Sio kuwapeleka watoto nyumbani likizo. Kama bado una wazazi wako baba, mama, mashangazi, wajomba, n.k unaowaamini au ambao walikulea na wewe na bado wapo kijijini, peleka wanao wakasomee huko angalau elimu ya msingi tu alafu watoe waendelee na elimu zingine huku mjini. Hii itawafanya sio kujua nyumbani bali kuwa sehem ya jamii ya kwenu. Pili watapapenda sana kwa moyo wao na watakuwa wanataka wenyewe kwenda na sio kuwalazimisha kwenda kwa sababu wana moments nyingi sana za kukumbuka huko nyumbani, wana marafiki waliokua nao huko tangu utotoni, n.k. Lakini pia unawafungulia nafasi ya fursa nyingine nyingi kwa kuwa watakuwa na uwezo wa kurudi kijijini kutumia fursa zilizopo ukizingatia mijini kumeshakuwa congested na fursa nyingi ziko occupied. Mfano mtu anaweza kurudi kijijini kugombea hata nafasi za kisiasa kama udiwani, ubunge, n.k na bado akafanikiwa maana anatambulika na jamii yenyewe.
Lakini pia watoto wakikulia kijijini wanakuwa warithi wa boma na mashamba yenu na kuyaendeleza. Mfano mzuri mimi niliacha kazi Standard Chartered Bank mwaka 2015 nikarudi kijijini nikapewa mashamba na babu nikaanza kilimo na sasa nimepiga hatua na nimefungua kampuni ya masuala ya kilimo. Babu alinipa mashamba nikalime kwa kuwa nimekulia kwake na anaona kabisa baba yangu na baba wadogo wameshalowea mjini hawawezi kurudi kukaa tena kijijini. Sasa babu ameshafariki mimi ndio jicho la ukoo mzima maana baba na baba wadogo wote na familia zao wakija wanafikia kwangu na hata wao kama Mungu akiwachukua wana uhakika familia yetu ina mtu wa kuendeleza heshima yake pale kijijini japokuwa watoto wao wengine hawataki kukaa kijijini ila wanapendaga kuja kwa ajili yangu.
Watoto wakifanikiwa kurudi kijijini hata nyie wazazi mnakuwa na hamu ya kwenda kijijini.
N.B: Japokuwa kila jambo lina faida na hasara zake na ndo maana wengi hamko tayari kupeleka watoto wenu wakalelewe na wazazi au ndugu zenu kwa kufikiria ndo kuwapenda sana, ila pia ina faida sana kwa upande mwingine na kwa baadae.