Kwanini hili gazeti lisiconcentrate na habari za kuteswa kwa Mhariri Mkuu Kibanda? Kuna siri gani iliyojificha:frusty:?
hii hoja yako ipo na inasimama japo wengi tutaikataa! Maana wanasema nchi inaendeshwa na watu na watu wa kweli wako jfkumbe JF tunaweza kuongoza nchi,hii habari wameisoma cluods Jerald Hado akachangia kuwa imewahi kujadiliwa kwenye forum ila hakuitaja hadi PJ alipomwambie kuwa ni jamii forum
Tusubiri tuone kama slaa atajibu hizi tuhuma,,,,habari hii ilikuwa kwenye mitandao sasa ipo kwenye gazeti,,bila shaka kuna kila sababu kwa dr kujisafisha katika hili,,,!!!
Mbona ameshajibu.Tusubiri tuone kama slaa atajibu hizi tuhuma,,,,habari hii ilikuwa kwenye mitandao sasa ipo kwenye gazeti,,bila shaka kuna kila sababu kwa dr kujisafisha katika hili,,,!!!
By Zitto
Mimi binafsi nikikutana na Ben Saanane leo naweza kupishana naye maana sijawi kumwona, wala kukutana naye. Ndugu Ben Saanane nimewasiliana naye kwenye simu mara mbili au tatu kuhusu masuala yake ya kitaaluma au pale alipohisi kuonewa ndani ya chama. Sijawahi kukutana naye hata siku moja. Kama nasema uwongo yeye binafsi aje hapa kukanusha.
Mkuu Magwangala, hizi ni hesabu za functions darasa la 4, if x=y and y=z, then x=z na yumkini (probability) darasa la 5 kama ukizungusha shilingi mara 1, unaweza kupata kichwa au mwenge, then ukizungusha mizunguko miwili, probability ni kupata au kichwa sifuri, au kichwa kimoja au vichwa viwili, pia unaweza kupata mwenge sifuri, mwenge moja au mwenge 2.Unazungumza vitu gani Pasco?umekuwaje siku hizi mkuu?
Ben saanane nakushauri hao madogo wapeleke mahakamani this is too much, wakamuliwe hela zote walizohongwa na magamba! Plz do it kurudisha heshima!!.
Mbona ameshajibu.
Lakini na wewe kwa kutumia akili yako tu unasemaje? Maana Zitto mwenyewe amekana kuwa hajawahi kukutana na Ben Saanane.
Here, due to integrity of Zitto, we presume that Zitto was telling nothing but the truth.
......Sasa kwa sababu kiongozi wangu Zitto Kabwe ameibuka na kujaribu kukanusha na kupotosha imebidi nije niweke sawa upotoshaji huu japo kwa kifupi:
Ndugu Zitto,
Mosi:
Sishangazwi na kauli yako kwamba hunifahamu. Ni muendelezo wa siasa zile zile za kutosimamia ukweli na kuendekeza siasa za uongo na upotoshaji. Nimemkumbuka Mwanasiasa Mzee Stephen Wassira (Aliyekitabiria CHADEMA kwamba kitasambaratika) aliposimama na kumkana Mwanafamilia wake mbele ya vyombo vya habari kwa sababu ya siasa na katika mkakati wa kuendeleza ghiliba. Kama mwanasiasa wa Tanzania anaweza kumkana hata mwanafamilia au kusema chochote hakuna la kushangaza.
Sasa, kwa kuwa ushahidi ninao wa jinsi tunavyofahamina na jinsi tulivyoshirikiana kuwashughulikia viongozi wa juu wa chama pamoja na uhusika wetu katika hujuma dhidi ya chama nitaomba chama changu sasa kiitishe kikao cha dharura ili nimwage mambo yote nyeti na ushahidi nilio nao ndani ya vikao. Naamini katika vikao kwa kuwa napenda kuona CHADEMA kikikua kama Taasisi imara ya mabadiliko.
Jana nilimwambia Dr. Kitila haya mambo baada ya wewe kuongea nae na kunitaka mimi niingie JF nikanushe thread hii iliyoanzishwa na Mamuya. Kumbe shinikizo lote ulitaka nikusafishe tu, kitu ambacho sikuwa tayari kufanya. Ushahidi nianao pia! Ulipoona imeshindikana mimi kumkana Exaud Mamuya, wewe ukaamua kuja huku kuja kunikana. Hizo rhetorics unazotumia katika dhana ya kujenga ukabila kwa kufanya ulinganisho wa Mamuya na Ben Saanane ni muendelezo wa propaganda chafu dhidi ya chama ambazo mimi na wewe tulikuwa tukizitumia kuhalalisha kazi yetu hii ambayo kimsingi niliamua kuachana nayo na sikuwa tayari kuendelea kuishiriki.