Mimi ni mawazo yangu binafsi na nawatakia yaliyo mema kama Taifa.
Warnings: Hii tabia iliyoanza kiongozi akiachia madaraka, basi mnaanza kushitakiana ni dalili mbovu kabisa kama Taifa. Mambo mengine kama kiongozi yalishapita ni busara na hekima kuyaacha yapite.
Kumbuka uongozi siyo suala la kudumu itafikia wakati mtaachia hatamu na wanaweza kuingia tena ktk uongozi wengine watakao kutarget wewe binafsi na jamii yako.
Nawataenda mbali zaidi na kuondoa kinga ya kutoshitakiwa kwa kiongozi. Na kwa mtindo huo mnatengeneza siasa za kuanza kupiga kura kwa ukabila na ukanda ili kuja kukomoa watu fulani. Viongozi kuweni makini.
Nawahusia kwa sauti ni kitoka nyikani.
1. Kwani kuna kiongozi aliyepita kashtakiwa na aliyepo...? Kumbukumbu zilzopo ni kuwa;
å Mpaka Hayati J. K. Nyerere anakufa, hakuwahi kushtakiwa popote na Rais Ally H. Mwinyi...!
å Retired Pres. Ally H. Mwinyi, huyo anakula pension yake tu. Hayati Benjamin Mkapa hakuwahi kumpeleka ktk mahakama yoyote...!
å Hayati Retired Pres. Benjamin Mkapa, kafa akiwa hana kesi yoyote mahakamani kutoka kwa mrithi wake Retired Pres. J. M. Kikwete...!
å Retired Pres. J. M. Kikwete huyo anaendelea kura pension yake kwa raha zake Msoga, hakuna kesi yoyote dhidi yake toka kwa aliyempokea kijiti Mwendazake John P. Magufuli...!
å Vivyo hivyo Hayati John P. Magufuli, hakuna kumbukumbu kuonesha kuwa amefunguliwa kesi fulani mahakamani na utawala wa Rais Samia S. Hassan....!
2. Au unataka kutuambia kuwa Ole Lengai Sabaya ndiye usemaye kuwa kashtakiwa..? Sasa huyu yeye ni nani kwani kwa sababu hadhi yake ni raia ya raia wa kawaida tu kama walivyo raia wengine walio na kesi mahakamani...??
3. It's obvious that, wewe ni mfuasi wake na mnufaika wa uhalifu wake because if someone looks at your face, he/she can easily see desperation and disappointment...
4. Na bado. Hii ni rasha rasha tu. Maana viongozi wajinga na wapumbavu sampuli ya Ole Lengai Sabaya, wasio na kinga yoyote ya kikatiba, wasioweza kutumia akili zao vizuri ktk kutekeleza majukumu yao ya kiserikali na badala yake wanatumia vibaya madaraka yao (abuse of power) ili kuumiza, kuiba, kuua na kufanya ufisadi dhidi ya raia huku wakijidai na kusema "mimi ndiye serikali, hakuna wa kunifanya lolote", wako wengi sana....!!
5. Siku utawala wa CCM utakapokuja kuanguka na kukoma, mahakama zitakuwa bize mno. Mpaka makaburi ya baadhi ya binadamu hawa yatakuja kufukuliwa au la basi yatacharazwa viboko sana....!!