Mtazamo wangu kuhusu Mahojiano aliyofanyiwa Rais Putin

Unaweza kwenda kula bata Beijing au Moscow?
Utakula bata lipi huko wakati muziki mzuri, NBA, Football, sinema na starehe nyingine zote unazozijua viko USA na Ulaya.
Starehe kumbe umeziyakisi kwa mtindo wa kimarekani??
Mbona hata UAE/Dubai starehe zipo pia?
Pata muda katembelee visiwa vya Cappadoccia Uturuki kuna starehe zote unazozijua wewe.
 
Bado udini unakukandamiza fikra we kijana.
1)Sababu ya waarabu kuhamia US ni ukimbizi na kwa sasa hivi wakimbizi wengi hukimbilia Turkiye na Qatar ambako uchumi umekua.
Kafuatilie idadi ya wakimbizi wa kiarabu utakuja kuona Uturuki imepokea wakimbizi wengi kuliko hiyo US.
Kuhusu CHINA TOWN UNAREJELEA KIPINDI CHA OPIUM WAR AMBAPO CHINA ILIKUA INAONGOZWA NA WARLORDS KILA KONA,Wimbi la uhamiaji likatokea kutoka China kuja US kutafta maisha na China town ilianza miaka ya Opium war,hujui historia kasome.
2)Unaowataja wewe wengi wao wakimbizi na wahamiaji haramu ndio wana ndoto za kuzamia huko.
Ila kwa watu wanaotafuta potentials asia ndio kuna potentials nyingi.
KAFUATILIE INDONESIA,MALAYSIA,QATAR,TURKIYE NA SINGAPORE NA MACAU KESHA URUDI.
Halafu usipende tu kudandia directly inapotajwa nchi kinzani na US ukakimbilia za kiarabu,japo zipo baadhi za kiarabu.
Hiyo Saudi Arabia yenyewe inatajwa kutaka kuua soko la mpira la Ulaya kwa uwekezaji wanaouweka.

Pia Trump alipiga katazo la waislam SIO WAARABU.
 
Basi kuna mengi huyafuatilii ndugu.
Sio kila masharti anayoweka US katika ushirika basi ni kuwabana mataifa kisa yanaendekeza kuomba misaada.
Kuna sehemu ngapi USA alipokosa interest zake akafanya regime change katika hizo nchi??
Kuna sehem ngapi USA aliponyimwa interest zake akaziwekea sanctions hizo nchi?
Mathalan kafuatilie mzozo wa Venezuela kesha uniambie je, hiyo sio kuingilia sovereignty ya nchi husika??
 
Kwa nini nao hawa-reciprocate? Vikwazo vya Marekani ni unilateral - vinazuia ushirikiano na Marekani na washirika wake (wanaokubali). Sio vya kimataifa kama vya UN.

Nchi zilizopigwa vikwazo nazo zinaweza kuiwekea Marekani vikwazo unilateral zikitaka.

Btw, hivi karibuni Urusi, China, Mexico, Canada na EU wameshawahi kuiwekea Marekani vikwazo vya kibiashara kujibu mapigo.
 
Unafikiri US wanaweza kufanya regime change North Korea, China au Iran? Ya Venezuela, Cuba na South America yote nayajua vizuri sana. Nchi yeyote ikijilegezalegeza wako wahuni watakajaribu kuiingilia.

Uzuri wa US serikali yao inapofanya mambo ya ovyo nje ya nchi habari zake zikivuma ndani ya nchi, wananchi huanzisha harakati nzito kupinga na kupambana na serikali. Mfano ni vita ya Vietnam, Korea, Iraq, hata vita ya Urusi na Ukraine na ile ya Gaza Wamarekani hawako pamoja wao kwa wao na wao na serikali yao.

Angalia Rwanda inachofanya huko DRC na kwa majirani wengine. US ina interest zake ambazo kusema kweli nyingi sio njema kwa mataifa husika. Ikipata mwanya inajipenyeza. Mataifa mengi yenye uwezo hufanya hivyo. Ni juu ya kila nchi kuwa makini kujilinda. Ndizo kazi za TISS na majeshi mengine.
 
N.korea alitaka ila kashindwa maana N.Korea iko backed na China since vita za mgawanyo 1959.
Iran alijaribu pia mpaka sasa na anajaribu na aliposhindwa kufanya regime change akaiwekea economic sanctions kibao Iran pamoja na hiyo N.Korea hata hiyo Venezuela alitaka fanya regime change akafeli akaishia kuwawekea economic sanctions pia.
China hawezi maana ni taifa lenye nguvu sawa na yeye US kiuchumi na kisiasa za kidunia,ndio maana hata Ursula Vonder leyen aliwaambia US wazungumze na China wayamalize juu ya mzozo wa Taiwan maana ikilipuka vita dunia itaumia kwa namna ambayo haikuwahi kabla.

Hata hao wananchi wanapolalamika juu ya mambo ya hovyo ya ufadhili wa vita zinazoteketeza kodi zao je lini walisikilizwa?
Si mpaka leo US inapanga package mpya ya msaada wa kivita Ukraine na Israel?
Mataifa mengi hufanya hivyo ila mtindo wa USA and allies ni mbovu na unaoacha makovu.
Bora hata mtindo wa China wa kung'ata na kupuliza atleast kuna mutual benefits.
 
Usichokijua ni kwamba kila muda linapoanguka taifa fulani kubwa hua zinakuja na ideology mpya au namna ya kuendesha dunia

Kulikua na mataifa yaliitawala dunia miaka na miaka ila yalianguka na maisha yakaendelea kama kawaida yaani

Hata Americant ikitokea likaanguka maisha yataendelea kama yalivyoendelea huko nyuma ila kutakua tu na mabadiliko fulani fulani basi
 
Ndio mlivyo karirishwa na MSM kama
 
Obvious. Ni kama kuelewa kuwa mwaka 2095 wote tunaochangia hapa JF mwaka huu hatutakuwepo.

Anyway, watakaobahatika kuwapo Marekani ikianguka watashuhudia hilo anguko.

Wenye kupata tabu hivi leo ni wale wanaotarajia anguko la US litakuja upesi; kwamba lipo karibu sana kutokea. Kitu ambacho siamini.
 
Us ipi ambayo haiwezi kuingilia nchi nyengine na nchi makini kwa mtazamo wako inakaaje

Us hii hii iliwachagulia mpaka rais wa mchongo wale Venezuela baada ya kuona rais aliepo hatakua kwa maslahi yao
 
Nadhani hakuna anaetarajia anguko la Americant litakuja lini hili suala umesema wewe

Ila uhakika nikwamba hata kama mwaka 4000 Americant itaanguka na maisha yataendelea bila ya uwepo wa Americant na hii ndio system ya maisha ama dunia ilivyo
 
In reality US ishaanguka ila theoretically bado super power wa mchongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…