KWELI Mtanzania Bara huruhusiwi kuendesha gari Zanzibar bila kuwa na kibali maalum

KWELI Mtanzania Bara huruhusiwi kuendesha gari Zanzibar bila kuwa na kibali maalum

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.

Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.

Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.

Huu Muungano ni wa kishenzi sana.

Bilikundi.jpg

 
Tunachokijua
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa Aprili 26, 1964 ikiwa ni Muungano wa Mataifa mawili huru ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo yaliingia mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964 huko Zanzibar.

images

Picha: Mwalimu Julius Nyerere (kushoto) na Sheikh Abeid Amani Karume (kulia) wakibadilishana Hati za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili, 1964.
Sababu ya Muungano
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwepo kutokana na sababu mbalimbali kama vile kuwepo kwa mahusiano ya karibu na ya kihistoria baina ya Tanganyika na Zanzibar katika nyanja mbalimbali kama vile undugu wa damu, biashara, utamaduni, lugha na mahusiano ya karibu kisiasa hususan baina ya vyama vya TANU na ASP.

Pamoja na kuwepo muungano lakini Tanganyika na Zanzibar hazikuungana kwenye kila jambo bali kwa baadhi ya mambo tu, hivyo kuwepo kwa mambo yahusuyo Muungano na ambayo hayahusu Muungano hivyo kila upande huyashughulikia bila kuhusisha Muungano.

Je, Mtu wa Tanzania bara anaruhusiwa kuendesha gari Zanzibar kwa kutumia leseni yake aliyopewa na TRA?

JamiiForums Imezungumza na Kamanda wa Polisi Ramadhani Ng'azi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, ambaye amekiri kuwa:

"Ni kweli mtu hawezi kutumia leseni yake aliyopewa na mamlaka ya Mapato Tanzania( TRA) kwasababu Mamlaka ya utoaji wa leseni sio jambo la kimuungano hivyo Mamlaka za utoaji wa Leseni kati ya Tanzania bara na Zanzibar zipo tofauti.

Tanzania bara Mamlaka inayotoa leseni ni TRA, baada ya kupata uthibitisho kutoka jeshi la Polisi kuwa mtu huyo amesomea udereva na amepitia mitihani ya polisi au utahini wa polisi na kupewa hati maalum ya kufaulu na kwamba mtu huyo anatakiwa kupatiwa daraja fulani la leseni.

Baada ya TRA kupokea taarifa ya uthibitisho kutoka Polisi hutoa leseni kulingana na maelekezo ya jeshi la polisi kikosi cha usalama Barabarani.

Lakini Zanzibar wao wana mamlaka yao ya utoaji leseni ambayo ni tofauti na huku Bara na ndio maana wameweka utaratibu mtu akitoka huku kwenda kule ataomba kibali maalum kwa kuwa mamlaka ya utoaji leseni siyo jambo la kimuungano.

Hivyo
mtu akienda Zanzibar ataomba kibali maalum na vivyo ivyo mtu akitoka Zanzibar kuja bara ataomba kibali maalum ili aweze kuendesha gari".


Pia, JamiiForums imezungumza na Abubakar Nassor Ali Mkuu wa Divisheni ya Upasishaji Madereva, Mamlaka ya usafiri na usalama barabarani Zanzibar, ambaye amesema kuwa:

"Kimsingi tunapozungumzia suala la usafirishaji, Tanzania tuna sheria 2 tofauti, zikiwa na lengo moja la udhibiti wa usalama barabarani. Huko bara mna sheria ile namba 30, ya mwaka 1973 (Road Traffic Act) lakini Zanzibar tuna sheria namba 7 ya mwaka 2003 kwa ivyo ni sheria 2 tofauti ila lengo ni moja la shughuli za usafirishaji.Na hii kutokana na jambo hili kutokuwa la kimuunano.

Kwa maana Zanzibar tuna sheria yetu, sheria hiyo ndio inashughulika na mambo mbalimbali ya leseni, na inamtaka dereva yeyote awe na leseni.

Sheria yetu inatuambia mtu yoyote ambaye atatoka nje ya nchi, inamtaka mwenye leseni ya udereva mbali na ile iliyotolewa na Msimamizi Mkuu wa usafiri barabarani( Mkurugenzi wa mamlaka na usalama Barabarani) kwenda kufanya jaribio au kuangalia afya au kufanya mtihani ili kupima uwezo wake wa uendeshaji chombo cha moto akiwa ndani ya nchi.

Kwa maana hiyo mtu yoyote ambaye atakuwa na leseni ya nje ya nchi( nje ya nchi hapa ni pamoja na Tanzania bara)
anatakiwa kukata permit, kwa hiyo kwetu mtu yoyote ambaye atakuwa anatokea bara maana yake anatokea nje ya nchi, na anatakiwa kukata Permit (kibali maalum) ambapo kwa sasa gharama yake ni 15,000 ambayo hudumu kwa miezi 3.

Na kwa yule ambaye atakuwa anataka kuendelea kukaa Zanzibar kwa muda mrefu zaidi au kuweka makazi ya kudumu basi ana uwezo wa kubadilisha leseni yake, yaani atakata leseni ya huku Zanzibar,( hatubatilishi leseni ila atabaki nayo ya bara na atapewa nyingine ya huku baada ya kufuata taratibu za kuchukua leseni huku)

Mtu atakayekiuka sheria hii na kuendesha bila leseni atakuwa ametenda kosa, Kosa la mtu kuendesha bila leseni hapa ni kwa wageni wote ( nchi nyingine pamoja na wa bara) adhabu yake ni faini ya dola zisizopungua 50 ambapo kwa sasa ni sawa 116,500".


bilikundi-jpg.2703699
JamiiForums baada ya kusoma mambo yahusuyo muungano na kujiridhisha kuwa suala la usafirshaji si la kimuungano na kuzungumza na mamlaka za usafirishaji pande zote 2 za muungano ambao wamekiri mtu anayetoka upande 1 kwenda mwingine anatakiwa kukata kibali maalum ivyo imejiridhisha kuwa ni kweli Mtu wa Tanzania bara haruhusiwi kuendesha gari Zanzibar mpaka akate kibali maalum(permit)
Mimi sikulaumu kwani huyo baba yenu Nyerere alikuwa hana akili , yaani Jinchi lote Tanganyika kuja kujiunga na kanchi ambacho huko Tanganyika kinaingia zaidi ya mara 10 000 yaani uuwe maelfu ya watu kwa kuunganisha nchi hii Zanzibar na Tanganyika ?? Hivi hiyo ni akili ??
Poa ndiyo shida ya Watoto wa kikeni huwa mnasumbua Sana dada walituletea shida kwa kuzaa na wageni
 
Ohooo!😂 kashakuja zezeta mwingine. At least alietoka alikua sio roporopo kama wewe. Lakini usiwe na wasiwasi mkuu kwakua muda ninao hivyo nitakuelewesha na utaelewa.

Haya afande Rama, tueleze unachotaka kujua tukujuze.
Mambo yenyewe mumekuwa wafuasi wa kanisa la Nabii Tito, ni kuwapiga bei tu
 
Mambo yenyewe mumekuwa wafuasi wa kanisa la Nabii Tito, ni kuwapiga bei tu

Hata haueleweki unaongea nini. Kichwa kisicho na akili ni mzigo kwa shingo. HAUNA AKILI NDUGU YANGU.
 
Review ifanyike

Hakuna review ni huu uvamizi uitwao muungano uishe , kila nchi iende kivyake tuwe na uhusiano mwema tu , muungano ni kudanganyana kwani Wazanzibari kamwe hawawezi kusahau nndugu na wazee wao waliouliwa na uvamizi wa Nyerere na kuchukuliwa nchi yao.

Tutakaa hivyo hivyo pamoja lakini moyoni kila mtu yuko kivyake , UNAFIKI MTUPU
 
Unapaswa ujibu kwanza swali ndipo unauliza swali lako jipya.

Kistaarabu ngoja nikujibu swali lako.

Leseni ya Zanzibar haiwezi kuruhusiwa bara sababu bara sio Zanzibar.

Naomba na wewe unijibu swali langu

Swali langu kwani Zanzibar sio sehemu mojawapo ya Tanzania ?

Naomba kumsaidia kujibu swali lako.
Zanzibar ni sehemu ya Tanzania kwa baadhi ya mambo, lakini si sehemu ya Tanzania kwa baadhi ya mambo likiwemo hili la usafirishaji.
Kwenye hili Zanzibar inabaki kua Zanzibar.
 
Muungano wa kipumbavu sana huu.Ndo maaana hata Bandari wanauza kwa sababu wanajua hawana faida nazo
 
Huu muungano hata Mangungo angeukataa sijui Nyerere kwa nini aliwadekeza sana hawa wazanzibar
Alafu walivyouwa wanjanja wa Zanzibar. Serikali yao imesha sign mikataba na ushirikiano wenye sekta za madini za bara. Yaani wameshawahi kujiingiza kwenye keki hata kama muungano ukivunjika. Nomaa sanaa.! Sijui watanganyika na sisi tumeenda zanzibar ku sign kitu gani in return.
Tumelala sanaa wa bara..!
 
Usiamini sana haya Mambo ya mtandaoni, mi nimefanya kazi sana, zenj, ofc zetu zipo pale michenzani mall, nimezunguka zenj, vijijini(wanaita shamba), uroa, pongwe,nimeendesha, gari sana, na kila nikisimamishwa, naonyesha leseni yangu ya bara,tunaishia kupeana asalaaam ALEIKUM, nasepa,sikuwahi kuoana hiyo shida, kuna mwenzangu shughuri zake zote anafsnyia zenj, ameoa kule, amejenga, na kampuni yake ya ukandarasi, inapewa tender sana, ni mkristo, lakini kwenye cycle za, waislamwanamkubali sana,
Tatizo wa bongo wengi, hupenda kuleta swaga za bara, zenj, wa zenj hawapendi kupelekwa pelekwa,
Wao saa 11 wamefunga maduka! Ijumaa, wakitoka kazini,hakuna kupika, ni kwenda kula biriani cafe.
Gari nimekodisha kwa kuacha kadi au passport tu,
Nimesafirisha majenereta ya thamani kubwa kwa kumpa mtu tu bila maandishi, na mzigo unafika vzr,
Tuache hizi chuki zinazopigiwa kelele na wanasiasa, wananchi wa kawaida wa zenj, na bara tunashirikiana sana,
 
Usiamini sana haya Mambo ya mtandaoni, mi nimefanya kazi sana, zenj, ofc zetu zipo pale michenzani mall, nimezunguka zenj, vijijini(wanaita shamba), uroa, pongwe,nimeendesha, gari sana, na kila nikisimamishwa, naonyesha leseni yangu ya bara,tunaishia kupeana asalaaam ALEIKUM, nasepa,sikuwahi kuoana hiyo shida, kuna mwenzangu shughuri zake zote anafsnyia zenj, ameoa kule, amejenga, na kampuni yake ya ukandarasi, inapewa tender sana, ni mkristo, lakini kwenye cycle za, waislamwanamkubali sana,
Tatizo wa bongo wengi, hupenda kuleta swaga za bara, zenj, wa zenj hawapendi kupelekwa pelekwa,
Wao saa 11 wamefunga maduka! Ijumaa, wakitoka kazini,hakuna kupika, ni kwenda kula biriani cafe.
Gari nimekodisha kwa kuacha kadi au passport tu,
Nimesafirisha majenereta ya thamani kubwa kwa kumpa mtu tu bila maandishi, na mzigo unafika vzr,
Tuache hizi chuki zinazopigiwa kelele na wanasiasa, wananchi wa kawaida wa zenj, na bara tunashirikiana sana,

Watu wa kawaida hata kabla ya Uvamizi wanashirikiana katika mambo ya jamii wala Hakuna matatizo yoyote. Matatizo yameletwa na Nyerere baada ya kuvamia na kuuwa watu kwa maelfu , na kila uchaguzi unapokuja kuuliwa watu.
 
Zanzibar wana vijisheria vya kishenzz shenzz sana
 
Nimeenda kwa mara ya kwanza Zanzibar last week, ovyo kabisa. Ni wabaguzi mno, maneno kama "we wa bara" na "waDanganyika" nimeyasikia sana.

Tuko nao kimwili tu ila kiakili na kiroho hawako nasi kabisa, kiufupi HAWATUTAKI. Tunafanana lugha na rangi tu ila sisi sio wamoja hata kidogo. Muungano uvunjwe ili uundwe upya ama uvunjwe mazima, the latter is more preferable.
Kuna jamaa yangu anafanya kazi huko, hata wasichana hawamtaki sababu yeye ni mtu wa bara. Huwa anampakia kwenye boti msichana wake kutoka bara kila weekend ili apumzike.
 
Au zenji wanaendesha magari juu ya maji? 🤣🤣
 
Back
Top Bottom