Mtanzania: Dr. Slaa atajwa kumtuma Ben Saanane kummaliza Zitto

Mtanzania: Dr. Slaa atajwa kumtuma Ben Saanane kummaliza Zitto

Status
Not open for further replies.
furaha ya CCM ni kushuhudia anguko la Dr.Slaa kabla ya 2015, ila kazi imekua ngumu sana kwao...Dr.Slaa wewe ni tumaini la watanzania waliokatishwa tamaa na utawala wa CCM,hivyo tunakuomba usiyumbishwe na propaganda za kijinga simamia unachokiamini.!!!
 
kumbe haina maaana ya kununua magazeti sasa,hii habari imezungumzwaaaa weee mpaka imechakaa mbaya zaidi na watu walewale kwa malengo yaleyale.iweje leo ndiyo mtanzania liandike?lilikuwa wapi?au wanaandika leo kwa malengo gani?.hao kina shonza,mwampamba na wenzao kama wanaushahidi wa wanachokisema kwanini wasichukue hatua zinazostahili za kumlinda wanae mtumia kuwaweka kwenye chati kisiasa?maana hawa vijana wenzetu bila kutaja Zito hawawezi kufanya kazi za siasa.cha kushangaza Zito mwenyewe hana habari nao maana kazi yao kwake ilishakwisha maana Zito ni kiongozi wa chadema na wao ni makada wa ccm sasa wapi na wapi?any way mjini hapa kila mtu na ujanja wake wa kuishi.
 
Baada ya CHADEMA kufanikiwa kuondoa masalia sasa wameanza kutumia media na waandishi makanjanja wenye njaa kali kuchafua cCHADEMA

CHADEMA ipo kwa mpango wa MUNGU hakuna wa kukihujumu

Zitto tumemwomba apambane na hiyo mkata ba 17 mpaka ajue nini kilichopo ndani na yale madola ya Uswiss ( Kazi ya bunge ljalo)
 
Najutia muda wangu kusoma huu upuuzi,ningekuwa nimeshaingiza hel kibao,
 
Wanasema hivi:
Anamtaja mtu aliyetumwa kumuua Zitto kuwa ni Ben Saanane, ambaye aliangusha karatasi ya nailoni iliyokuwa na ungaunga unaosadikiwa kuwa sumu na kuonekana kwa watu waliokuwa eneo hilo, akiwemo Zitto mwenyewe pamoja na aliyekuwa Naibu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba.

Zitto anasema hivi
Sijawahi kukutana naye hata siku moja. Kama nasema uwongo yeye binafsi aje hapa kukanusha

Hatudanganyiki!
 
..........Ule Wakati wa kuanza sasa chafu za maji taka kupitia magazeti ndo unaanza .... gazet la MTANZANA linajulikana kuwa ni mali ya nani na liko kwa misingi ipi.... litaingia kuwa miongoni mwa magazeti uchwara...dawa ni kulikwepa
 
Ben saanane nakushauri hao madogo wapeleke mahakamani this is too much, wakamuliwe hela zote walizohongwa na magamba! Plz do it kurudisha heshima!!.
 
Kama CHADEMA ndiyo kwanza wanahangaikia kuingia ikulu kama chama pinzani na wamekuwa hivi tunavyowasikia akina Shonza na Mwampamba kuhusu Zitto, je serikali iliyokaa madarakani kwa miaka zaidi ya 50 imetenda uovu kiasi gani!!!

Nasema hivi kwasababu MTOTO HUFANYA YALE WAZAZI WAO WAYAFANYAYO. Very few are born as TALENTED but the rest are born as INHERITED. What if true Dr Thlaa (Slaa) might have done is just what CCM have been doing for over fifty years.

But if this is part of "politics" then Shonza and if Mwampamba will accent this information to second the Shonza allegation then Ben Saanane has to go to court to get cleaned or otherwise Ben Saanane must be arrested for questioning. Shonza Think Befor You Leap.
 
Anamtaja mtu aliyetumwa kumuua Zitto kuwa ni Ben Saanane, ambaye aliangusha karatasi ya nailoni iliyokuwa na ungaunga unaosadikiwa kuwa sumu na kuonekana kwa watu waliokuwa eneo hilo, akiwemo Zitto mwenyewe pamoja na aliyekuwa Naibu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba.
Mimi binafsi nikikutana na Ben Saanane leo naweza kupishana naye maana sijawi kumwona, wala kukutana naye
Haya hapa angalieni uongo wa walau mmoja wa wahusika wa stori. Gazeti la Mtanzania linasema Ben Saanane aliangusha sumu na ikaonekana na watu waliokuwepo eneo hilo, akiwemo Zitto mwenyewe. Zitto anasema hajawahi kukutana na Ben Saanane na hata wakikutana hatamjua. Sasa nani mkweli na nani muongo, Gazeti Mtanzania/Shonza au Zitto au wote hawa?
 
Kwanini hili gazeti lisiconcentrate na habari za kuteswa kwa Mhariri Mkuu Kibanda? Kuna siri gani iliyojificha:frusty:?
 
Hata wasemaje,Dr Slaa hawezi kuachia funguo za jeneza la CCM!
 
Haya hapa angalieni uongo wa walau mmoja wa wahusika wa stori. Gazeti la Mtanzania linasema Ben Saanane aliangusha sumu na ikaonekana na watu waliokuwepo eneo hilo, akiwemo Zitto mwenyewe. Zitto anasema hajawahi kukutana na Ben Saanane na hata wakikutana hatamjua. Sasa nani mkweli na nani muongo, Gazeti Mtanzania/Shonza au Zitto au wote hawa?
Halafu unga wenyewe mwekundu!
Alisema wakiwa katika maongezi, huku Saanane akionyesha kuzidiwa na kilevi alichokuwa amekunywa, alitoa bahasha ya kaki yenye fedha ili alipie gharama za vinywaji vya wote ambayo ilidondoka na ndani yake ikatoka karatasi ndogo ya nailoni ikiwa na unga mwekundu.
Walikuwa gizani?

Zitto alikuwa anakunywa kinywaji gani hadi wachague sumu nyekundu iwekwe kwenye kinywaji chake? Hivi hata hao wengine si wangeshtuka?

Lakini kwa nini uhalifu upelekwe kwenye magazeti na si polisi?
 
Yaani miandishi ya habari ya Tanzania kwa sasa inashinda JF kutafuta habari za kuandika kwenye magazeti,
lakini walivyo makanjanja hawaandiki source kuwa ni JF.kwa mitindo hii mtang'olewa meno sana ili waendelee
kutafuta kusingizia CDM na Dr Slaa.

Wakati wenzao wakitoa vitu vya ukweli na kufanya kazi vyombo vinavyolipa kwa dola na paund wao wanakaa na shoza na mwampamba wasio na ajira kuwahoji
 
Hawa jamaa hawana akili kweli waliotunga hii story, haiingii akilini mtu unaenda kufanya tukio baya kiasi hiki halau ulewe chakari hadi uangushe "Zana" yako, kwa kipande hiki tu nimeidharau habari nzima, kwaheri

Alisema wakiwa katika maongezi, huku Saanane akionyesha kuzidiwa na kilevi alichokuwa amekunywa, alitoa bahasha ya kaki yenye fedha ili alipie gharama za vinywaji vya wote ambayo ilidondoka na ndani yake ikatoka karatasi ndogo ya nailoni ikiwa na unga mwekundu.
 
CHADEMA ITAWATESA SANA. Hivi Wasira hajarudishwa Gombe national park.
 
:A S 39: hebu ngoja kwanza........:nono: siasa chafu, mwanzo wa mwisho wenu ndio huu, na bado ngoja ije katiba mpya......mtajuta MAGAMBA
 
Kuna jambo moja najiuliza nalo ni kwanini mwandishi wa habari hii hakumuhoji Zitto swala hili!

Kama ni swala la kuwa JKT zitto ameshamaliza mafunzo,sasa kwanini Zitto hajatafutwa kwani kama angemtafuta hata kwa simu lazima angeripoti kwenye habari hii kuwa Zitto alitafutwa ila hakupatikana au vinginevyo.

Ni wazi hakufanya jitihada ya kumtafuta mh.Zitto.

Je,ni kwa madhumuni gani?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom