Mtazamo wa vijana wa Afrika kuhusu China waendelea kuboreka

Status
Not open for further replies.

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111255268459.jpg

Elias Gebreselassie alilelewa Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, na kama wenzake, amekuwa na fikra kuwa kwamba majengo marefu, maduka makubwa na barabara kuu zinaweza kuwa maonyesho tu katika sinema za Hollywood.

Lakini katika kipindi cha muongo mmoja uliopita Gebreselassie amejionea kwa hakika mji wa Addis Ababa ukibadilika kwa muonekano na kwa miundo mbinu.

Bila shaka sio sinema tena lakini ni ukuaji unaowezeshwa na ushirikiano wa China na Ethiopia katika sekta ya uwekezaji .

Na sasa Gebreselassie mwenye umri wa miaka 34 anasifu uwekezaji wa China katika miundombinu ya kisasa kama vile barabara na vituo vya kijamii, ambayo ilifanya mji mkuu kuwa jiji kuu la kimataifa linalopendeza na makao makuu ya Umoja wa Afrika.

Yeye ni mfano wa jinsi watu wa Afrika na hasa vijana wanavyoendelea kubadili mitazamo yao kuhusu China.

Gebreselassie anasema ufahamu wake kuhusu China umeongezeka sana baada ya kushuhudia mchango wake katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Afrika kupitia ujenzi wa maeneo ya viwanda, majumba makubwa ya biashara na reli za umeme.

“Hii imewahamasisha vijana wa Ethiopia kufahamu zaidi kuhusu China na watu wa China. Vijana wengi, kama vile wadogo zangu sasa wamechagua kusoma nchini China, na wengine wengi wanapendelea kwenda vyuo vikuu vya Ethiopia kusoma Kichina kupitia Taasisi za Confucius, "Gebreselassie anasema.

Anasema kuwa sinema za Kung Fu alizokuwa amezitazama akiwa mtoto zilimpa ufahamu wa utamaduni wa Wachina. Lakini pia anasema uelewa wake umejikuza zaidi kupitia uwezo wa kiteknolojia wa China na maendeleo ya haraka ya kiuchumi.

"Hivi karibuni, idadi inayoongezeka ya vijana wa Ethiopia pia wamepata uelewa mpana kuhusu China na mtindo wa maisha wa Wachina kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii kama TikTok pamoja na sinema za jadi,", anasema Worku, kijana mwingine wa Ethiopia.

Maoni ya vijana hawa wa Ethiopia ni sawa na wengine wengi kote barani Afrika.

William Douglas, kijana Mtanzania mwenye umri wa miaka 21, anasema kuwa vifaa vya nyumbani, vifaa vya ujenzi na mashine zinazotengenezwa nchini China ni maarufu miongoni mwa wateja nchini humo sababu ya ubora na bei nafuu.

"Hapa Tanzania, chapa za simu kama vile Huawei na Oppo ni maarufu sana," anasema Douglas.

"Tunatazama sinema nyingi za China," Anasema Nurdin, mwenye umri wa miaka 25, na kuongeza kuwa ufahamu wake wa utamaduni wa China umekua mwaka hadi mwaka kutokana na mabadilishano ya watu kwa watu.

Naye Ibrahima Diao, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop cha Dakar nchini Senegal, anaamini kuwa vijana wa Senegal sasa wanajua mengi zaidi kuhusu utamaduni wa Wachina kuliko walivyokuwa miaka michache iliyopita, akibainisha kuwa nchi hizi mbili zimekuza ushirikiano thabiti.

Vijana wa Kiafrika wamechangia pakubwa katika uhusiano wa kitamaduni na kiuchumi kati ya Afrika na China, kupitia kujifunza lugha ya Kichina na mabadilishao mengine ya kitamaduni na kiteknolojia.

"Vijana wa Afrika hakika wanaendelea kuwa na kiu ya kufahamu China na kushirikiana nayo tofauti na hapo awali. Wanavutiwa sana na maendeleo ya miundombinu yalioletwa na China katika nchi nyingi za Kiafrika, ” anasema Ndiye Kidet, mwanafunzi wa elektroniki katika Chuo cha Uhasibu cha Botswana.

Kidet alisema kuwa vijana wa Kiafrika wamepuuza hadithi za uwongo kwamba fadhili za China kwa Afrika ni zenye nia mbaya, na kuongeza kuwa China imethibitisha kuwa mshirika wa kuaminika katika harakati za Afrika za kujitegemea.

Utafiti uliofanywa huko Gaborone, Botswana mapema mwaka huu ulionyesha kuwa vijana wa nchi hiyo walithamini ushirikiano na misaada ya China kwa Afrika, kwani inasaidia sekta za kilimo, sanaa, michezo na utengenezaji.

Clifford Mboya, mtafiti wa Kenya aliyesomea siasa za kimataifa katika Chuo Kikuu cha Fudan mjini Shanghai, China anasema kuwa maisha yake nchini China yalikuwa ya kipekee kwa njia nyingi.

Anasema licha ya kuwa nchi hiyo ina changamoto zake kama nchi nyingine yoyote duniani lakini pia kuishi huko kulimsaidia kupanua mawazo yake katika maswala mengi.

“Nadhani ni nchi ambayo imejikita katika kufikia malengo yake. Ninapenda jinsi wanavyofuatilia ndoto zao na miradi yao na kuifanikisha", anasema Mboya.

Mboya anasema kuwa ripoti nyingi kwenye vyombo vya habari kuhusu China zilikuwa hasi kabla ya kwenda nchini humo.

"Lakini, ilivutiwa na kile nilichokiona, kwa sababu hakuna tofauti yoyote na hapa, ni kwamba tu wana mfumo wao wa kisiasa, maadili ya kazi yao na utamaduni ni tofauti. Lakini mara tu unapoelewa jinsi mifumo inavyofanya kazi huko, unaanza kuthamini utamaduni wao na njia yao ya kufanya mambo.”anaongeza.
 
Upvote 1
Kuna mawili: (a) ni kweli mchina amesaidia sana kwenye ujenzi wa miundo mbinu afrika, ingawa akina nanihii watakuambia ni maendeleo ya vitu, ila (b) mchina haleti free lunch na wala siyo mjomba wa afrika. Anataka kuwa mkoloni mpya wa afrika baada ya nchi za magharibi kiuondolewa.
 
Huwa naona ni heri ya China kuliko mataifa ya Magharibi ambayo ndiyo yameusimamia kucha uchumi wa mataifa ya Afrika miaka nenda miaka rudi. Masharti ya China yako wazi sana. Mfano, naijenga hii barabara/bandari/reli/nk halafu nitaitumia muda huu na nitakuwachia, ama utanilipa hivi. Nchi za Magharibi zina masharti ambayo ni laini (soft) lakini yanaathari kubwa sana. Watakupa mkopo lakini watakupa masharti ya namna ya kuendesha nchi kisiasa/kikatiba na kisheria, pia watakutengenezea sera na kukutaka uzifuate. Mchina hana habari na namna mnavyofikiri kuiendesha nchi yenu, yeye yupo katika manufaa ya kile alichokufanyia (kama ni barabara, bandari, reli, nk). Mambo kama "Structural Adjustment Programs-SAPs, Multipartism, LGBT, nk", yote yanatoka Magharibi, na wanaviweka karibu sana na hiyo wanayoita michango yao ya maendeleo. Na mbaya zaidi masharti yao mengi si ya kimsaada wa kuinua uchumi wa nchi wanazozisaidia.
Bahati mbaya tu wao ndiyo wameshikiria "media" za dunia, wao ndiyo namba moja kumpaka matope Mchina, na sisi tunajaa.
 
Huwa naona ni heri ya China kuliko mataifa ya Magharibi ambayo ndiyo yameusimamia kucha uchumi wa mataifa ya Afrika miaka nenda miaka rudi. Masharti ya China yako wazi sana. Mfano, naijenga hii barabara/bandari/reli/nk halafu nitaitumia muda huu na nitakuwachia, ama utanilipa hivi. Nchi za Magharibi zina masharti ambayo ni laini (soft) lakini yanaathari kubwa sana. Watakupa mkopo lakini watakupa masharti ya namna ya kuendesha nchi kisiasa/kikatiba na kisheria, pia watakutengenezea sera na kukutaka uzifuate. Mchina hana habari na namna mnavyofikiri kuiendesha nchi yenu, yeye yupo katika manufaa ya kile alichokufanyia (kama ni barabara, bandari, reli, nk). Mambo kama "Structural Adjustment Programs-SAPs, Multipartism, LGBT, nk, yote yanatoka Magharibi, na wanaviweka karibu sana na hiyo wanayoita michango yao ya maendeleo. Na mbaya zaidi masharti yao mengi si ya kimsaada wa kuinua uchumi wa nchi wanazozisaidia.
Bahati mbaya tu wao ndiyo wameshikiria "media" za dunia, wao ndiyo namba moja kumpaka matope Mchina, na sisi tunajaa.
Una mtazamo mfupi sana; mtu anajenga reli au bandari anaitumia miaka 99, si akimaliza muda huo anakuachia kutu tupu? Mtazamo wako ni wa kupenda vya bure, lakini unapata vya bure ambavyo havina thamani.

hayo mambo unayopinga ndiyo hayo wachina wanayatumia, lakini kama wewe kwa mfano siyo gay halafu serikali ikasema gay wote wana haki sawa na watu wengine wewe yatakuhusu nini, kwani hao gays watakuja kukupanda kwa nguvu? Serikali yetu ina sheria dhidi ya kulawiti, na kuruhus gay haina maana ya jufuta shera hiyo.

Multiparty system ndiyo tunayo kwa miaka takriban 30 sasa, je unailalamikai pia? imekuharibia nini? Structural adjustment programs ni swala la serikali yetu; siyo swala na nchi za Magharibi.
 
Bahati nzuri hujui unachochangia!!
Mosi, kitendo cha kusema tu SAPs ni suala la serikali yetu na sio suala la Magharibi ni wazi umekiri mapungufu ya SAPs na kuitupia lawama Serikali. Shida yako hapa inaonekana ni elimu tu, kasome vizuri ujue kuwa SAPs si ya Serikali, ni ya Magharibi (Mkuu, umeshindwa hata kutazama Wikipedia tu kabla ya kuandika? Structural adjustment - Wikipedia).
Pili, unaonekana kuwa na mawazo mafupi sana. Umeonekana kutetea ushoga na multipartism, na umeshikilia hapo wakati unaona kuna "nk". Umeonesha kutojua ilipo hoja. Hoja si mifano. Siku nyingine unapojibu tafuta hoja ilipo na usishambulie mifano (hii ikusaidie katika maisha yako yote).
Tatu, ni nani amekuambia miaka ni 99 tu?! Hivi na akili yako huwa unadhani kila "negotiation" inaleta 99?
Mwisho, bado hujanishawishi. Ni heri mimi niamue namna ya kuuendeleza uchumi wangu, kama ni kujenga madaraja, shule, barabara, bandari, nishati, reli, hospitali, nk, halafu nitafute muwezeshaji tukubaliane terms kuliko mtu aniletee hela na anipangie jinsi ya kuishi ili aendelee kunipa hiyo misaada.
 
Pumba tupu, hata kujenga hoja zako hujui badala yake unatumi unatumia muda wote kujitangza kuwa unajua zaidi ya wenzako wakati umeshindwa hata kuilewa hiyo article ya Wikipedia ambayo bado ni debated. Unasoma maana ya structural adjustment kama vile ni imposition from the west badala ya kujua kuwa ni economic redress kwa ya nchi husika. IMF au world bank wakiona ni program yenye matumaini ya kufufua uchumi wanaweza kusaidia, lakini siyo kuwa wao ndio wanalazimisha. Hawawezi kukukopehsa hela zao huku wakiona kuwa hutaweza kuzirudisha.

Mwaka 1981 Malima alitangaza structural adjustment program Tanzania bila kuwa na pesa zozote za IMF wala world bank, kwa vile Nyerere alikuwa kakataa kudevalue shilingi; je ile SAP ya Malima ilikuwa imetoka huko. Elewa maana ya phrase hiyo ya structural adjustmenet from economic point of view, siyo kwa definition longolongo unazoleta bila kuelewa maana yake. Hata mtu binafsi anaweza kufanya structural adjustement katika maisha yake kwa kuunguza matumizi anayoona siyo ya muhimu, na huenda kufanya kazi za ziada kujiongezea kipato. Kama nchi ina uchumi unaodoral, wakaomba mkopo IMF au World Bank, ni kweli benki itawataka watekeleze structural adjustement program kunusuru uchumi wao kabla ya kupewa mkopo huo, lakini maana ya structural adjstement ni zaidi ya IMF na world bank.

Iwapo wewe unadhani kutetea ushoga ni mawazo mafupi, ujue kuwa wewe ndiye huna mawazo kabisa. Maisha ya mtu binafsi wewe yanakuhusu nini. Kuna nchi wanazuia mwanamke kutoa mimba, je wewe kama ni mwanamke itakuhusu nini iwapo wewe huna haja ya kutoa mimba. Unapokaa ukatumia muda wako kufikiria maisha ya jirani yako kalala na nani badala ya kuangalia maisha yako mwenyewe ndiyo mwanzo wa kutokuwa na mawazo; mambo ya ngoswe mwachie ngoswe!. Serikali kusema haina haja ya kuangalia nani analala na nani haina maana kuwa inakulazimisha wewe uwe shoga ili hali hutaki.

Mikataba yote mikubwa ya infrastructure inayotolewa Chinani ya miaka 99 kumfanya mkopaji aweze kuwa analipa kidogo kidogo na kujiskia kama hana burdem ila collateral ndiyo huwa ni ya ajabu sana; kama hujui hilo basi usichangie lolote. Nchi zote za mashariki ya mbali: malaysia, Indonesia, Thailand, na Sri-Lank zimeikaaa kwa sababu hiyo. Ni elementary principle finacing; je wewe unayedai kujua negotiation, uliwahi kuingia nao mkataba ukanegotiate wakakupa mkopo usiokuwa na masharti ya kuurudisha? Hata mkopo wa benki hapa ndani unakuja na masharti kwamba uwe na colateral, na ile periodic payment inatokana na urefu wa kipindi cha mkopo huo.
 
Mahusina yeyote lazima yawe mutual na win win situation must prevail. Inapokuwa mahusiano hayo hayajajengwa juu ya hilo basi uhusiano huo hufaidisha upande mmoja. Shida ya Waafrica ni moja Nchi inaweza kuja na proposal ya win-win anatokea mmoja wa Waafrica anajitokeza upande wa pili na kusema oor tufanye hivi na mimi nipeni kidogo. Kwa hiyo sisi ndio tunaoharibu na kuwafundisha Nchi za nje corruption. Waafrica wengi hawapo serious when it comes to National interest, ubinafsi unatangulizwa basi kila kitu kinaharibika na kusingizia wageni. Kama sisi hatuna good negotiators what do you expect tutaliwa tu. Negotiator ni mtoto wa dada hana qualification unatarajia nini.
 
Hii hoja naweza kuielewa kama tunafanya biashara na nchi za magharibi, Japan au Korea Kusini lakini sio China. Wachina wamekaa kiwiziwizi sana linapokuja swala la mikopo hivyo hata kiongozi wako akiwa mzuri haitosaidia sababu hatofikia makubaliano nao ndomaana wanapenda sana nchi za madikteta kufanya nazo kazi. Kwanza sijawahi kuona nchi yoyote iliyoneemeka kwa mikopo au mahusiano mazuri na China( kama ipo utaniambia). Kifupi ni watu wa hovyo na siwaoni kama mbadala wa nchi za magharibi.
 
Huwa naona ni heri ya China kuliko mataifa ya Magharibi ambayo ndiyo yameusimamia kucha uchumi wa mataifa ya Afrika miaka nenda miaka rudi. Masharti ya China yako wazi sana. Mfano, naijenga hii barabara/bandari/reli/nk halafu nitaitumia muda huu na nitakuwachia, ama utanilipa hivi. Nchi za Magharibi zina masharti ambayo ni laini (soft) lakini yanaathari kubwa sana. Watakupa mkopo lakini watakupa masharti ya namna ya kuendesha nchi kisiasa/kikatiba na kisheria, pia watakutengenezea sera na kukutaka uzifuate. Mchina hana habari na namna mnavyofikiri kuiendesha nchi yenu, yeye yupo katika manufaa ya kile alichokufanyia (kama ni barabara, bandari, reli, nk). Mambo kama "Structural Adjustment Programs-SAPs, Multipartism, LGBT, nk", yote yanatoka Magharibi, na wanaviweka karibu sana na hiyo wanayoita michango yao ya maendeleo. Na mbaya zaidi masharti yao mengi si ya kimsaada wa kuinua uchumi wa nchi wanazozisaidia.
Bahati mbaya tu wao ndiyo wameshikiria "media" za dunia, wao ndiyo namba moja kumpaka matope Mchina, na sisi tunajaa.
Nakubaliapo mkuu
 
Kuna mawili: (a) ni kweli mchina amesaidia sana kwenye ujenzi wa miundo mbinu afrika, ingawa akina nanihii watakuambia ni maendeleo ya vitu, ila (b) mchina haleti free lunch na wala siyo mjomba wa afrika. Anataka kuwa mkoloni mpya wa afrika baada ya nchi za magharibi kiuondolewa.
kwa iyo africa tutakua watu wa kuliwa vichwa tu..ametoka mzungu sasa mchina🙁
 
Una mtazamo mfupi sana; mtu anajenga reli au bandari anaitumia miaka 99, si akimaliza muda huo anakuachia kutu tupu? Mtazamo wako ni wa kupenda vya bure, lakini unapata vya bure ambavyo havina thamani.

hayo mambo unayopinga ndiyo hayo wachina wanayatumia, lakini kama wewe kwa mfano siyo gay halafu serikali ikasema gay wote wana haki sawa na watu wengine wewe yatakuhusu nini, kwani hao gays watakuja kukupanda kwa nguvu? Serikali yetu ina sheria dhidi ya kulawiti, na kuruhus gay haina maana ya jufuta shera hiyo.

Multiparty system ndiyo tunayo kwa miaka takriban 30 sasa, je unailalamikai pia? imekuharibia nini? Structural adjustment programs ni swala la serikali yetu; siyo swala na nchi za Magharibi.
Umejibu vyema kabisa China ni mkoloni mpya wa afrika hana cha kupoteza wanao muona China kama mkombozi, ni wale wenye vichwa panzi wasio kuwa na mtazamo chanya.
 
Pumba tupu, hata kujenga hoja zako hujui badala yake unatumi unatumia muda wote kujitangza kuwa unajua zaidi ya wenzako wakati umeshindwa hata kuilewa hiyo article ya Wikipedia ambayo bado ni debated. Unasoma maana ya structural adjustment kama vile ni imposition from the west badala ya kujua kuwa ni economic redress kwa ya nchi husika. IMF au world bank wakiona ni program yenye matumaini ya kufufua uchumi wanaweza kusaidia, lakini siyo kuwa wao ndio wanalazimisha. Hawawezi kukukopehsa hela zao huku wakiona kuwa hutaweza kuzirudisha.

Mwaka 1981 Malima alitangaza structural adjustment program Tanzania bila kuwa na pesa zozote za IMF wala world bank, kwa vile Nyerere alikuwa kakataa kudevalue shilingi; je ile SAP ya Malima ilikuwa imetoka huko. Elewa maana ya phrase hiyo ya structural adjustmenet from economic point of view, siyo kwa definition longolongo unazoleta bila kuelewa maana yake. Hata mtu binafsi anaweza kufanya structural adjustement katika maisha yake kwa kuunguza matumizi anayoona siyo ya muhimu, na huenda kufanya kazi za ziada kujiongezea kipato. Kama nchi ina uchumi unaodoral, wakaomba mkopo IMF au World Bank, ni kweli benki itawataka watekeleze structural adjustement program kunusuru uchumi wao kabla ya kupewa mkopo huo, lakini maana ya structural adjstement ni zaidi ya IMF na world bank.

Iwapo wewe unadhani kutetea ushoga ni mawazo mafupi, ujue kuwa wewe ndiye huna mawazo kabisa. Maisha ya mtu binafsi wewe yanakuhusu nini. Kuna nchi wanazuia mwanamke kutoa mimba, je wewe kama ni mwanamke itakuhusu nini iwapo wewe huna haja ya kutoa mimba. Unapokaa ukatumia muda wako kufikiria maisha ya jirani yako kalala na nani badala ya kuangalia maisha yako mwenyewe ndiyo mwanzo wa kutokuwa na mawazo; mambo ya ngoswe mwachie ngoswe!. Serikali kusema haina haja ya kuangalia nani analala na nani haina maana kuwa inakulazimisha wewe uwe shoga ili hali hutaki.

Mikataba yote mikubwa ya infrastructure inayotolewa Chinani ya miaka 99 kumfanya mkopaji aweze kuwa analipa kidogo kidogo na kujiskia kama hana burdem ila collateral ndiyo huwa ni ya ajabu sana; kama hujui hilo basi usichangie lolote. Nchi zote za mashariki ya mbali: malaysia, Indonesia, Thailand, na Sri-Lank zimeikaaa kwa sababu hiyo. Ni elementary principle finacing; je wewe unayedai kujua negotiation, uliwahi kuingia nao mkataba ukanegotiate wakakupa mkopo usiokuwa na masharti ya kuurudisha? Hata mkopo wa benki hapa ndani unakuja na masharti kwamba uwe na colateral, na ile periodic payment inatokana na urefu wa kipindi cha mkopo huo.
Ukielimishwa huwa unachutama!
Ulikataa ukadai SAPs ni shida ya Serikali sio ya Western, nimekuwekea hadi link ujifunze zaidi bado unatafuta konakona. Sehemu tu ya hiyo link inakueleza "Structural adjustment policies were developed by two of the Bretton Woods institutions, the IMF and the World Bank, as the conditions that they attach to their loans since the early 1950s. These policies are typically centered around increased privatization, liberalizing trade and foreign investment, and balancing government deficit". Unatoa mfano wa Malima as if ndiyo policy pekee inayofanya SAPs. Hivi ubinafsishaji wa mashirika na makampuni ya umma alioufanya Marehemu Mkapa miaka ya 90s na ruksa (opening policy) ya Mzee Mwinyi, kwa mtazamo wako yalikuwa mapenzi ya Serikali ya Tanzania? ...Ni masharti ya Magharibi ili kutoa mikopo kwa nchi kama zetu. Ninachokiona pia kwako ni kuamini kuwa masharti hayo ni ya manufaa kwenu, ukiamini sera hizo (SAPs) mnaundiwa dhahiri kuwaletea maendeleo. Ndiyo maana uko kuzishabikia!! China ameibuka recently, miaka yote mpo na Magharibi wakiwatengenezea sera za kufuata, mmenyanyuka wapi zaidi ya kuendelea kuwa wanyonywaji? Na kwa taarifa yako, upo mjadala sasa kuhusu mapungufu makubwa ya SAPs unaozidisha walakini wa hizo financial institutions mbili katika maendeleo ya nchi masikini.

Lakini pia, hakuna mahala nimekwambia kuna mkopo usiorudishwa (sijui hoja yako imetokea wapi kuniuliza kama nimewahi pata mkopo usiorudishwa). Au unataka kuniambia mikopo ya West hairudishwi, ila ya China ndiyo inarudishwa? Kama hukuelewa hoja unauliza. It was straightforward kuwa mikopo/misaada ya miaka yote tuliyoipata na tunayoipata kutoka West tunailipa eidha kwa monetary repayments ama kwa masharti ya kuimplement sera fulani wanazozitaka wao. Hizo sera wenyewe hudai ni kwa ajili ya kusaidia tujikwamue kimaendeleo, jambo ambalo halijawahi kuthibitishwa na nchi yeyote kuendelea kwa kufuata sera zinazotoka West. Badala yake sera hizi huzifanya nchi masikini zishindwe kujitengenezea sera zao wenyewe. China wao wamekuja tofauti, hawajali unavyoiendesha nchi na mipango ya sera zako. Isipokuwa, wao wanaingia nawe mkataba katika eneo mnalokubaliana wao kuligharamia. Na hii model yao imekuwa tishio kwa West. West wanaichukia China kwa kuwa China haiendani na tabia zao za kuzitungia nchi masikini sera na taratibu za kuendesha nchi. Na nchi masikini sasa zinaiona China kama kimbilio maana haina masharti juu ya kisera na taratibu za kiutawala wa nchi.

Mwisho, fungua mawazo usitegemee habari za West tu. Maana naona nawe umekuja na habari za Malaysia sijui Indonesia. Bado uko na BBC na CNN. Dunia ni zaidi ya West sasa.

#Kalaghabao
 
Iwapo ulisoma kwa kukariri, hayo ndiyo matokeo ya elimu yaklo.

Kwa elimu yako ya kukariri utasema kuwa vile philosophy ya market economy ilikuwa developed na mwingereza John Maynard Keynes, basi imekuwa imposed Africa na nchi za Magharibi. Au kwa mfano mwingine, kwa vile magari yalivumbuliwa na mjeruman Karl Benz, basi yamekuwa aimposed kwenye maisha ya waafrika na nchi za Magharibi. Au kwa vile ndege zilivumbuliwa na wamarekani Wright Brothers, basi zimekuwa imposed Afrika na nchi za Magharibi.

Pumba tupu!!
 
Hawa wachina hawa kunguni?au kuna wengine labda siwajui?Huko Ethiopia tunawakamata mamia kila siku hapa kwenye malori mara porini wanakimbia kwao.
Si wabaki huko km mchina kawasaidia.
Tafadhalini sana
 
Iwapo ulisoma kwa kukariri, hayo ndiyo matokeo ya elimu yaklo.

Kwa elimu yako ya kukariri utasema kuwa vile philosophy ya market economy ilikuwa developed na mwingereza John Maynard Keynes, basi imekuwa imposed Africa na nchi za Magharibi. Au kwa mfano mwingine, kwa vile magari yalivumbuliwa na mjeruman Karl Benz, basi yamekuwa aimposed kwenye maisha ya waafrika na nchi za Magharibi. Au kwa vile ndege zilivumbuliwa na wamarekani Wright Brothers, basi zimekuwa imposed Afrika na nchi za Magharibi.

Pumba tupu!!
Ona sasa, ndiyo shida ya vitoto vinavyoamka na kushindia TV!
 
Bahati nzuri hujui unachochangia!!
Mosi, kitendo cha kusema tu SAPs ni suala la serikali yetu na sio suala la Magharibi ni wazi umekiri mapungufu ya SAPs na kuitupia lawama Serikali. Shida yako hapa inaonekana ni elimu tu, kasome vizuri ujue kuwa SAPs si ya Serikali, ni ya Magharibi (Mkuu, umeshindwa hata kutazama Wikipedia tu kabla ya kuandika? Structural adjustment - Wikipedia).
Pili, unaonekana kuwa na mawazo mafupi sana. Umeonekana kutetea ushoga na multipartism, na umeshikilia hapo wakati unaona kuna "nk". Umeonesha kutojua ilipo hoja. Hoja si mifano. Siku nyingine unapojibu tafuta hoja ilipo na usishambulie mifano (hii ikusaidie katika maisha yako yote).
Tatu, ni nani amekuambia miaka ni 99 tu?! Hivi na akili yako huwa unadhani kila "negotiation" inaleta 99?
Mwisho, bado hujanishawishi. Ni heri mimi niamue namna ya kuuendeleza uchumi wangu, kama ni kujenga madaraja, shule, barabara, bandari, nishati, reli, hospitali, nk, halafu nitafute muwezeshaji tukubaliane terms kuliko mtu aniletee hela na anipangie jinsi ya kuishi ili aendelee kunipa hiyo misaada.

Nilikuelewa kutoka point ya kwanza!! Lakin hiki kichambo nimekielewa zaidi[emoji1430][emoji1430]
 
Una mtazamo mfupi sana; mtu anajenga reli au bandari anaitumia miaka 99, si akimaliza muda huo anakuachia kutu tupu? Mtazamo wako ni wa kupenda vya bure, lakini unapata vya bure ambavyo havina thamani.

hayo mambo unayopinga ndiyo hayo wachina wanayatumia, lakini kama wewe kwa mfano siyo gay halafu serikali ikasema gay wote wana haki sawa na watu wengine wewe yatakuhusu nini, kwani hao gays watakuja kukupanda kwa nguvu? Serikali yetu ina sheria dhidi ya kulawiti, na kuruhus gay haina maana ya jufuta shera hiyo.

Multiparty system ndiyo tunayo kwa miaka takriban 30 sasa, je unailalamikai pia? imekuharibia nini? Structural adjustment programs ni swala la serikali yetu; siyo swala na nchi za Magharibi.

Kichungu[emoji23][emoji23][emoji23]wazungu wamekupa nn kichungu !! Africa ina more than 5decades tangu uhuru laki hamna chochote
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom