Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
- Thread starter
-
- #41
Yah ni kweli mkuu, wengi ni wa Dar haswa maeneo ya Mbagala, TMK na Tandika yake.Wanaozamia huko wengi wametoka Dar usitegemee uchakalikaji wa njia za halali hapo
😂😂😂🤣🤣🤣watoto wanasema BINDUKI
Watanzania wengi ni kama vile tunalaana ya Mungu, maana miaka nenda rudi hatubadiliki iwe nchini au nje ya nchi bado tuko nyuma kwa kila kitu.WaTz sijui nini kinaturoga, malezi, elimu au ainavya maisha yetu?
Ni bora nipige gitaa mkuu, huenda kuna wale ambao watazinduka kutokana na maelezo yetu hapa JF.Unapiga gitaa Mbele ya kwaya ya mbuzi
Tusikimbilie kuwalalamikia wenzetu kabla kwanza ya kujilalamikia sisi wenyewe. Maisha tunayoishi wabongo nchi za wenzetu laiti wangeishi raia wa nchi zingine hapa nchini kwetu tungelalamika sana kuwa raia hao wanakuja kutuharibia watoto wetu.Nimezika washkaji wanne tena wawili madogo kwangu wamepigwa shaba yaani kweupe hakuna kesi wala nn tumezika ...Kingine hebu nendeni kule Facebook...
Yah anaweza kuwa mtu poa machoni, lkn kazi au biashara anayofanya ikawa tofauti na muonekano wake.Jamaa anaonekana ni mtu poa tu, shida ni nini wakuu...japo wanaume tunapitia maswahibu mengi sana.
Jamaa sijui imekuwaje?....
Tatizo south ukizinguana na mtu anakuwinda hakubali yaishe.
Yah panya road anataka akifika huku aendeleze mtindo wake wa kupiga ndole kwenye mkusanyiko wa watu wengi, matokeo yake anakwenda kumpiga ndole mtu sio na kuishia kaburini.Sio mafala bali hawapendi mafala. Wabongo nyookonyoko nyingi. Panya road wanakwenda kuishi south
Mkuu umesoma vizuri kweli?Rudini nyumbani, huku mapori mengi yanahitaji nguvu kazi
Tozzy nyangema 😂😂😂Kwahiyo unamsema mwanangu NYANDU TOZZY sio?
Amiin 🤲Kila mtu ako na destiny ya life yake though alazwa pema peponi.... kamanda
Woza pagamisa, awee ma bru🤣🤣🤣🤣Bora wawapunguze punguze huko huko,maana wakishafeli maisha wanarudi huku na itikadi zao za 26,27 wanatusumbua.
Dah mle mle 🤣🤣🤣🤣Wosa pagamisa, awee ma bru🤣🤣🤣🤣
Cape Town imejaa watoto wa Kitanga wana miji yao kabisa. Ukienda Athlone (Vlei - inatamkwa flei) ni kama vile upo Ngamiani Tanga.Wanaozamia huko wengi wametoka Dar usitegemee uchakalikaji wa njia za halali hapo
Uliloongea ni kweli na wengi shughuli zao ndio hizi nilizoeleza hapa.Cape Town imejaa watoto wa Kitanga wana miji yao kabisa. Ukienda Athlone (Vlei - inatamkwa flei) ni kama vile upo Ngamiani Tanga.
Kwa South Africa Cape Town naijua vilivyo maana nimeishi huko miaka 8. Japo niliishi kihalali sio kwa mazabe.Uliloongea ni kweli na wengi shughuli zao ndio hizi nilizoeleza hapa.
Bila shaka wewe ni mwenyeji unajua ninachoongea mkuu.
Mkuu kwa aina hii ya maisha wanayoishi watanzania wenzetu hata waende Marekani hawawezi kutoboa. Kama ulivyosema kwamba wabongo wengi wanapenda maisha ya short cut, ila hawawezi kujishughulisha na kazi za mikono yao. Wengi wamefeli kwa sababu ya kutokujua au kujishughulisha na kazi.Nimetoka Maitland -Cape Town mwaka 2012,niliporudi Bongo nikawa nawashauri madogo hasa wanaopenda Ubaharia wa Kisela wasiende Kaburu kwa kuwa hakuna maisha,wajaribu kuingia Namibia tena wakiwa na Leseni au ufundi wa nguo,
Kuna kitu kikubwa inabidi kifanyike katika nchi hii,vijana wengi wanapenda Utajiri lakini hawajui mbinu au maarifa ya kufikia Ndoto zao matokeo yake yanakuwa machungu kwao,
Ni rahisi kutajilika ukiwa Tanzania kuliko Afrika Ya Kusini,tufundishe mbinu na maarifa ya kutoboa kwa wadogo zetu ili kuwasidia kuondokana na stori za vijiweni.
Asante mkuu kwa maelezo mazuri yaliojitosheleza. Kifupi ulichoandika ndio uhalisia wa kile kinachoendelea hapa.Kwa South Africa Cape Town naijua vilivyo maana nimeishi huko miaka 8. Japo niliishi kihalali sio kwa mazabe.
Asilimia kubwa ya vijana wa kitanzania wanauza madawa (vipinchi) na hawa wengi wao huishia kuwa watumiaji wakuu kupelekea kuwa vibaka.
Wengi wanauza vitu vidogo vidogo mabarabarani (ndau) wengi wao hivyo vitu vidogo vidogo huwa ni geresha ya kuuza vitu vya wizi (simu zaidi) na bangi.
Kazi nyingine kubwa ni vinyozi (bora hawa wanaishi kihalali japo wengi wao wakipata channel wanaingia kwenye kuuza madawa).
Kipindi nilichokuwepo huko kulikuwa na jopo kubwa la vijana matapeli kwa kupitia uganga feki na mchomoko (kurubuni watu kuwa wanaweza kuzalisha pesa zaidi kwa chemicals halafu wanakimbia na pesa za watu). Wengi sana waliuliwa na wale waliowaibia.
Kwa kifupi asilimia kubwa ya wabongo waliopo South Africa wana ndoto moja tu ya kuwa madon wa kuuza unga na wengi wanaamini ili hili kutimia basi apate safari ya upunda kwenda brazil au pakistan kubeba unga. Wengi huishia kudhulumiwa na waliowabebesha au kukamatwa kuishia jela.
South Africa ina fursa nyingi mno ukiwa unaenda kimstari. Na unaweza hata usihisi kuwa upo ugenini.