Kijana uwe unasoma yaani unathibitisha uwepo wa uchawi bila kujua na hapa umekiri ya kuwa uchawi upo.Hakuna uchawi, kuna tricks tu
Got takent huangaliagi?
Mle si ndo kila kitu utasema uchawi sasa?
Uchawi ni mbinu (tricks) japo kuwa si kila mbinu ni uchawi.
Soma hapa chini ili siku nyingine usibishe kwa usiyo yajua.
Nanukuu.
Al Azhari ambaye ni mtungaji wa kamusi maarafu ya kiarabu iitwayo “LisanulArab” amesema:
“Neno “Uchawi”, kwa kiarabu “As Sihr”, maana yake ni kitendo cha kujikurubisha na Shaytwaan na kwa msaada wake (Shaytwaan)”, na akasema pia kuwa; “Uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli.” Ama Swahaba Ibni 'Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema:
"Uchawi ni kuidhirisha batili katika sura ya haki." Hayo ni katika kamusi za lugha.
Amma katika kamusi ya dini, maana ya neno Uchawi (As Sihr), kama alivyofasiri Mwanachuoni mkubwa Fakhruddin Al Razi kuwa:
"Ni kila jambo lililofichika sababu zake, linalotokeza kwa sababu zisizo za kawaida na ndani yake mna hadaa (khidaa)."
Msingi wa uchawi ni mbinu maalumu.