- Uzi huu ni mrefu.
- Ukichangia naomba ujikite Zaidi katika kutoa maoni yako lakini kukosoa kunaruhusiwa.
Binafsi nadhani maamuzi haya yangechukuliwa mwezi mmoja uliopita pale Waziri Mkuu alipotangaza kuzifunga shule na vyuo, lakini haikuwa hivyo badala yake shule zilifungwa kisha hakukuwa na mpango mkakati madhubuti wa kukabiliana na COVID-19, Zaidi ya makatazo ya kuepuka mikusanyiko na kunawa mikono na maombi. Lakini huu sio muda wa kuendelea kulaumiana zaidi ni wakati wa kupeana mawazo na kushauriana.
Pia bado naamini athari za kiafya kama watakaofariki kutokana na Virusi hivi bado watakuwa wachache kuliko watakaoathirika kutokana na athari za kuwepo ugonjwa huu haswa suala la uchumi na elimu. Hivyo ni lazima kuwe na mpango mkakati wa haswa kuhakikisha kuwa baada ya muda fulani tuwe tumefikia jambo Fulani.
Anyway, binafsi kama ningekuwa na mamlaka ningetumia njia hii kutatua tatizo la hili |Ushauri wangu.
- Kwanza ni lazima kila mmoja ( Serikali na wananchi kwa ujumla) kuwa na fikra ya kutatua tatizo na siyo kutengeneza faida, waswahili husema hasara roho, pesa makaratasi na zinatafuwa, huu ni wakati wa Serikali na wananchi kujua kuwa nchi iko kwenye vita kubwa sana na inapambana na adui wa ajabu asiyeonekana mwenye madhara lukuki ikiwemo kupoteza maisha na hali mbaya ya uchumi, amapo kama Serikali ni lazima iwe tayari kutumia rasilimali zilizopo katika kunusuru Taifa, rasilimali hizi kama fedha na watu na miundombinu
Nini cha kufanya?
- Serikali inainishe maeneo ambayo yako hatarishi zaidi katika maambukizi ya virusi vya Corona, naamini yako wazi. Maeneo mengi ya mjini yana muingiliano mkubwa wa watu kutokana na shughuli zao za kiuchumi.
- Baada ya kuanisha maeneo hayo, viongozi wa mtaa na katika maeneo yalioainishwa wapite wachukue idadi ya watu wote katika mtaa husika wakizingatia mambo yafuatayo:-
- Idadi ya watu katika nyumba husika (hili nimesikia limefanyika maeneo ya Dar sina uhakika.
- Hali yao ya kiuchumi
- Kuchukua mawasiliano wa watu wawili waliopo katika nyumba hiyo na kuacha mawasiliano ya viongozi wawili wa mtaa husika.( namba za simu zenye uhakika).
- Baada ya hatua ya kuainiasha maeneo na kujua wakazi namba ya wakazi husika na hali zao za kimaisha, Serikali ikishirikiana na wadau, waangize bidhaa muhimu kutoka nje( kwenye upungufu) pia kwa wakati huu Serikali inunue au iongoze vifaa vya kupimia Virusi vya corona Viwepo kwa wingi zaidi visambazwe kila wilaya. Kama nilivyosema huu ni wakati wa kutumia rasilimali tulizonazo katika kupamba na janga hili si wakati wa kuanza kuangalia faida.
- Hatua ya nne ni Serikali kugawa chakula kwa familia zilizo na uchumi duni ambao hawana uwezo wa kuishi kwa siku ishirini na moja wakiwa ndani. Hatua hii inahitaji unaminifu na uadilifu kwa viongozi wa serikali wanaokadiria hali za kiuchumi za wananchi na pia kwa wananchi ambao watakua wanaeleza uhalisia wa maisha yao ili wasiibebeshe serikali mzingo ambao wanauweza, wasiwakoseshe wale wenye uhitaji na wala wasionewe. Watu wanosihi kijijini wengi chakula wanacho, shida walionayo ni hela ya kusagia mahindi, hela ya sukari chunvi na mafuta ya taa.
- Hatua ya tano Serikali itangaze lockdown kwa siku ishirini na moja (21) . Hapa wananchi wakiwa tayari wana mahitaji muhimu hasa chakula. Katika kipindi hiki.
- Serikali itumie vyombo vya usalama katika kuhakikisha watu wanafata utaratibu lakini wawe ni wenye kuelewa kuepuka maafa kama yaliotokea nchi nyingine.
- Tangazo la kuwa lockdown liwe mapema na watu kufanya maandalizi ikiwa ni pamoja na wale watakao pewa msaada mapema
- Katoka kipindi hiki cha wiki tatu, kodi za biashara, umeme na maji viwe free kwa ambao luku zao zitaisha basi wasizime, pia wakadirie matumizi ya maji ya wiki tatu wasihesabu katika bili ya maji.
- Mawasiliano ya karibu ya viogozi wa serikali katika kujua kinachoondelea latika kila kaya, hasa kwa dharura ya wagonjwa na mama wajawazito kuweza kupatiwa uduma.
- Wale wanaotamulika kama homeless na watoto wa mitaani, watafutiwe sehemu ya kuhifadhiwa( nashauri kwenye walo moja la kambi ya jeshi mana watakua na adabu, au watakapo wekwa wasimamiwe na wanajeshi).
- Mipaka ifungwe kabisa.
- Wiki ya pili ya lockdown, yaani siku ya kumi na nne (14), serikali ichukue sampuli ya watu wawili au mmoja kutoka katika kila nyumba, nashauri awe yule anaetoka toka sana( mtafutaji) na yule mtu mzima Zaidi au ambao anaumwa. Lengo na madhumuni ni kua,
- Kwa kipindi cha wiki mbili kama kama mtu alikua na virusi basi atajulikana.
- Lengo la kuchukua mtu mzima au yule mgojwa ni kua, mwenye virusi anaweza kua yuko na kinga madhubutu hivyo kwa mtu mzima itasaidia hugundulika mapema.
- Kuchukua watu wawili au hata mmoja kila nyumba kutasaidia kupunguza utumiaji wa rasilimali katika upimaji. Mfano kama idadi ya watu katika kaya yenye nyumba 300 na watu 2000, then tunapima 300 au 600 (kama wakichukua kila nyumba wawili) badala ya watu 2000.
- Baada ya kuchukua sampuli kutoka katika kila nyumba, kutegemea na siku watakazo tumia. Kasha nyumba zitakazo kutwa na maambukizi watawekwa katika ungalizi( kutotoka au kuwapeleka katika maeneo maalumu yaliotengwa ) na kui disinfect nyumba.
- Baada ya kuchukua familia zilizokutwa positive, kutegemea na siku zilizotumika kupima na kupata majibu, na kufanya mapendekezo ya namba saba, the tunaweza kufungua shule na shughuli zikaendelea huku tukiendelea na tahadhali, suala la level seat likendelea, kunawa mikono na uvaaji wa barakoa.
- Katika kipindi chote hicho , Serikali isisite kufanya utafiti katika jamii mbalimbali kwa asili yao kwa jinsi walivyoweza kupambana na magonjwa ya mfumo wa hela ili kuangalia uwezekano wa tiba mbadala.
Haya ni mawazo yangu ya jinsi ninavyoona jinsi gani ya kuweza kupambana na suala hili.
Amani ya Bwana iwe nanyi wote.
---MICHANGO---
Kwa habari zaidi. soma:
Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga - JamiiForums
Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus) - JamiiForums