Mtihani wa usaili wa Tax Officer (TRA) wavuja

Poleni sana vijana. Inauma lakini sitaki kuamini kama ilivuja. Vinginevyo, uthibitishe pasipo na shaka.

Sawa, majibu unapaswa kuyarudisha na karatasi ya maswali. Lakini wapo wenye uwezo wa kurudisha majibu pekee. Au mtu alipewa karatasi mbili za maswali, moja akapeana nyingine akabaki nayo. Akaja kupiga picha na kurusha online.

Lakini kama ilipangwa iwe lazima iwe tu. Hata kama paper lisingevuja, kama fulani alishapangiwa kupewa kazi, hata kama atafeli huo mtihani atapewa tu kibarua.

Maisha haya ya sasa ni magumu sana kwa waajiriwa. Kipindi hicho cha JK, sisi tulikuwa na uangalau.
 
Hahah unatoa majibu mepesiiii kwny maswali magumu.Bongo tambaraleeeee aisee.
 
Ukirudisha karatasi ya majibu bila kuweka hiyo ya maswali unakuwa disqualified. Pia msimamizi hawezi kukubali kuipokea
Nani afanye hivyo ili tu aende kupiga picha?
Hiyo paper ni kweli imevuja, na hii ndio sababu nchi ipo vilevile miaka nenda rudi sababu wajinga ndio viongozi
 
Na ndio maana nimemwambia huyo jamaa anatoa majibu mepesiiii kwny maswali magumu.
 
Na ndio maana nimemwambia huyo jamaa anatoa majibu mepesiiii kwny maswali magumu.
Huna logic!.

Hujaona point kuwa inaweza kutokea ukapewa karatasi mbili za maswali kwa wakati mmoja? Mbona unakaza fuvu?

Anyway, I don't have to argue with a fool.
 
Duuh! Tena karatasi yenyewe imechoka dizain. Hii inaonesha ni kweli kitu kilivuja. Mkuu utumishi achana nao, utapoteza pesa nyingi.

Binafsi sina mchongo kwa sasa lakini siwezi kuomba kazi kupitia hao jamaa
 
Hata mwaka 2014 interview ya fire pale gereza la Ukonga paper ilivuja,watu tunatoka kwenye interview majamaa wanatamba wako na paper
Hakuna kipya chini ya jua aisee., at least sa hivi watu wamekuja na evidence huku mitandaoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…