama yake ni 15,000 ambayo hudumu kwa miezi 3.

Na kwa yule ambaye atakuwa anataka kuendelea kukaa Zanzibar kwa muda mrefu zaidi au kuweka makazi ya kudumu basi ana uwezo wa kubadilisha leseni yake, yaani atakata leseni ya huku Zanzibar,( hatubatilishi leseni ila atabaki nayo ya bara na atapewa nyingine ya huku baada ya kufuata taratibu za kuchukua leseni huku)

Mtu atakayekiuka sheria hii na kuendesha bila leseni atakuwa ametenda kosa, Kosa la mtu kuendesha bila leseni hapa ni kwa wageni wote ( nchi nyingine pamoja na wa bara) adhabu yake ni faini ya dola zisizopungua 50 ambapo kwa sasa ni sawa 116,500".

bilikundi-jpg.2703699
JamiiForums baada ya kusoma mambo yahusuyo muungano na kujiridhisha kuwa suala la usafirshaji si la kimuungano na kuzungumza na mamlaka za usafirishaji pande zote 2 za muungano ambao wamekiri mtu anayetoka upande 1 kwenda mwingine anatakiwa kukata kibali maalum ivyo imejiridhisha kuwa ni kweli Mtu wa Tanzania bara haruhusiwi kuendesha gari Zanzibar mpaka akate kibali maalum(permit)
Wanzanzibari wasiotaka muungano ni wale masikini, vijana wa vijiweni

Ila 80% ya wanzanzibari waliopo bara hawataki kurudi kwao, wakafanye nini?? Wanaajiriwa bure, wanamiliki mashamba, biashara etc etc

Wanadanganywa Zanzibar itakua kama Dubai, wajiulize Shelisheli, Madagascar wamekua kama Dubai??

Uislam wa mtu mweusi hautajirishi bali unaongeza umaskini tu
 
Sasa kuambiwa we wa bara kumekuumiza nn aisee?
Mbona watu hmna hoja thabiti

Mm nimekaa sana tu bara mbona naona kawaida tu wakiniita mpemba

Mbona uko kwenu mnabaguana kwa makabila!

Unaongea nonsense kabisaaa

Normalize reading between the lines big man. Ubaguzi na matabaka huanzia kwenye majina watu wanayoitana na ndio maana majina kama gringo, nigga, mzungu na mengineyo yanaweza kuwa yanayotumika kuashiria uhalisia wa ethnicity ya mhusika ila huchukuliwa kama offensive yakitumika in most cases.

Kwetu Tanzania tuna makabila zaidi ya 126 na kwakua nchi yetu ndio home of pan-africanism, wala hatuoni noma kutaniana na kuitana "we mpemba, we msukuma, we muha" na kadhalika kwakua tumefundishwa utani na hivyo hatuchukulii uzito kama maeneo mengine ya dunia. Hata hivyo, name-calling has never been ideal anywhere in the world kwakua inapandikiza chembe chembe za migawanyiko na ubaguzi.

Wewe umeona tu kuitwa "mtu wa bara" hilo la "waDanganyika" hujaliona eti eeh? MUUNGANO HUU HAUNA USAWA NA MTU YOYOTE MWENYE AKILI TIMAMU HAHITAJI MIWANI KUONA HILI.
 
Huu ni muungano wa kipuuzi na wa kipekee kabisa hapa duniani. Na cha kushangaza maCCM bado yanaungangania kwa sababu finyu za kisiasa. Haya majamaa ni mapuuzi sana.
 
Huu muungano hata Mangungo angeukataa sijui Nyerere kwa nini aliwadekwza sana hawa wazanzibar
Nyerere hakuwa mtu smart kivile kama tunavyoaminishwa, ukitaka kujua hilo tazama watoto wake kama wana maajabu kiakili pamoja na privileges walizopata kwenye elimu na malezi yao. Baba yao kawa kiongozi kwa umri mdogo tu na exposure alikuwa nayo sio kusema aliwapatia ukubwani.
 
Walinda AMANI wa TANZANIA YETU PENDWA wakati mwingine tunawasema humu vibaya (sababu ya mambo ya hovyo ya wanasiasa wetu) mtusamehe

Ila msije mkaacha KUIKALIA ZANZIBARI, nawahakikishia siku mkiondoka itakua KITOVU CHA UGAIDI na JIHAD.
 
Siku huu Muungano utakapo vunjika. Hasara itakua kwa wananchi wa Zanzibar wa level ya kawaida.

Maana hakuna fursa watakamata hapa bara. Na waliopo hapa watatimuliwa.

Ndipo akili zitawakaa kua viongozi wao walikua wanawapotosha.

Ni ujinga kung'angania mipaka ilio wekwa na wakoloni inayo ounguza namna ya kujaminaa na majirani.

Ingekua sawa hata kama tungefungya mipaka yote ya EA kukawa na easy movement of people and goods.

Mkuu Mo

Mie nadhani una underestimate zanzibar na wazanzibari. Kumbuka sisi tulikuwa empire. once empire forever empire. Tuliitawala afrika mashariki yote. Zanzibar ni kama mti ulokatwa tu, shina lipo, pakipatika huduma zitakiwazo mti unachipua tena.

Zanzibar haifaidiki na chochote na tanganyika. na zaidi ya hapo Watanganyika hamutuwawezi wanzanzibari sababu kubwa ni hizi:

1. Sie wazanzibar tuna damu ya kutawala, wazanzibari ni colonialists by nature
nyie watanganyika muna damu ya kutawaliwa. Watanganyika ni subjects by nature.

wazanzibari ni waarabu, waarabu walioko aurabuni wataweza kufika zanzibar na kuitumilia fursa ya kibiashara iliopo na kujenga uchumi, ikiwa unajuwa mambo ya geographical economy unajuwa zanizbar ipo katika "very strategic location economically". Yaani zanzibar ipo katika eneo la aflrika kwa nje ya bara. fursa kubwa ni kwaba waafrika wote wamelala dororo. Kwahivyo export za viwada vya zanzibar zitaeleka africa nzima.

Watanganyika mutabaikisha na udini wenu huku mukiitajirisha serikali ya zanzibar.
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
hilarious.
 
Mkuu Anyisille

Marehemu Karume baada ya kushituka, marehemu Jumbe baada y akushituka, na Maalim Seif walijitahidi sana katika harakati za kuitowa zanzibar katika muungano, unaona watanganyika walivoing'ang'ania zanzibar.

Unafiki mkuu, ni mavazi ya wanasiasa, hata huko tanganyika ufukara wenu unatoka na unafiki mkubwa sana wa wanasiasa wenu.

Sisi tunaloomba kwamba nyie watanganyika mudai utaifa wenu, maana mpaka hivi ninavyondika nyie hamuna utaifa wetu. Tanzania si taifa ni muungano. kilichoungana ni nchi inaiyotwa zanzibar na ina serekali yake na nchi ilikuwa haijuilikani duniani. Narejea tena zanzibar imeungana na nchi isiyokuwepo duniani. nyie watanganyika hamuna nchi, mupo mupo munabutuwa burutwa tu na ccm . tafuteni nchi yenu kwanza.
Watu wa visiwani kinachowakwamisha ni kaunafiki Tu, na huu Mungano si kweli kwamba hamuupendi mwasema msichokiishi na kuishi msichosema.

Hiyo Ngoma na mduara wenu wa hatuutaki Muungano ukipigwa sasa wala hakuna wa kuwabishia Ila mmefyata kwa sababu mnazozijua
 
Huu muungano ni wa kipuuz sna
 
Sikulaimu mkuu

Watanganyika vichwa vyenu vimekufa zamani. Nyie sio watu wa ufahamu. Wala hamuwezi kufahamu. Poleni sana
Hapa ndipo napata shida Sana kuelewa hii slogani ya Wazenji kujisifu Kimaarifa then kutwa Kucha wakilia kuwa Yule aso na maarifa Mtanganyika amewakalia

Can you please be open inahere!
 
Mkuu Mo

Mie nadhani una underestimate zanzibar na wazanzibari. Kumbuka sisi tulikuwa empire. once empire forever empire. Tuliitawala afrika mashariki yote. Zanzibar ni kama mti ulokatwa tu, shina lipo, pakipatika huduma zitakiwazo mti unachipua tena.

Zanzibar haifaidiki na chochote na tanganyika. na zaidi ya hapo Watanganyika hamutuwawezi wanzanzibari sababu kubwa ni hizi:

1. Sie wazanzibar tuna damu ya kutawala, wazanzibari ni colonialists by nature
nyie watanganyika muna damu ya kutawaliwa. Watanganyika ni subjects by nature.

wazanzibari ni waarabu, waarabu walioko aurabuni wataweza kufika zanzibar na kuitumilia fursa ya kibiashara iliopo na kujenga uchumi, ikiwa unajuwa mambo ya geographical economy unajuwa zanizbar ipo katika "very strategic location economically". Yaani zanzibar ipo katika eneo la aflrika kwa nje ya bara. fursa kubwa ni kwaba waafrika wote wamelala dororo. Kwahivyo export za viwada vya zanzibar zitaeleka africa nzima.

Watanganyika mutabaikisha na udini wenu huku mukiitajirisha serikali ya zanzibar.

First off, Zanzibar haijawahi kuwa empire mkuu ilikua ni sultanate. Na kuhusu kauli yako ya "once an empire, forever an empire", ziko wapi Ottoman, Mongolian, Shongai na empire zinginezo leo hii?

Kingine, Zanzibar haijawahi kuitawala Afrika Mashariki yote bali pwani yake tu na hii haikuwa kwa muda mrefu na wala haikuwa kimabavu bali ni kiuchumi.

Eti "Zanzibar haifaidiki chochote na Tanganyika"😂 hata malaika wanakucheka huko waliko. Umeme mnatoa wapi? Mnakuja huku mnanunua mashamba na viwanja na mnajenga makazi yenu kwa amani tu, hii sio faida? Faida ni nyingi kiasi kwamba muda wa kuainisha yote hapa sina.

Hili suala la waZanzibari kuwa colonialists na kuwa waArabu😂 naomba nijibu kwa kucheka tu.
 
Pole Mleta mada kwa kuchelewa kujua hili.
Suala la kununua kibali cha udereva kwa watanganyika/foreigners wanaotaka kuendesha gari Zenji lipo miaka mingi sana mara ya kwanza nakutana nalo Zenji ilikuwa 2008.

Muungano wa kisiasa na kichawa tu hakuna kingine.
 
Back
Top Bottom