Mtindo mpya wa rushwa wa kubomoa na kujenga Hospitali ya Taifa Muhimbili

Wacha wabomoe, pesa za tozo si hazina kazi?
Mbona camp nu sijui santiago konobwa imebomolewa?
 
Huu utawala wa mama unatakiwa usifike 2025 ingefaa ajiuzulu maana wanachokifanya sasa ni ujambazi tu. Wanauza nchi na wahuni wake wanapiga dili za ajabu. Sasa eti muhimbili ibomolewe na kujengwa upya. Kwa hizi akili zao wangeanza kwanza kubomoa mji mkongwe zanzibar wajenge upya majengo ya kisasa. Uliona wapi watu wahitaji eti majengo mazuri yanakidhi yanabomewa ili kujenga ya kisasa? Wakifikiri hela rahisi ya kuhongwa wanapoteza akili. Hebu fikiri kwa nini jpm na washauri wake wakaona mfano wa ikulu ya dar ihamie dodoma kama sio kwamba uzamani au historia ya usanii wa majengo ni thamani. Watu tuko kutafuta maendeleo unakuja na wazo la ubadhirifu wa kiasi hicho na unajiita professor.
 
umbea, wivu na roho mbaya ndio sifa kuu ya muafrica mmeliona la Prof janabi ila ikulu kujengwa Dodoma mmekaa kimya.
Muhimbili lazima tuijenge upya hutaki nenda Burundi
Tunakubali jengeni ila tu msivunje ile ya sasa hata ikulu ya dodoma hawakubomoa ile ya Dar tusiifute hiatoria yetu jamani kule tulivyoanza kweli tujenge navkwa kuwa nafasi tunayo basi twende tukajenge majengo mapya na ya kisasa zaidi kuliko kubomoa upya na kupoteza taswira ile ya awali ukarabati wa ndani ya majengo ni sawa tu kuweka air condition ,labda lifti na miundo mbinu ya kisasa lakini sio kupiga nyundo na kuanza upya.
 
kwanza hiyo ni kumbukumbu ya mzee sewa haji aliijenga hiyo hospital na akataifishwa kwa nini waibomoe ? wajenge ya kwao sehemu zingine kama walivyo jenga iloganzala, huu ni wakati wa kula akija mwingine nafasi hii huipati
Jengo litakaloachwa ni sewahaji pekee kibasira na mwaisela yote yanavunjwa

Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
 
Bongo hakuna kitu tunajiweza, unaweza kuona kama utani ila ndio hali halisi. Muda mwingine unajiuliza au huko juu kwenye hizi teuzi kuna neema za kutisha? Wasomi wetu wanabadilika akili kabisa, mpaka unashangaa.
 

Tusimlaumu Mama kwenye kila kitu huu utamaduni wa rushwa umeanza siku nyingi sana. Kwasababu kuna pesa za ujenzi siku hizi hata Uwanja wa Taifa tutasikia ubomolewe maana ujenzi ndiyo rushwa mpya Tanzania.
 
Hakika lisemwalo lipo rushwa sio mpaka mtu atoe hongo, hataplan tu ttajua kuna ujanjanja tu kuna sehemu hakuna hata dispensa halafu leo ubomoe jengo na hakuna dawa unaenda nunua nje ipo vipi hapo
 
Wacha wabomoe tu maana ni kuiboresha
 
Kuna watu wanaumia na maendeleo wakati hata muhimbili hawajawahi fika
 

Tuna nchi ya ajabu sana -- TAL
 
Kwanini msitafute sehemu nyingine kujenga tena ukizingatia pale pamejaa. Ni kama vile kuna mashindano sasa ya kutafuta miradi ya kula pesa
Mbona washaeleza wanajenga upya kwenda juu bqdala ya chini
 
Akili ile ya kujenga lami ya Bagamoyo road na kuibomoa muda wa kufanya upanuzi wa barabara ndio imehamishiwa kwenye majengo ya serikali halafu mnasema nchi ni maskini. Upuuzi mtupu yani!!!
Hospital itajilipa

Barabara ya Bagamoyo miaka 10 ishapita toka wamejenga, mahitaji ya wakati ule na ya sasa ni tofauti, hivyo lazima wajenge upya kwa mahitaji ya miaka 25 ijayo.
 
Mradi hauna tija kwako ila kwa wahusika wanao ona mbele na walio pale kila siku wanaona kuliko kuongeza majengo bora kujenga mengine bora
 
We mhaya kumbe Unasafiri kwa basi?
 
Unasema kama nani?

Ushauri wako hauna maana ndo maana hukuulizwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…