Mtazamo huru: Kizazi cha wanaume wa miaka ya 1980s hadi 1990s ndo cha mwisho kufaidi mapenzi ya kweli kutoka kwa wanawake

Mtazamo huru: Kizazi cha wanaume wa miaka ya 1980s hadi 1990s ndo cha mwisho kufaidi mapenzi ya kweli kutoka kwa wanawake

Mngoni asiyepiga gambe

Senior Member
Joined
May 4, 2017
Posts
151
Reaction score
318
Achilia mbali raha ya kusoma whatsap text au kupokea video call kutoka kwa mpenzi umpendaye, unaijua raha ya kupokea barua ukiwa shuleni toka kwa mpenzi wako ikiwa imefungwa na sticker za kopa na ndani unakutana na dedication za nyimbo bomba enzi hizo kama Mimi na wewe Mr blu, Nataka niwe na wewe milele , LOVE YOU wyclef Jean,When i see you Fantasio n.k ukiachilia hilo mambo mengine yaliyofanya mapenzi ya enzi zile kuwa na kumbukumbu ya kipekee ni kama yafuatayo.

1. Hakukuwa na simu mkononi so appointment ni zile za kusubiriana sehemu ama kumtuma shoga ake demu akuletee hadi eneo la tukio na kama anakuja kwa daladala basi mlume ukagande stand siku nzima macho kwenye kila abiria anaeshuka 😀 but yet hakukuwa na fake promise ingawa uvumilivu ulihitajika sio poa

2. Msoto unaopitia mpaka kumuweka demu sawa yaani kama una nyota nzuri ni mwaka mmoja hapo sizungumzii kuja kupewa tunda special

3. Pisi ikija home kupewa tunda kidume hadi utoe chozi ila uzuri hakuna kuombana nauli wala hela ya kusuka yaani sometime pisi unaipa hela inakataa 😀

4. Possibility ya kukutana na binti bikra ilikuwa kubwa au tena unamkuta mtu ana feelings kama zote kwenye tendo siku hizi binti unapeleka moto simu yake ikiita utasikia anasema " Atakuwa Mama huyo ananitafuta "😀

Sema nyi madogo wa 2000 siku hizi mnapigwa sana .
 
Duuuh
20241116_173101.jpg
 
Umenikumbusha enzi hizo nipo kigonsera High School.... Nilikua nikimuandika I LOVE YOU Mtoto Anna Ndunguru wa Songea girl's, kunijibu I LOVE YOU TOO hapo ni miezi mitano au sita.
Siku unayojibiwa shule nzima mwamba wewe wengine mijusi😀😀😀😀 sema kaigo ilikuwa unyama mwingi sana
 
Na ndo kizazi cha mwisho kufilisiwa kisa mapenzi, hii generation mpya ya nipe nikupe itakua na maisha bora Sana huku ikipata utamu bila kupangiwa ratiba
nyinyi ndo kizazi cha kataa ndoa kila siku mnapigwa matukio 😀
Si malejendari hauna mbanga hizo coz tunajua ku scout mtu sahihi
 
Nikajua utasema wanawake wa 1980s hadi 90s ni waaminifu kumbe umeleta zile mambo za 'miaka yetu tulifaidi....'

Haya, wa 2000s tutakumbuka zile photoshoot tulizokuwa tunaenda pamoja, kupostiana status na ig, kula pizza na burger pamoja.....

Kwenda swimming, cinema....

Na wale walioopoa pisi kali kwa kuwa madancer shuleni watatamba....

After school bash zile, mademu wanafika bila kiingilio, ukiweza unakamata unaemmudu....
 
Kwani wanaotakiwa kufaidi penzi ni wanaume tu wanawake ni wasindikizaji wa mapenzi tu? Acha ubinafsi hata wanawake pia wa enzi hizo walifaidi sana, ila wababa wa sasa hawana hata muda wakukaa na wake zao, wapo vuruvuru kama matenga ya ntarali hamna kitu kabisa, Wana miili mikubwa lakini haina maana.
 
Nimegusia suala la wanawake kuwa loyal kwa wanaume imagine mnapeana appointment tukutane chini ya mbuyu saa 12 jion na mtu anatokea on time bila kukumbushwa kwa simu wala nn ,ilikuwa ni uaminifu na utiifu wa hali ya juu
 
Mimi ni mwanaume nazungumzia experience yangu atatokea mwanamke pia nae atazungumzia experience yake
 
Nimegusia suala la wanawake kuwa loyal kwa wanaume imagine mnapeana appointment tukutane chini ya mbuyu saa 12 jion na mtu anatokea on time bila kukumbushwa kwa simu wala nn ,ilikuwa ni uaminifu na utiifu wa hali ya juu
ni genye tu

hamna cha uaminifu

unadhani hata leo mabinti hawaliwi vichumini na mikahawani?
 
Back
Top Bottom