KWELI Mtanzania Bara huruhusiwi kuendesha gari Zanzibar bila kuwa na kibali maalum

KWELI Mtanzania Bara huruhusiwi kuendesha gari Zanzibar bila kuwa na kibali maalum

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.

Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.

Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.

Huu Muungano ni wa kishenzi sana.

Bilikundi.jpg

 
Tunachokijua
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa Aprili 26, 1964 ikiwa ni Muungano wa Mataifa mawili huru ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo yaliingia mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964 huko Zanzibar.

images

Picha: Mwalimu Julius Nyerere (kushoto) na Sheikh Abeid Amani Karume (kulia) wakibadilishana Hati za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili, 1964.
Sababu ya Muungano
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwepo kutokana na sababu mbalimbali kama vile kuwepo kwa mahusiano ya karibu na ya kihistoria baina ya Tanganyika na Zanzibar katika nyanja mbalimbali kama vile undugu wa damu, biashara, utamaduni, lugha na mahusiano ya karibu kisiasa hususan baina ya vyama vya TANU na ASP.

Pamoja na kuwepo muungano lakini Tanganyika na Zanzibar hazikuungana kwenye kila jambo bali kwa baadhi ya mambo tu, hivyo kuwepo kwa mambo yahusuyo Muungano na ambayo hayahusu Muungano hivyo kila upande huyashughulikia bila kuhusisha Muungano.

Je, Mtu wa Tanzania bara anaruhusiwa kuendesha gari Zanzibar kwa kutumia leseni yake aliyopewa na TRA?

JamiiForums Imezungumza na Kamanda wa Polisi Ramadhani Ng'azi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, ambaye amekiri kuwa:

"Ni kweli mtu hawezi kutumia leseni yake aliyopewa na mamlaka ya Mapato Tanzania( TRA) kwasababu Mamlaka ya utoaji wa leseni sio jambo la kimuungano hivyo Mamlaka za utoaji wa Leseni kati ya Tanzania bara na Zanzibar zipo tofauti.

Tanzania bara Mamlaka inayotoa leseni ni TRA, baada ya kupata uthibitisho kutoka jeshi la Polisi kuwa mtu huyo amesomea udereva na amepitia mitihani ya polisi au utahini wa polisi na kupewa hati maalum ya kufaulu na kwamba mtu huyo anatakiwa kupatiwa daraja fulani la leseni.

Baada ya TRA kupokea taarifa ya uthibitisho kutoka Polisi hutoa leseni kulingana na maelekezo ya jeshi la polisi kikosi cha usalama Barabarani.

Lakini Zanzibar wao wana mamlaka yao ya utoaji leseni ambayo ni tofauti na huku Bara na ndio maana wameweka utaratibu mtu akitoka huku kwenda kule ataomba kibali maalum kwa kuwa mamlaka ya utoaji leseni siyo jambo la kimuungano.

Hivyo
mtu akienda Zanzibar ataomba kibali maalum na vivyo ivyo mtu akitoka Zanzibar kuja bara ataomba kibali maalum ili aweze kuendesha gari".


Pia, JamiiForums imezungumza na Abubakar Nassor Ali Mkuu wa Divisheni ya Upasishaji Madereva, Mamlaka ya usafiri na usalama barabarani Zanzibar, ambaye amesema kuwa:

"Kimsingi tunapozungumzia suala la usafirishaji, Tanzania tuna sheria 2 tofauti, zikiwa na lengo moja la udhibiti wa usalama barabarani. Huko bara mna sheria ile namba 30, ya mwaka 1973 (Road Traffic Act) lakini Zanzibar tuna sheria namba 7 ya mwaka 2003 kwa ivyo ni sheria 2 tofauti ila lengo ni moja la shughuli za usafirishaji.Na hii kutokana na jambo hili kutokuwa la kimuunano.

Kwa maana Zanzibar tuna sheria yetu, sheria hiyo ndio inashughulika na mambo mbalimbali ya leseni, na inamtaka dereva yeyote awe na leseni.

Sheria yetu inatuambia mtu yoyote ambaye atatoka nje ya nchi, inamtaka mwenye leseni ya udereva mbali na ile iliyotolewa na Msimamizi Mkuu wa usafiri barabarani( Mkurugenzi wa mamlaka na usalama Barabarani) kwenda kufanya jaribio au kuangalia afya au kufanya mtihani ili kupima uwezo wake wa uendeshaji chombo cha moto akiwa ndani ya nchi.

Kwa maana hiyo mtu yoyote ambaye atakuwa na leseni ya nje ya nchi( nje ya nchi hapa ni pamoja na Tanzania bara)
anatakiwa kukata permit, kwa hiyo kwetu mtu yoyote ambaye atakuwa anatokea bara maana yake anatokea nje ya nchi, na anatakiwa kukata Permit (kibali maalum) ambapo kwa sasa gharama yake ni 15,000 ambayo hudumu kwa miezi 3.

Na kwa yule ambaye atakuwa anataka kuendelea kukaa Zanzibar kwa muda mrefu zaidi au kuweka makazi ya kudumu basi ana uwezo wa kubadilisha leseni yake, yaani atakata leseni ya huku Zanzibar,( hatubatilishi leseni ila atabaki nayo ya bara na atapewa nyingine ya huku baada ya kufuata taratibu za kuchukua leseni huku)

Mtu atakayekiuka sheria hii na kuendesha bila leseni atakuwa ametenda kosa, Kosa la mtu kuendesha bila leseni hapa ni kwa wageni wote ( nchi nyingine pamoja na wa bara) adhabu yake ni faini ya dola zisizopungua 50 ambapo kwa sasa ni sawa 116,500".


bilikundi-jpg.2703699
JamiiForums baada ya kusoma mambo yahusuyo muungano na kujiridhisha kuwa suala la usafirshaji si la kimuungano na kuzungumza na mamlaka za usafirishaji pande zote 2 za muungano ambao wamekiri mtu anayetoka upande 1 kwenda mwingine anatakiwa kukata kibali maalum ivyo imejiridhisha kuwa ni kweli Mtu wa Tanzania bara haruhusiwi kuendesha gari Zanzibar mpaka akate kibali maalum(permit)
AY 5225

Tulia nikujibu, tatizo sijui ukubwa wa ufahamu wako wa mambo ya dunia. Lakini hatahivyo nitakujibu upate kucheka. Nitakwenda deep kidogo, ikiwa ni above your capacity utaniwiya radhi kwa hilo.

"mumeshidwa, hamuna, mulikuwa, mukitawalia, mutarudi"

Aisee! unanipa tabu sana kusoma, ningekuwa naongea na mCongo angalau ningejitahidi kuvumilia. Yote kwa yote, hakijaharibika kitu hivyo naomba tuendelee na darasa letu.

2. Hakuna mahala popote katika historia ya nchi yangu panaposema the so called Zenj empire ilikuwa mtawala wetu na Afrika mashariki yote. Hata reign ya Sultan ilikua na kauli kwa baadhi tu ya miji ambayo yote ipo ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki na si vinginevyo.

Nimeona pia umeandika kwamba hatuna historia wala uzoefu wa kujitawala. Kauli hii imenifanya nizidi kukuona ni mtupu kichwani, na wahenga wanasema kichwa kisicho na akili ni mzigo kwa shingo. Nina wapwa wangu wako darasa la 3 na wengine la 5 na 6 na wote wanajua kuhusu uwepo wa Chiefdoms zenye nguvu nchini Tanganyika kabla hata ya ukoloni kufikiriwa kuanzishwa. Nenda kasome kuhusu makabila kama waHehe, waChagga, waYao, waNyamwezi na mengine mengi itakusaidia kuondokana na tatizo lako la kutumia kichwa kama kizibo ama kifuniko cha mwili na si kiungo chenye uwezo wa kuchanganua mambo.

It's so unfortunate that the same can not be said about Zanzibar. Hakujawahi kuwepo na mtawala yoyote mashuhuri aliewahi kuleta utofauti kabla na arguably, hata baada ya zama za utumwa.
 
Tanzania ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Bahati mbaya Zanzibar ipo hai wakati Nchi ya Tanganyika ilishakufa baada ya 1964.

Iwapo Nchi ya Tanganyika ingekuwa hai ina maana Mzanzibari ili aendeshe gari Nchi ya Tanganyika angelazimika kuomba kibali pia.

Tanganyika irudi tu
 
AY 5225

Tulia nikujibu, tatizo sijui ukubwa wa ufahamu wako wa mambo ya dunia. Lakini hatahivyo nitakujibu upate kucheka. Nitakwenda deep kidogo, ikiwa ni above your capacity utaniwiya radhi kwa hilo.

1 Kwanza Sultanate haikuwa Empire, Zenj Empire, ndio ilokuwa Empire. Sultanate ilikuwa Serikali ya zanzibar. Ingawaje ni anganyika mutarudi tena katika himaya yetu.


3. Mkuu sidhani kama tafsiri ya neno faida ni jambo ambalo linahitaji mjadala ila naomba kuuliza kwako wewe, faida unaitafsiri kwa namna gani? Faida ya muda mrefu na faida ya muda mfupi zote kwa ujumla wake ni aina za faida.

Umesema pia kwamba sisi Tanganyika ni hohehahe (japo umeandika "muko hahe hoe"😂nimetumia jitihada za ziada kuelewa ulicho maanisha ndugu mjuzi wa mambo), lakini nimetoka juzi juzi Zanzibar umeme unakatika mpaka masaa 8 haurudi na nikaambiwa pia mna historia ya kukaa miezi mitatu bila umeme na hii ni karne ya 21, hohehahe ni nani kati yetu? Rasilimali zetu ambazo hazijawa fully harnessed kuweza kukidhi mahitaji ya waTanganyika, tunajinyima hivyo hivyo ili kuwasaidia na nyie kupe wetu msioweza kujizalishia umeme wenu wenyewe na bado hauna soni unakuja kutukejeli mitandaoni? Kweli fadhila mfadhili mbuzi maana binadamu wana maudhi na shukurani ya punda siku zote ni mateke ila kwakua kwenye hii scenario nyie ndo punda, basi endeleeni kutupiga mateke huku mkijua dawa yenu inachemka na mtapewa sooner or later.

Mnao ma rais watatu, mna wizara zenu na wabunge wenu, hawa wote kwanini wameshindwa kuwasaidia kuvuna huo umeme wa jua, upepo, geothermal na hydrogen? Kwanini bado mnaendelea kuwa kupe msio na shukurani kwa tunaowasaidia?

Kudhihirisha utegemezi wenu, hata wewe mwishoni kwenye aya uliyoipa namba 3, umesema "na hata Kenya"😂, yaani kumaanisha kwamba tukiwanyima sisi msaada wa umeme mtaenda kuomba msaada kwa waKenya. Dependency, dependency, dependency. Zanzibar bila msaada wa foreigners, mtaishia kuwa wavuvi kwenye ngarawa na uchumi wenu utazidi kuwa duni. Kwanza mna sifa jumuishi ya kutukuwa watu wenye kupenda kazi. Wimbi la vijana wenu wanashinda Forodhani kujitupa kwenye maji huku wakiomba chelechele kwa wazungu, wengine wanafuga rasta na kujiita beach boys huku wakitumainia kupata udhamini wa wazungu ili wakimbie umasikini wa kutupwa wa nchi yao waende kutumikishwa mbele kwa mbele.

Kuhusu hili suala la kusema Zanzibar ilikua nchi ya tatu kutumia umeme duniani, naomba niseme kwa heshima kabisa kwamba HAUNA AKILI NDUGU YANGU.
 
3. Mkuu sidhani kama tafsiri ya neno faida ni jambo ambalo linahitaji mjadala ila naomba kuuliza kwako wewe, faida unaitafsiri kwa namna gani? Faida ya muda mrefu na faida ya muda mfupi zote kwa ujumla wake ni aina za faida.

Umesema pia kwamba sisi Tanganyika ni hohehahe (japo umeandika "muko hahe hoe"😂nimetumia jitihada za ziada kuelewa ulicho maanisha ndugu mjuzi wa mambo), lakini nimetoka juzi juzi Zanzibar umeme unakatika mpaka masaa 8 nchi ya tatu kutumia umeme duniani, naomba niseme kwa heshima kabisa kwamba HAUNA AKILI NDUGU YANGU.

AY 5225

Kwanza ahsante san akwa majibu yako, weye inaonekana tunaweza kuzungumza kiutuuzima. Let me keep thigs coear for you.

Nianze ne neno "FAIDA"

Katika level ya kinchi faida ni kupatika manufaa katika vitengo mbali mbali, ikiwemo elimu bora, matibabu bora, uchumi bora ikewemo control ya pesa, uatwala wa mipaka na mahusiano ya nchi za nje. kupatika kwa uzalishaji wa kila aina, viwanda, food security kama vile uvuvi, kilimo bora ardhini na baharini, mawasiliano bora na ya uhakika N.K, heshma ya uraia kwa wananchi, freedom katika personal economy, freedom of travelling. kwa mtazamo wangu ninapozungumzia faida huwa nazungmzia mambo kama hayo. Mambo yote hayo hayapatikani kwasababu tanganyika ndio yenye benki kuu, mahusiano ya nje, na control ya sarafu.

Nasema tanganyika hahe hohe kwasababu utajiri asilia mulonao na ikawa bado ni mafukara, hamuna wa kumlaumu, wala musimlaumu Mungu, maana amekupeni kila kitu. Ikiwa munaweza kuilima ardhi yenu basi mutaweza kuilisha afrika na ulaya yote, nyie bado leo hii mwafa na njaa. Kuhusu zanzibar, sis hatuna uchumi kabisa, tunalijuwa hilo nje na ndani. sababu kubwa ni kwamba nyie watanganyika mumeweka mikono yenu michafu. na nyie kila muwekapo mkono panageuka matope. Kila tukitaka kufanya kitu anatoka mtanganyika mmoja naweka mguu, tukitaka kuomba misaada nje lazima tupitie foreign affairs ya tanganyika na pesa ziingie katik abenk kuu ya tanganyika, mara nyingi pesa zinaishia katika madaa ya ulevi tu huko huko. Tukitaka kukopa pesa lazima pesa zipite benki kuu ya tanganyika, na vikwazo hivi ni kama makaburu walokuwa wakiwafanyia waafrika kule south afrika. Ndio maana tukawa hatuna umeme.

Kweli tuna maraisi watutu na wizara zetu, lakini hatuna pesa kwasababu tunatumi apesa za tangayika, benki kuu ya tanganyika, tukiwa na safaru yetu na benki kuu yetu, nyie mutaona uwezo wetu. kweli mkuu shida sana kulazimisha kuungana na watu wenye akili za kifukara, watanganyika

kuhusu utegemezi wetu, mkuu sijui kama umesoma uchumi, au utataka kutajie nchi zinazonunuwa ueme hapa hapa afrika mashariki? umeme sio kipimo. nyie hapo tangayika munanunwa samaki kutoka uchina, huamini nenda sokoni pale kivukoni, hiyo ndio aibu mkuu. bahari yote hiyo hamuwezi hata kuvua.

Unasema wazanzibari wavivu, hakuna kazi tu, sababu kubwa ni control ya pesa. siku tukiwa na sarafu yetu, nakugerentii, utaona, kwanza tutafunguwa offshore banking system, ajira zitakuwepo, ingawaje kwanza ni lazima tuvunje elimu ya kitanganyika, lakini in the long run, offshore factories and industries, re-export economic zones, sasahivi kufanya haya kuna uchawi mwingi kutoka muungano.

Kuhusu suala la umeme, mkuu, labda weye hukusomeshwa historia ya ukweli, sio umeme tu, katika beit el jaibu, lift iliyokuwepo ni katika lift za mwanzo duniani 1880s, lfit za otis. mie sikumoja nilikuwa katika moja ya nchi za falme za kiarabu kwa kazi, tutakawa tunazunumza njiani, akaja mzee wa kiarbu mwenyeji wa nchi hiyo, akasema na sie kwa kiswahili na kutuuliza tunatoka wapi. Tukamwabia sie ni wazanzibari (tukiwa nje sie hatujihisi wala hatujitaji kama ni wa tanzania). tukamuuliza kajuwa vipi kiswahili, akasema alikuwa baharia wakija siku hizo zanzibar kuchukuwa vyakula na kupeleka uarabuni. si siku za nyuma sana no katika 1950s tu. Sasa tatizo la zanzibar narejea tena ni kuwepo mkono wa watanganyika mkono mchafu, unapokuwa panahribika. Ukifika zanzibar lazima ufike telephone house, utakuwa record ya 1886, embassy of America 1832, Richard waters kutoka salem massachusetts alikuwa balozi wa kwanza. siku hizo nyie huko bado munavaa makaniki mkuu.
 
AY 5225

Tulia nikujibu, tatizo sijui ukubwa wa ufahamu wako wa mambo ya dunia. Lakini hatahivyo nitakujibu upate kucheka. Nitakwenda deep kidogo, ikiwa ni above your capacity utaniwiya radhi kwa hilo.

Nimesema sitochoka, NITAKUELEWESHA NA UTAELEWA WALA USIWE NA WASIWASI NDUGU YANGU.

4. Naomba nikuelimishe kidogo kuhusu neno EMPIRE. At its most basic sense, an empire is a complex political organization where a dominant central state controls weaker peripheral states. Zingatia hapo kwenye "CONTROLS WEAKER PERIPHERAL STATES". Hata hivyo, hakuna sifa ya moja kwa moja ya kuifanya state kuwa empire, lakini the main ingredient is always control. Sasa hiyo point yako ya kwamba empire zote ulizoziainisha hapo juu zimebanwa na global political dominance ya watu weupe haileti maana kabisa. Utaiitaje empire wakati haiko self-autonomous? Utaiitaje empire nawakati ina mianya ya kuingiliwa na kupangiwa na foreign states?

Hivyo vikwazo vinavyowekwa juu ya nchi ulizozitaja (Iran, China, Japan, Turkey na Zanzibar), si hata Russia imewekewa na inaendelea kuwekewa? Ila bado ina prevail na ina prosper regardless. That's the true definition of a firm empire. North Korea is still defying the rules and so it might also amount to a true empire in the near future. Ukishaona unapangiwa what to do, when to do it and how to do it, you sure as hell not an empire.

ZANZIBAR HAIJAWAHI KUWA SELF-AUTONOMOUS KAMWE. YOU GUYS HAVE ALWAYS BEEN UNDER SOME STATE'S CONTROL AND YOU WILL FOREVER BE SUBJECTS KWAKUA HAMJITOSHELEZI KWA RASILIMALI WALA TECHNOLOGY.
 
AY 5225

Kwanza ahsante san akwa majibu yako, weye inaonekana tunaweza kuzungumza kiutuuzima. Let me keep thigs coear for you.

Nianze ne neno "FAIDA"

Katika level ya kinchi faida ni kupatika manufaa katika vitengo mbali mbali, ikiwemo elimu bora, matibabu bora, uchumi

Tafsiri yako ya neno faida ni batili, ifanyie marekebisho. Hivi nikiwa nafanya kazi ya kulipwa mwisho wa mwezi na siku za katikati nikawa napokea per diem, haya maokoto ya siku za katikati haya'amount kuitwa faida? Jibu utakalopata ndo ujue ulipoteleza kwenye kutafsiri neno faida.

Naomba usininukuu vibaya, mimi sina chuki na Zanzibar hata kidogo. As a matter of fact, Zanzibar is a very beautiful archipelago. Pia napenda kutanabaisha kwamba sina phobia na waZanzibari waopambania maslahi mapana ya nchi yao kwakua it's the purest thing one can do for one's nation. Sisi pia waTanganyika tunafanya the very same thing.

Shida yangu ipo kwenye kejeli, dharau na matusi mnayoturushia sisi waTanganyika wakati sisi tunajaribu kuweka wazi kero zetu za huu muungano ambao ni ukweli usiopingika kwamba hauridhiwi na pande zote mbili ila wala hauhitaji kuwa na Phd ili ujue kwamba tunaoumia zaidi ni upande wetu waTanganyika.

Uwepo wa rasilimali nyingi na bado nchi kuwa masikini sio tatizo la Tanganyika tu. Hili tatizo ni la bara lote la Africa isipokuwa kwa baadhi ya nchi ambazo hazifiki hata mbili, maana ukiniambia nitaje nitaitaja Egypt pekee ndio imesalimika na kitanzi hiki.

Hivi kweli unahitaji mwalimu kutoka Uingereza aje akueleweshe kwamba rasilimali bila technology ya kuzi'match haziwezi kuleta matokeo yenye tija? Unahitaji ashuke mtume mwingine aje kwa lengo la kukufahamisha kwamba ukosefu wa mtaji, sera mbovu, rushwa, elimu duni, health insecurity na population structure yenye watoto wengi kuliko watu wazima ni adui wa maendeleo?

Ni takribani miaka 24 toka nimekuja duniani, SIJAWAHI KUSIKIA MTANGANYIKA AMEFARIKI KISA AMEKOSA CHAKULA. Kufa kisa umekosa chakula kwa nchi yangu labda usiwe na akili timamu. Ninachokiongea nimeki'experience first hand na wala siropoki. Nimekuwa homeless kwa miezi miwili, nimelala chini ya miti na misikitini, nina record ya kukaa masaa 53 bila mlo wowote ila nadiriki kusema kwamba "UKIFA NJAA TANGANYIKA WEWE NI MWEHU". Sisi ni wakarimu sana, hatuna ubaguzi wa kijinga na watu wema wanaoweza kukusaidia unconditionally wapo wengi sana.

Sasa kama chanzo cha nyie kukosa maendeleo ni kwakua mna diplomatic limitations, hao ma rais wote watatu wanafanya kazi gani? Bunge lenu limeundwa ili wavuvi wakutane kupiga soga?

Unasema Zanzibar haina uchumi wake, hiyo wizara inafanya kazi gani? Mna mamlaka yenu ya kodi ambazo zote mnakusanya na zinabakia kwenu na bado mnachukua fungu kutoka JMT ila hata kujigharamia umeme hamuwezi na nchi yenu haiendelei kwa chochote halafu mnakuja kutulaumu sisi tunaosamehe madeni na kuwapa fursa za ajira, mikopo ya elimu na kumiliki ardhi ambavyo vyote hata sisi wenyewe waTanganyika havitutoshelezi. Hela zenu mnapeleka wapi? Mmetengeneza ka bureaucratic structure ka ki'mwinyi ili mpate mwanya wa kuchukua hela zetu na kuchezea za kwenu mnazokusanya. Mnatutaka nini lakini? Tuwape nini nyie watu?

Hebu nieleze sababu za kuwa na ma rais watatu na bunge kama hata kujiwekea umeme toka miaka ya early 60's mmeshindwa?

MOJA YA SIFA COMMON MIONGONI MWETU MASIKINI WOTE DUNIANI NI KUTAFUTA MTU WA KUMLAUMU KWA MATATIZO YETU SISI WENYEWE.

Mimi hapa nilipo yakaribia mwaka toka nihitimu chuo na ka degree kangu, sina kazi yoyote na umasikini umenijaa ila yote kwa yote kwa hali niliyoshuhudia kwa macho yangu huko kisiwani kwenu, SITOKUBALI MZANZIBARI YOYOTE ANIITE MIMI FUKARA KWAKUA NYIE NDIYO MAFUKARA TO THE HIGHEST CALIBRE.

Nimesoma MNMA na kwa miaka yote mitatu nimeishi Kigamboni na bado ninaishi Kigamboni ila Ferry fish market sijawahi kujua kwamba kuna samaki wanatoka China😂. Hivi unaongea nini wewe lakini?
 
AY 5225

Kwanza ahsante san akwa majibu yako, weye inaonekana tunaweza kuzungumza kiutuuzima. Let me keep thigs coear for you.

Nianze ne neno "FAIDA"

Katika level ya kinchi faida ni kupatika manufaa katika vitengo mbali mbali, ikiwemo elimu bora, matibabu bora, uchumi

Let me finish what I started kabla sijalala maana sisi waTanganyika hatuna kawaida ya uvivu kama nyie ndugu zetu😂.

Naomba kuuliza, hivi Zanzibar hakuna wizara ya elimu? Kama wanajua kazi yao wameshindwa nini kubadilisha structure ya elimu? Mmeshindwa nini kujenga vyuo na mashule yenye kutoa aina ya elimu itakayowasaidia na wakati mnakusanya kodi? Yaani hamna vyuo wala shule nzuri kwenu, tunawa'host huku kwetu na kuwapa mikopo ila bado wakosa shukurani kama wewe mnajificha nyuma ya keyboards na kutudhihaki, seriously? Dah! dunia hii ina watu na viatu kwakweli. And just for the record, elimu sio sifa ya waZanzibari. Matokeo yenu kwenye Necta ni YANACHEKESHA TO SAY THE LEAST.

Turudi kwenye suala la umeme. Beit al-Ajaib ilijengwa mwaka 1883 kwa amri ya Sultan na wakati Michael Faraday ali'invent electric motor ya kwanza mwaka 1821, you seriously out here saying Zanzibar ni nchi ya tatu kutumia umeme duniani? So for the entire 62 years, only two other countries apart from your kaZanzibar had been using electricity! Wisen up.

Nafurahi kusikia kwamba waZanzibar mkiwa ughaibuni hamjitambulishi kama ni waTanzania. Angalau mnatupunguzia fedheha za kuonekana kwamba Tanzania ina watu wa aina yenu msiopenda kujishughulisha mkisubiria misaada.

Huyo baharia kama kweli ndivyo alivyowaambia kwamba walikua wakitoka uArabuni kuja Zanzibar kufuata vyakula na sio spices, yeye na wewe hamtofautiani upeo. Utafuataje chakula kwenye sehemu ambayo haina chakula inategemea iletewe? Unless otherwise kulikua na soko la kimataifa huko, kitu ambacho sio kweli kwa miaka uliyoitaja (1950's). Enzi za utawala wa waIngereza huku Tanganyika wala hawakuwa na sera ya kuuza vyakula vitokavyo mainland kwa waArab.

CHECK YOUR SOURCES AND GET WELL-INFORMED TO AVOID BRINGING SUCH KIND OF NONSENSE TO THE WEB.
 
Nimesema sitochoka, NITAKUELEWESHA NA UTAELEWA WALA USIWE NA WASIWASI NDUGU YANGU.

4. Naomba nikuelimishe kidogo kuhusu neno EMPIRE. At its most basic sense, an empire is a complex political organization where a dominant central state controls weaker peripheral states. Zingatia hapo kwenye "CONTROLS WEAKER PERIPHERAL
Unajichosha vip kubishana na mpumbavu aliyekalili ujinga na kujazwa mindset za mwarabu?

Ubaya uko hapa
Watu wa Zanzibar ni matokeo ya vizazi vya waTanganyika waliochukuliwa Utumwani huku Wanakokuita Tanganyika na baadae wako huko Zanzibar leo hii na wamezaana na hao waliowatumikisha babu zao(waarabu).

Hiki kizazi chotara na baadhi ya mablack pure wameshaharibiwa akili na kuidharau asili yao badala yake wanajiona nao ni sehemu ya uarabu jambo ambalo si kweli.

Waarabu walioikalia Zanzibar walipaswa kufunguliwa mashitaka ya biashara haramu na kudaiwa fidia ndefu kwa ufedhuri walioutenda kwa waTanganyika.

Ni ngumu kumuaminisha Mtanzania/mzanzibar asili yake akaiubali , ni ngumu sana hawa jamaa wameshaharibiwa akili haswa suala la DINI, hawa jamaa wanawaona waarabu kama miungu wao yaan wanawatukuza na kuwathamini kulko hata kumthamini mTanganyika ambaye ndie ndugu.

KWA BAHATI MBAYA/NZURI huu muungano hauna faida kwa Tanganyika lakin kwa namna nyingine kuna faida kuu , ambayo ndiyo ilimfanya Nyerere akubali kuingia mkataba wa kusaini makubaliano ya muungano, kibaya zaid na Wazungu waliomkabidhi nyerere Hii nchi walishaubariki huu muungano hivyo HAUTOKUJA KUVUNJWA KAMWE, maana Mzungu wa UK hawezi kubali Koloni lake liingiliwe na mwarabu, ujuwe kwamba siku Zanzibar itakapojitenga hata wale mahayawani, majambazi na Vizazi vya wakolon wa uarabuni waliotawala zanzibar watarudi upya, najua wapo na ndio hawa wanaochochea , hili jambo la kuvunjwa muungano kwa maslahi yao kupitia vibaraka wao ambao ni hao Mashekhe washenzi waliokosa Uzalendo na kukubali kuuza utu wao kwa mwarabu.

Jiulize kwanini hata hao wazanzibar wanapopata nafasi za juu ktk uongoz Tanzania hawavunji muungano? Jibu ni kuwa huo mkataba uliowekwa una nguvu ambayo hakuna pimbi wa kuishinda, nguvu hiyo ilishabarikiwa na watawala wa Dunia kipindi cha muungano, pia Kama kiongozi suala la usalama ni muhimu zaidi kuliko kujali tamaa na kuwafuraisha wachache, ni mjinga tu atakayeruhusu mipaka yake ikaliwe na maadui, kwa akili ya kawaida tu eti zanzibar ijitenge na kujivisha yale masheria ya kipuuzi wanayoyatamani kutoka kwa mabwana zao unadhani Tanganyika itakuwa salama? Jinsi waarabu wasivyo na akili unadhani tutakuwa salama?

Kuvunjwa muungano hiyo haitowai kutokea sahauni kabisa, Zanzibar itaendelea kuwa Chini ya muungano na kamwe haitojitenga.

NA HUU NDIO UKWELI MCHUNGU AMBAO HAUTOAMBIWA NA MWANASIASA WALA KUAMBIWA NA YEYOTE MAANA UNAFICHWA ILI KUWATIA MOYO...Idumu milele Tanzania
 
Unajichosha vip kubishana na mpumbavu aliyekalili ujinga na kujazwa mindset za mwarabu?

Ubaya uko hapa
Watu wa Zanzibar ni matokeo ya vizazi vya waTanganyika waliochukuliwa Utumwani huku Wanakokuita Tanganyika na baadae wako huko Zanzibar leo hii na wamezaana na hao waliowatumikisha babu zao(waarabu).

Ameshaelewa mkuu ndo maana unaona yupo kimya. Ila daah! huu ni ukweli mchungu wa kwamba muungano utaendelea kudumu hata kama hatuutaki. Hakuna namna ngoja tuendelee kuvumilia matusi, dharau na majigambo ya ndugu zetu waArabu wa Pemba😂.
 
Yep lakini sasa mwasubiri nini kujitoa wakati mna njia nyepesi???

Sina hakika kama mwalazimishwa au mnashindwa kwa sababu mna maslahi ambayo huwa mnajifanya hamuyaoni.

Samia Mzenji, Mwinyi Mzenji si ndiyo ilikuwa so simple tena na zile nyimbo zenu za tunataka Nchi yetu zingeshamiri uzuri

Wazenji MNA kaunafiki Fulani Fulani hivi.[emoji23][emoji23]

Kama vile hao Samia na Mwinyi waliwekwa na wananchi kwa kura huru , wakati mwengine uwe unatumia akili ya kichwani kufikiri
 
Huu ni Upuuzi kama upuuzi mwingine wowote; kuongezeana gharama zisizo na Tija; ebu ongeeni ni wahusika hili jambo lifutwe kwa haraka sana..., Kuna vitu vingine wala havina manufaa kwa mtu yoyote...

Kwahio International Passport nayo vipi ?!!! Au watalii wanaotoka huko pande za mbali nao wanapata hizi Kero ? Kweli Akufukuzae hakwambii toka...
 
Kama hao Samia na Mwinyi waliwekwa na wananchi kwa kura huru , wakati mwengine uwe unatumia akili ya kichwani kufikiri
Umejuaje kama nimetumia akili za kichwani kufikiri na siyo akili ya magotini [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]wake up from your box bros, don't come here and spit these nonsense instead
 
Unajichosha vip kubishana na mpumbavu aliyekalili ujinga na kujazwa mindset za mwarabu?

Ubaya uko hapa
Watu wa Zanzibar ni matokeo ya vizazi vya waTanganyika waliochukuliwa Utumwani huku Wanakokuita Tanganyika na baadae wako huko Zanzibar leo hii na wamezaana na hao waliowatumikisha babu zao(waarabu).

Hiki kizazi chotara na baadhi ya mablack pure wameshaharibiwa akili na kuidharau asili yao badala yake wanajiona nao ni sehemu ya uarabu jambo ambalo si kweli.

Waarabu walioikalia Zanzibar walipaswa kufunguliwa mashitaka ya biashara haramu na kudaiwa fidia ndefu kwa ufedhuri walioutenda kwa waTanganyika.

Ni ngumu kumuaminisha Mtanzania/mzanzibar asili yake akaiubali , ni ngumu sana hawa jamaa wameshaharibiwa akili haswa suala la DINI, hawa jamaa wanawaona waarabu kama miungu wao yaan wanawatukuza na kuwathamini kulko hata kumthamini mTanganyika ambaye ndie ndugu.

KWA BAHATI MBAYA/NZURI huu muungano hauna faida kwa Tanganyika lakin kwa namna nyingine kuna faida kuu , ambayo ndiyo ilimfanya Nyerere akubali kuingia mkataba wa kusaini makubaliano ya muungano, kibaya zaid na Wazungu waliomkabidhi nyerere Hii nchi walishaubariki huu muungano hivyo HAUTOKUJA KUVUNJWA KAMWE, maana Mzungu wa UK hawezi kubali Koloni lake liingiliwe na mwarabu, ujuwe kwamba siku Zanzibar itakapojitenga hata wale mahayawani, majambazi na Vizazi vya wakolon wa uarabuni waliotawala zanzibar watarudi upya, najua wapo na ndio hawa wanaochochea , hili jambo la kuvunjwa muungano kwa maslahi yao kupitia vibaraka wao ambao ni hao Mashekhe washenzi waliokosa Uzalendo na kukubali kuuza utu wao kwa mwarabu.

Jiulize kwanini hata hao wazanzibar wanapopata nafasi za juu ktk uongoz Tanzania hawavunji muungano? Jibu ni kuwa huo mkataba uliowekwa una nguvu ambayo hakuna pimbi wa kuishinda, nguvu hiyo ilishabarikiwa na watawala wa Dunia kipindi cha muungano, pia Kama kiongozi suala la usalama ni muhimu zaidi kuliko kujali tamaa na kuwafuraisha wachache, ni mjinga tu atakayeruhusu mipaka yake ikaliwe na maadui, kwa akili ya kawaida tu eti zanzibar ijitenge na kujivisha yale masheria ya kipuuzi wanayoyatamani kutoka kwa mabwana zao unadhani Tanganyika itakuwa salama? Jinsi waarabu wasivyo na akili unadhani tutakuwa salama?

Kuvunjwa muungano hiyo haitowai kutokea sahauni kabisa, Zanzibar itaendelea kuwa Chini ya muungano na kamwe haitojitenga.

NA HUU NDIO UKWELI MCHUNGU AMBAO HAUTOAMBIWA NA MWANASIASA WALA KUAMBIWA NA YEYOTE MAANA UNAFICHWA ILI KUWATIA MOYO...Idumu milele Tanzania


Hiyo ndiyo propaganda ya kanisa na CCM yake, hivi kuna lugha ya kabila yoyote huko bara inayoongea kimakunduchi , kitumbatu , kikojani , nk ??

ujinga ulikuwepo wa viongozi wasioangalia future ya nchi yao na vizazi vya baadaye kama Nyerere.

Yaani alihiari kuivamia Zanzibar na kuuwa maelfu ya raia wasio hatia eti kulinda nchi yake Tanganyika na vita vya kikabila na udini badala ya kujikita kuyaunganisha makabila kuendeleza uchumi na kuweka utawala wa kidemokrasia na sheria.

Matokeo yake kaipeleka arijojo Tanganyika na Zanzibari yake pia.
Laana imshukie Nyerere
 
Umejuaje kama nimetumia akili za kichwani kufikiri na siyo akili ya magotini [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]wake up from your box bros, don't come here and spit these nonsense instead

Nimejua kwa namna ulivyoandika kuwa hujatumia akili hata ya uzito wa mdudu chungu
 
Ameshaelewa mkuu ndo maana unaona yupo kimya. Ila daah! huu ni ukweli mchungu wa kwamba muungano utaendelea kudumu hata kama hatuutaki. Hakuna namna ngoja tuendelee kuvumilia matusi, dharau na majigambo ya ndugu zetu waArabu wa Pemba😂.
Wacha tutauza mpaka makalio yenu 😛😛😛
 
wenye shida zaidi ni nyinyi mnaopiga kelele kajibandari kenu kameuzwa na Wazanzibari
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]lakini kama hatujakualika na shida zetu hazikuumizi wewe umeingilia wapi na kuanza kuumia sasa. I think you should not allow your rotten mouth to speak bro umesema sina akili asa kama unazo Una maintain vipi kujibizana nami
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]lakini kama hatujakualika na shida zetu hazikuumizi wewe umeingilia wapi na kuanza kuumia sasa. I think you should not allow your rotten mouth to speak bro umesema sina akili asa kama unazo Una maintain vipi kujibizana nami

Mimi sikulaumu kwani huyo baba yenu Nyerere alikuwa hana akili , yaani Jinchi lote Tanganyika kuja kujiunga na kanchi ambacho huko Tanganyika kinaingia zaidi ya mara 10 000 yaani uuwe maelfu ya watu kwa kuunganisha nchi hii Zanzibar na Tanganyika ?? Hivi hiyo ni akili ??
 
Wacha tutauza mpaka makalio yenu 😛😛😛

Ohooo!😂 kashakuja zezeta mwingine. At least alietoka alikua sio roporopo kama wewe. Lakini usiwe na wasiwasi mkuu kwakua muda ninao hivyo nitakuelewesha na utaelewa.

Haya afande Rama, tueleze unachotaka kujua tukujuze.
 
Back
Top Bottom