Pre GE2025 Mtazamo: Wanamtengenezea mazingira ya kuchukiwa na umma ili 2025, kundi kubwa la CCM lijitenge ili wamuangushe kwenye uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Heshima mkuu 'Uthman'.
Nashindwa kuelewa vizuri unacho lenga hasa ni kipi hapa.

Mhusika mwenyewe, kama unavyo muelezea; kisha onyesha ishara nyingi sana tokea achukue madaraka; na kwa bahati mbaya sana, ishara zote zinaonyesha kuchanganyikiwa!

Sasa unataka kunishawishi wakati wa saa mbaya hii kwamba atazinduka na kufanya maajabu?

Mimi siamini kamwe uwepo wa kundi la uhujumu; hii ni nadharia potofu inayo wekwa mbele kutafuta mchawi mwingine ambaye hayupo.
 
Na wewe ni walewale usijifanye kumtetea kiaina.
 
Jaribu kutafakari upya kuna mengi zaidi ya yaonayo macho yetu. Hakujakuwa na nguvu ya upinzani kuweza kushinda Urais wala majorty ya bunge.Tusidanganyike na mtandaoni ambako ni representation ndogo sana ya watanzania.Leo tukipiga kura Chama Tawala kinashinda kwa kishindo.Mkuu hana haja kabisa ya kupoteza watu ili ashinde uchaguzi,kwa nguvu ipi waliyonayo upinzani?
Nauona mnyukano ni wa ndani kwa ndani,kwani ashindae ndani kashashinda nje.
 
Jaribu kutafakari upya kuna mengi zaidi ya yaonayo macho yetu. Hakujakuwa na nguvu ya upinzani kuweza kushinda Urais wala majorty ya bunge.Tusidanganyike na mtandaoni ambako ni representation ndogo sana ya watanzania
Hapana. Kamwe sikubaliani na wazo hili. Hii ni sehemu ya mawazo yaliyopo huko CCM pekee.
Weka uchaguzi wenye mazingira ya haki; halafu njoo hapa uyaseme hayo. Kwa hiyo, hata hili uamini wako ni kwamba Samia siyo mshiriki katika kuwanyima wananchi haki ya kuwachagua viongozi wao?
Toa mfano wowote unaoonyesha kwamba yeye Samia atasimamia haki katika uchaguzi.

Ni rahisi sana kwa watu huko ndani ya CCM kutoa 'general statement' za aina hii uliyo toa hapa, bila ya kutoa uthibitisho wa aina yoyote.
 
Leo tukipiga kura Chama Tawala kinashinda kwa kishindo.Mkuu hana haja kabisa ya kupoteza watu ili ashinde uchaguzi,kwa nguvu ipi waliyonayo upinzani?
Nauona mnyukano ni wa ndani kwa ndani,kwani ashindae ndani kashashinda nje.
AAAlaaaa!
Kumbe unazungumzia yale yale ya kuwahujumu wananchi wakati wa uchaguzi?

Kama hivyo ndivyo, nami nitaunga mkono mnyukano huo uliopo huko ndani ya CCM ili mradi pawepo na ahueni kidogo huku nje.
 
UPo sahihi huyu mama anazungukwa na wana ccm wenzake yy aunde taasisi itayokuwa juu ya police na Takukuru.
Aisee 😯, unamaanisha aunde taasisi kwa maslahi binafsi ya kisiasa kisa wana CCM!!??
Hoi hapana kabisa.
 
🙏🙏🙏🙏 umemaliza
 


Tulisha toa mwongozo hapa. Mama kumaliza haya ni lazima awe wazi lakini wamepandikiza washauri wao ambao wana mwambia Mama asiongee iwe sirisiri kumbe ni wale wale wabaya wake.
 
Hajitambui yuko kizenji tu
 
Hakuna wa kuthubutu kujitenga.
 
watu hawaogopeshwi kwa style hiyo.Kilichofanyika nikujenga chuki na hasira kwenye mioyo ya watu.na kama mawazo yao ni hayo basi iko siku hawataamini kwasababu yatawageuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…