KWELI Mtanzania Bara huruhusiwi kuendesha gari Zanzibar bila kuwa na kibali maalum

KWELI Mtanzania Bara huruhusiwi kuendesha gari Zanzibar bila kuwa na kibali maalum

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.

Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.

Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.

Huu Muungano ni wa kishenzi sana.

Bilikundi.jpg

Tunachokijua
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa Aprili 26, 1964 ikiwa ni Muungano wa Mataifa mawili huru ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo yaliingia mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964 huko Zanzibar.

images

Picha: Mwalimu Julius Nyerere (kushoto) na Sheikh Abeid Amani Karume (kulia) wakibadilishana Hati za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili, 1964.
Sababu ya Muungano
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwepo kutokana na sababu mbalimbali kama vile kuwepo kwa mahusiano ya karibu na ya kihistoria baina ya Tanganyika na Zanzibar katika nyanja mbalimbali kama vile undugu wa damu, biashara, utamaduni, lugha na mahusiano ya karibu kisiasa hususan baina ya vyama vya TANU na ASP.

Pamoja na kuwepo muungano lakini Tanganyika na Zanzibar hazikuungana kwenye kila jambo bali kwa baadhi ya mambo tu, hivyo kuwepo kwa mambo yahusuyo Muungano na ambayo hayahusu Muungano hivyo kila upande huyashughulikia bila kuhusisha Muungano.

Je, Mtu wa Tanzania bara anaruhusiwa kuendesha gari Zanzibar kwa kutumia leseni yake aliyopewa na TRA?

JamiiForums Imezungumza na Kamanda wa Polisi Ramadhani Ng'azi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, ambaye amekiri kuwa:

"Ni kweli mtu hawezi kutumia leseni yake aliyopewa na mamlaka ya Mapato Tanzania( TRA) kwasababu Mamlaka ya utoaji wa leseni sio jambo la kimuungano hivyo Mamlaka za utoaji wa Leseni kati ya Tanzania bara na Zanzibar zipo tofauti.

Tanzania bara Mamlaka inayotoa leseni ni TRA, baada ya kupata uthibitisho kutoka jeshi la Polisi kuwa mtu huyo amesomea udereva na amepitia mitihani ya polisi au utahini wa polisi na kupewa hati maalum ya kufaulu na kwamba mtu huyo anatakiwa kupatiwa daraja fulani la leseni.

Baada ya TRA kupokea taarifa ya uthibitisho kutoka Polisi hutoa leseni kulingana na maelekezo ya jeshi la polisi kikosi cha usalama Barabarani.

Lakini Zanzibar wao wana mamlaka yao ya utoaji leseni ambayo ni tofauti na huku Bara na ndio maana wameweka utaratibu mtu akitoka huku kwenda kule ataomba kibali maalum kwa kuwa mamlaka ya utoaji leseni siyo jambo la kimuungano.

Hivyo
mtu akienda Zanzibar ataomba kibali maalum na vivyo ivyo mtu akitoka Zanzibar kuja bara ataomba kibali maalum ili aweze kuendesha gari".

Pia, JamiiForums imezungumza na Abubakar Nassor Ali Mkuu wa Divisheni ya Upasishaji Madereva, Mamlaka ya usafiri na usalama barabarani Zanzibar, ambaye amesema kuwa:

"Kimsingi tunapozungumzia suala la usafirishaji, Tanzania tuna sheria 2 tofauti, zikiwa na lengo moja la udhibiti wa usalama barabarani. Huko bara mna sheria ile namba 30, ya mwaka 1973 (Road Traffic Act) lakini Zanzibar tuna sheria namba 7 ya mwaka 2003 kwa ivyo ni sheria 2 tofauti ila lengo ni moja la shughuli za usafirishaji.Na hii kutokana na jambo hili kutokuwa la kimuunano.

Kwa maana Zanzibar tuna sheria yetu, sheria hiyo ndio inashughulika na mambo mbalimbali ya leseni, na inamtaka dereva yeyote awe na leseni.

Sheria yetu inatuambia mtu yoyote ambaye atatoka nje ya nchi, inamtaka mwenye leseni ya udereva mbali na ile iliyotolewa na Msimamizi Mkuu wa usafiri barabarani( Mkurugenzi wa mamlaka na usalama Barabarani) kwenda kufanya jaribio au kuangalia afya au kufanya mtihani ili kupima uwezo wake wa uendeshaji chombo cha moto akiwa ndani ya nchi.

Kwa maana hiyo mtu yoyote ambaye atakuwa na leseni ya nje ya nchi( nje ya nchi hapa ni pamoja na Tanzania bara)
anatakiwa kukata permit, kwa hiyo kwetu mtu yoyote ambaye atakuwa anatokea bara maana yake anatokea nje ya nchi, na anatakiwa kukata Permit (kibali maalum) ambapo kwa sasa gharama yake ni 15,000 ambayo hudumu kwa miezi 3.

Na kwa yule ambaye atakuwa anataka kuendelea kukaa Zanzibar kwa muda mrefu zaidi au kuweka makazi ya kudumu basi ana uwezo wa kubadilisha leseni yake, yaani atakata leseni ya huku Zanzibar,( hatubatilishi leseni ila atabaki nayo ya bara na atapewa nyingine ya huku baada ya kufuata taratibu za kuchukua leseni huku)

Mtu atakayekiuka sheria hii na kuendesha bila leseni atakuwa ametenda kosa, Kosa la mtu kuendesha bila leseni hapa ni kwa wageni wote ( nchi nyingine pamoja na wa bara) adhabu yake ni faini ya dola zisizopungua 50 ambapo kwa sasa ni sawa 116,500".

bilikundi-jpg.2703699
JamiiForums baada ya kusoma mambo yahusuyo muungano na kujiridhisha kuwa suala la usafirshaji si la kimuungano na kuzungumza na mamlaka za usafirishaji pande zote 2 za muungano ambao wamekiri mtu anayetoka upande 1 kwenda mwingine anatakiwa kukata kibali maalum ivyo imejiridhisha kuwa ni kweli Mtu wa Tanzania bara haruhusiwi kuendesha gari Zanzibar mpaka akate kibali maalum(permit)
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.

Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.

Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.

Huu Muungano ni wa kishenzi sana.

View attachment 2703699
Hii hatari kabisa. Huu muungano hapana
 
Nyerere hakuwa mtu smart kivile kama tunavyoaminishwa, ukitaka kujua hilo tazama watoto wake kama wana maajabu kiakili pamoja na privileges walizopata kwenye elimu na malezi yao. Baba yao kawa kiongozi kwa umri mdogo tu na exposure alikuwa nayo sio kusema aliwapatia ukubwani.
Nakubaliana na wewe.
 
Walinda AMANI wa TANZANIA YETU PENDWA wakati mwingine tunawasema humu vibaya (sababu ya mambo ya hovyo ya wanasiasa wetu) mtusamehe

Ila msije mkaacha KUIKALIA ZANZIBARI, nawahakikishia siku mkiondoka itakua KITOVU CHA UGAIDI na JIHAD.
Magaidi kwa nini hawaendi Comoro?
 
Mkuu Mo

Mie nadhani una underestimate zanzibar na wazanzibari. Kumbuka sisi tulikuwa empire. once empire forever empire. Tuliitawala afrika mashariki yote. Zanzibar ni kama mti ulokatwa tu, shina lipo, pakipatika huduma zitakiwazo mti unachipua tena.

Zanzibar haifaidiki na chochote na tanganyika. na zaidi ya hapo Watanganyika hamutuwawezi wanzanzibari sababu kubwa ni hizi:

1. Sie wazanzibar tuna damu ya kutawala, wazanzibari ni colonialists by nature
nyie watanganyika muna damu ya kutawaliwa. Watanganyika ni subjects by nature.

wazanzibari ni waarabu, waarabu walioko aurabuni wataweza kufika zanzibar na kuitumilia fursa ya kibiashara iliopo na kujenga uchumi, ikiwa unajuwa mambo ya geographical economy unajuwa zanizbar ipo katika "very strategic location economically". Yaani zanzibar ipo katika eneo la aflrika kwa nje ya bara. fursa kubwa ni kwaba waafrika wote wamelala dororo. Kwahivyo export za viwada vya zanzibar zitaeleka africa nzima.

Watanganyika mutabaikisha na udini wenu huku mukiitajirisha serikali ya zanzibar.
Eti wazanzibar ni waarabu
 
wazanzibar ni waarabu
Inawezekana kwa sababu Wapemba wengi ni Watoto wa kikeni si kiumeni ndiyo maana wengi hawana ubin wa kiasili wengi Wana ubin wa Kihindi, Kiyemeni, Kibangaladeshi, Kiarabu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ni Watoto wa dada zetu wa kounguja waliozaa na wageni lakini waunguja waliozaana wao kwa woa ndiyo unakuta wa ubini wa kiasili ie Makame, Mbalawa, Jecha,
 
Ndio maana wakasaini mkataba baina ya Tanzania na Zanzibar.
 
Kwani Zanzibar wana nini? Hizo jamii ni moja tabia zao ni sawa

Wanakuja huku wanachukua ajira zetu, wanachukua viwanja na mashamba yetu, watu wao wanashika nafasi serikalini, wanafunzi wao wanapewa mikopo yetu, umeme wetu tunagawana nao na madeni tunawasamehe tukijua ni wenzetu tuko nao pamoja ila kumbe wanaona tunawashobokea ndo maana wanakua na maneno ya kashfa na dharau.

Kuhusu sisi waTanganyika kutokumiliki ardhi kwao walau inaweza kuwa justified kwamba eneo lao ni dogo, ila kama mpaka driving license inayotolewa na JMT kwao haiko valid, maana ya kuungana ni nini sasa?
 
Makubwa. Ivi why even bother? Zenj is 0.1% ya Tanganyika and less than 2% of its pop and we have access to the ocean from Tanga, Pwani, Dar, Lindi na Mtwara; Yaani except ilo jina la Tanzania tunahitaji nn hasa from Zenj?🤐🤐🤐
 
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.

Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.

Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.

Huu Muungano ni wa kishenzi sana.

View attachment 2703699
Aisee
Tabu sana haya mambo
 
Makubwa. Ivi why even bother? Zenj is 0.1% ya Tanganyika and less than 2% of its pop and we have access to the ocean from Tanga, Pwani, Dar, Lindi na Mtwara; Yaani except ilo jina la Tanzania tunahitaji nn hasa from Zenj?🤐🤐🤐
Tunahitaji fairness.

Malalamiko dhidi ya Muungano yasipuuze bali yafanyiwekazi
 
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.

Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.

Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.

Huu Muungano ni wa kishenzi sana.

View attachment 2703699
Kwanza hakuna mtu anaitwa mtanganyika hapa duniani, au umechanganyikiwa?
 
Leseni ya Tanzania hairuhusiwi Zanzibar bila kibali ?

Swali langu kwani Zanzibar sio sehemu mojawapo ya Tanzania ?
unasikiliza wapumbavu? Hiyo picha ni ya nani, kwa hiyo ukitoka bara ndio uitwe foreigner? watu hawamwogopi hata Mungu ni wazushi wa kipuuzi. We kwa akili yako uliona wapi mtu amesafirisha gari yake kutoka bara kwenda Zanzibar ili akaiendeshee kule. Wanajaribu kupandikiza chuki za kipumbavu ila ukiwa na akili utawagundua, ukiwa zuzu km wao utaingia kingi
 
Back
Top Bottom