Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahaha!haina stop watch mkuu?Kwakifupi nikwamba unapokufa time linakuwa stoped to you. Ye kafufuka na umri uleule ila kakuta dunia ishasepa kwa miaka mitano mbele
Kichwa cha habari "MTOTO MIAKA 11 AFUFUKA MKOANI GEITA"
content "mtoto huyo alionekana usiku katika kijiji cha Segese kata ya Msalala wilaya ya kahama akiwa anaranda randa katika Maduka."
Mtoto kumbe alikua misele, we unapotosha unasema kafufuka
Kwahiyo ukizikwa unaendelea kukua! Waliofariki miaka 20 iliyopita wakiwa na umri wa miaka 90 leo umri wao ni miaka 110! Happy Birthday to you all.
Sasa hujaelewa nini hapoKichwa cha habari "MTOTO MIAKA 11 AFUFUKA MKOANI GEITA"
content "mtoto huyo alionekana usiku katika kijiji cha Segese kata ya Msalala wilaya ya kahama akiwa anaranda randa katika Maduka."
Mtoto kumbe alikua misele, we unapotosha unasema kafufuka
Kichwa cha habari "MTOTO MIAKA 11 AFUFUKA MKOANI GEITA"
content "mtoto huyo alionekana usiku katika kijiji cha Segese kata ya Msalala wilaya ya kahama akiwa anaranda randa katika Maduka."
Mtoto kumbe alikua misele, we unapotosha unasema kafufuka
Sasa wewe mbona umeshindwa kutafakari mada rahisi sana kama hii na ukaona ya kuwa anuani ya mada na kilichomo kwenye mada ni upotoshaji na ukashindwa kujua ya kuwa mpaka jambo limetangazwa ni kwamba wapo waliojitokeza ya kuwa wanamjua huyo mtoto ndiyo maana wamethibitisha ya kuwa alifariki.Yalipoishia mawazo yako kutafakari vitu complex ndipo idea ya uchawi inapo anzia
Alikufa kwa ugonjwa gani na ulithibitisha vipi kua waliyekua wanamzika mle kaburini alikua ni huyo dogo ambaye amekufa?Mtoto huyo alikufa 2017 na amepatikana mwaka 2021 akiwa anaranda randa mtaani.
Wameenda kwenye kaburi alipozikwa huyo mtoto, wakafukua wakakuta kuna nguo za baba yake ambaye tayari alishakufariki.
Mtoto huyo pia amekatwa ulimi
Nimesoma nimeona hakuna sehemu iliyoandika watu walikua wanapita nakaburini wakashangaa kuona kaburi linafumuka na dogo akitokaNaona mkuu unakaza ubongo, umesoma habari yote kweli ukaielewa??
Kutangazwa kwa jambo hakutoi uhalali wa hiyo habari ionekane ni ya kweliSasa wewe mbona umeshindwa kutafakari mada rahisi sana kama hii na ukaona ya kuwa anuani ya mada na kilichomo kwenye mada ni upotoshaji na ukashindwa kujua ya kuwa mpaka jambo limetangazwa ni kwamba wapo waliojitokeza ya kuwa wanamjua huyo mtoto ndiyo maana wamethibitisha ya kuwa alifariki.
Sikutukani ila una akili ndogi sana. Huwezi kung'amua haya mambo.
Hakufa wala kuzikwa.Kwahiyo ukizikwa unaendelea kukua! Waliofariki miaka 20 iliyopita wakiwa na umri wa miaka 90 leo umri wao ni miaka 110! Happy Birthday to you all.
Kiufupi hizo ni drama hakuna ukweli hapoSasa hujaelewa nini hapo
Huko Geita naona ushirikina ni part ya maisha yao kabisaMTOTO MIAKA 11 AFUFUKA MKOANI GEITA.
Mtoto Leonard Morisha Mwenye umri wa Miaka 11 Mkazi wa kijiji na kata ya Ngemo wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita aliyefariki June 27 ,2017 katika hospitali ya Geita amefufuka baada ya kuzikwa kwa kipindi cha miaka 5 mpaka kufufuka kwake huku ikidaiwa kukatwa ulimi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Henry Mwaibambe amesema mtoto huyo alionekana usiku katika kijiji cha Segese kata ya Msalala wilaya ya kahama akiwa anaranda randa katika Maduka.
Kamanda amesema mtoto huyo baada ya kuonekana katika Maduka hayo alikuwepo mlinzi katika Maduka hayo aitwae Emmanuel Busiga alimchukua na kumpeleka kwao badae alifikisha taarifa katika uongozi wa kijiji.
"Mtoto huyo ana afya njema lakini baada ya kufanyiwa uchunguzi katika kituo cha afya cha Masumbwe alibainika kukatwa ulimi kwa kiwango kikubwa mishipa ya ulimi wake na kusababisha ashindwe kuongea, " Mwaibambe.
Mwaibambe amesema baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la polisi lilipata kibali kutoka katika Mahakama kwa ajili kufukuwa kaburi lake ambalo mtoto huyo alikuwa kazikwa na kukuta kaptura pamoja na suruali ya Baba mzazi wake aliyefariki mwaka 2019.
#KitengeUpdatesView attachment 2047442
Na hakuzikwa, futi sita mchezo. Unatokaje kwenye futi sita?Hajafa ukifa haurudi ukiona karudi ujue hakufa
Sasa kwanini hukujiuliza maswali ya msingi ya kwamba kwanini akusudiwe mtoto huyo huyo na si mwingine ?Kutangazwa kwa jambo hakutoi uhalali wa hiyo habari ionekane ni ya kweli
Weka mfano wa hizo records kisha nikuulize maswali.Tuna records za habari kama hizo ambazo zilikuja kuwa refuted na hao hao waliozianzisha.
Unajua Uchawi ni nini kwa maana ? Au unakataa jambo usilo kuwa na elimu nalo ? Huu ni uhayawani.Vile vile vyombo vya habari zinaangalia maslahi kutafuta habari zitazofanya watu wafatilie ili wao wanufaike kwa njia ambayo wao wamejiwekea
Hili halibatilishi uwepo wa tukio husika. Jikite kulikosoa tukio hili na utuonyeshe kutowezekana kwake au kinyume chake.Na hiyo inachangiwa na media za kibongo, waandishi wa habari wanekua wakitumia nguvu kubwa kupata habari ambazo wanajua watu wengi watashawishika kuwafatilia, ndio maana huwezi kuona habari kama hizo kwenye CNN, BBC, nk
Alikufa kwa ugonjwa gani na ulithibitisha vipi kua waliyekua wanamzika mle kaburini alikua ni huyo dogo ambaye amekufa?
Kwasababu hiyo michezo hata american got talent inafanyika so we're mature enough kujua tricks za watu katika kitafuta ugali