Mtazamo wangu kuhusu siasa za Tanzania na Rais Magufuli


..Mbunge anatoa msaada halafu anaishia kukamatwa?

..kwanini huo msaada wake usipokelewe na kukamilishiwa taratibu badala ya kumsumbua na kumdhalilisha?

..huyo angekuwa ni mbunge wa ccm asingetendewa namna hiyo na hicho ndicho kinachotukera baadhi yetu.
 
Wewe hueleweki.

Hoja yako ilisimamia Lissu kuichafua Tanzania, sasa huku kwenye ushoga siku zote huwa mnapatumia kama kichaka kuficha maovu yenu.

Hata Makonda alivyozuiwa kwenda Marekani mlijaribu danganya watu sababu ya ushoga, wakati ukweli halisi mnaujua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahyo unataka kusema kwmb Tanzania inahitaji Rais mwenye siasa nyingi kuliko kutenda, ckia nikwambie mnyonge tumnyonge ila haki yake tumpe, mm cjampigia kura Rais Magufuli lkn pia hata maisha yng co mazuri kivile but haitoshi kuwa mbinafsi kwa kutoona juhudi anazofanya Magu, japo ni kweli ana mapungufu yake lkn kwa hali tuliyokuwa nayo ilitupasa kuwa na rais huyu, umeongelea kuhusu siasa kubanwa, cjui uhuru wa habari, je watu wanakula uhuru wa habari?, watu wanatembea juu ya uhuru wa habari? Watu wanakunywa uhuru wa habari? Nikukumbushe tu kwmb tangu tupate uhuru nchi hii hatujawahi kujenga reli zaidi ya kuhangaika na reli ya mkoloni, je hilo hulioni unaona uhuru wa habari, ni kweli uhuru wa habari kwa ss umebanwa, je unaonaje uhuru wa habari kubanwa kwa miaka 10 lkn kupata reli kwa vizazi na vizazi au kukosa reli, miundombinu bora, maji safi na salama, vituo vya afya lkn kuwa huo uhuru wa habari ambao kila cku tulijiongopea kuwa nao ilihali watu wana EPA nchi, wana ESCROW nchi kila cku.

Watanzania tuache unafki na ubinafsi, tusimame pamoja kujenga nchi, siasa hazijawahi kutupeleka popote zaidi ya kutuumiza tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

..wakati wa kesi Babu Seya alidai yeye ni hanithi.

..hivi majuzi amefuna ndoa na KADA WA CCM!!
 
Kama hilo ulikuwa hulifanhamu, hata yaliyofuata baada ya hilo tukio nayo utakuwa huyafahamu pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

..Reli ya TAZARA ilijengwa kati ya 1970 na 1975.

..haya madai kuwa hatukujenga reli tangu tupate uhuru mnayatoa wapi?
 
Kusema kuwa Tanzania inakandamiza ushoga kwa kukataa sio kuichafua Tanzania? Anadai kinachofanyika ndani ya chupa cha mashoga hakihusu serikali sio kuichafuta Tanzania?

Swali langu linabaki pale pale Tundu Lisu anazunguka kwa mabeberu akiwabembeleza na kupeleka hoja ili Tanzania iwekewe vikwazo mbalimbali na inyimwe misaada kitu ambacho kinalenga kuwaathiri waTanzania wote kwa ujumla na si Magufuli yeye kama yeye (ila kwa chuki zake tu binafsi juu ya Magu).

Nadhani kwa hapa tulipofikia tunaweza kufunga huu mjadala naona kama hatuelewani, ila unayemkubali wewe anatetea ushoga na kutaka Tanzania tunyimwe misaada kwa kuwekewa vikwazo huku akiwa hatafakari inatuathiri vipi sisi kam Tanzania. .
 
Kama hilo ulikuwa hulifanhamu, hata yaliyofuata baada ya hilo tukio nayo utakuwa huyafahamu pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mie nina kazi nyingi na mambo mengi sio kila kitu nitakifahamu ila nimekosoma na nimekijua. Hata wewe ulikuwa hujui Lisu anatetea ushoga ila leo umejua
 
Kuna mtu aliitwa oil chafu, nadhani unakumbuka ni chama gani kiliyasema hayo lakini baadae wakaja irudisha kwenye engine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..Reli ya TAZARA ilijengwa kati ya 1970 na 1975.

..haya madai kuwa hatukujenga reli tangu tupate uhuru mnayatoa wapi?
Bara bara ya morogoro road imejengwa toka miaka ya 1954 huko ila mpaka sasa inajengwa unachosangaa hapo ni nini?
 
Hii mitazamo ya ajabu sana, yani mtu kwasababu anajenga reli na barabara ndio azuie mengine kufanyika, kwani vikifanyika vyote kwa pamoja atapungukiwa nini?!

Kutokuwapa watu uhuru wa kuongea unategemea maovu yanayotokea yasemwe na nani?

Wewe kwa kifupi ndio mbinafsi, hujui umuhimu wa vyombo vya habari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bara bara ya morogoro road imejengwa toka miaka ya 1954 huko ila mpaka sasa inajengwa unachosangaa hapo ni nini?

..kuna mchangiaji amedai Tz haijawahi kujenga reli tangu tupate uhuru. Kuwa Jpm ndiyo Raisi wa kwanza kujenga reli ktk Tanganyika / Tanzania huru.

..nilichofanya mimi ni kumkumbusha kuhusu ujenzi wa TAZARA ambao ulikuwa ktk miaka ya 70.
 
Hivi hapo "kwa chuki zake binafsi tu juu ya Magu"

Huoni kama huyo Magu wako nae anachuki zake kwa Lissu?

Kwanini akatae uchunguzi kufanyika juu ya lile tukio?

Nakushangaa zaidi unapojumlisha mtu binafsi na taswira ya nchi [Tanzania]

Kama yeye ndie kabeba taswira ya nchi ana wajibu wa kuhakikisha ulinzi na usalama kwa raia wake wote, sio kuchagua, wacha kumtetea.

Nilijua toka mwanzo haupo "neutral" km ulivyodai, sema nikaamua kwenda nawe sawa mpk nikupate, nimeshakupata.

Nami nimeufunga mjadala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hahah
Unalazimisha vitu amabvyo havipo viwe
Unalazimisha maneno juu ya kinywa changu
Unalenga kuwa Magufuli kazuia uchunguzi juu ya Lisu kitu hapocho hakipo
Nionyeshe ushahidi hata wa makala ya gazeti wapi Magu alipinga uchunguzi wa Lisu?????

Mie unanipush ili nionekane namtetea Magu kwa kitu amabcho hakina ukweli ndani yake
Unaibadilisha mada iwe juu ya tukio la Lisu
Hulku swali langu hata moja hujibu huku ukiwa pamoja na Lisu kwa sababu tu hata akitetea ushoga na kuitaka kubomoa maendeleo yetu

Magu ana mapungufu yake, Lisu nae ana yake ila at least Magu hakubali ushoga aiseee
Turudi kwenye Mada yangu kuwa chuki kati ya Lisu na Magu inatuathiri sie huku mabishano yake hayana faia yeyote kwetu
 
Sawa umeweka mtizamo wako, lakini huitaji hata elimu ya form four kujua bandiko lako linatetea nini pamoja na kujificha kwenye kichaka cha 'Sina Chama'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa umeweka mtizamo wako, lakini huitaji hata elimu ya form four kujua bandiko lako linatetea nini pamoja na kujificha kwenye kichaka cha 'Sina Chama'

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa sababu nimeweka mtazamo wangu juu ya Magufuli na Siasa za Tanzania kwa hiyo ina ulazima wa mie kuwa na chama??????

Tanzania bado sana aisee athari za ukoloni watu hawawezi jenga hoja anachoamini yeye anataka kiwe. Mie naheshimu sana mtazamo wako kwa kuwa ni wako hainilazimu niukubali na wala haina ulazima ukubali mtazamo wangu. Vyovyote vile ukweli haubadiliki utabaki kuwa ukweli tu. .
 
Kwani hayo yote hayawezi kufanyika bila kubana uhuru wa habari na demokrasia? Au bila kutekana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CHADEMA hawawez kuwasifia CCM Wala CCM haiwez kuwasifia CHADEMA Kwan CHADEMA au CCM mmoja akijenga nchi lazika meingine atapinga tu cos siasa ni ajira kwao wao kua wanasiasa Sio kwamba ni sababu wanataka tujengewe vitu vizuri apana wanataka madaraka ili maisha Yao yawe saf

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…