Scars
siku moja rafiki yangu ambaye wakati huo akiwa mwanafunzi shule ya msingi huko Tarime alikwenda shule kama kawaida na masomo yakaanza asubuhi, ilipofika muda wa break wanafunzi walitoka nje ndipo rafiki yangu alikuta pesa ipo chini eneo la shule na akaiokota,ghafla ikatokea kimbunga ambacho alikiona yeye tu,kimbunga kilikuja na mtu ambaye alikuwa amepanda fisi (ni asubuhi) yule mtu akamwambia yule jamaa apande juu ya fisi na jamaa bila kujielewa alipanda na wakatoweka (ikumbukwe tukio hili hawakiona wanafunzi wengine na ile pesa ilitegwa na dawa so jamaa ikamharibu akili akakubali kupanda fisi)
basi ile fisi ilikimbia speed mpaka Gamboshi,huko gamboshi kuna mapokezi aliwakuta na wenzie wanapokelewa kama yale mapokezi tulipewa wakati tunaanza form one,basi walivuliwa nguo zote hapo na ika planiwa wakatwe ulimi baadae,muda huu jamaa akili imemrudi analia sana na kupigwa,baadae wenzie walikatwa ulimi ila yeye hakukatwa (wazazi wake waliwahi kwa mganga) so ikafika muda wa chakula cha usiku msosi ni nyama ya binadamu imepikwa jamaa alikataa kula akapigwa sana so alilala bila kula siku hiyo,anadai misukule haiongei inaguna guna tu kama bubu na kesho yake asubuhi waliamshwa alfajiri kwenda shamba na anadai wakati wanalima watu walipita ila watu wale hawakuwaona misukule ila misukule pamoja na jamaa yangu waliwaona wapita njia wale na kuna muda unakuta mtu anatembea anaenda anagongana na msukule ila yeye kibinadamu anaona kajikwaa tu,ikumbukwe nature ya ufanyaji kazi ni kama movie ya escape from sobibor yani ukichoka ni kupigwa sana na mnalima kutoka asubuhi mpaka mida ya jioni non stop
baadae walikuwa wakirudi gamboshi huko walikuta uji au ugali na kile ambacho hatuwez kuita mboga ya majani yani ni manyasi yamechemshwa (gamboshi hawali nyama kila siku), ilikuwa ikifika usiku wanajipanga kwenye ungo kwenda makaburini kufufua maiti ambazo zimezikwa recently kwa ajili ya kuzila na zile za zamani zimeanza kuoza walipelekea fisi, daily routine nyingine ni kwenda kuwanga usiku ambapo sheiria inassma ukiingia kwa mtu iba vyakula au kama anakula ule nae na ule pale anapofinya yeye ukizubaa ukate ugali pembeni atagundua na usiibe pesa maana utashindwa kutoka
siku zingine walienda highway kusababisha ajari,hizi ajari mnasikiaga gari zimegongana uso kwa uso huwa ni wachawi wanatega vitu fulani barabarani kati kati then wao wanakaa pembeni,hivo vidude nimevisahau jina ila ni vi living things kwenye dunia ya uchawi na ndivo huangusha gari,gari ikianguka tu wanakuja wachawi na kuchukua maiti na kuondoka (wanaacha migomba,ukitaka uelewe hii relate na huu uzi huyo dogo kwao walimzika kabisa wakidhani ni yeye kumbe sio mwili wake)
siku nyingine wachawi wanaroga mtu akiwa na afya njema kabisa,unaugua weeh,ukikaribia kufa wanakuja kuweka kambi nyuma ya mlango wa nyumba ya mgonjwa na wanakaa hapo mpaka mgonjwa afe,akikata roho tu wanaweka mgomba kitandani na kuondoka na mgonjwa (muda huu anapona kabisa) so nyie mtazika mgomba au wakati mwingine wanawaacha mkamzike ndugu yenu kabisa ila usiku wanakuja kumchukua kaburini kwa kupiga kaburi na ka fimbo then maiti inaibuka (wachawi hawachimbi kaburi) wakiichukua maiti inaenda
jana niliongea kuhusu kuzaliana,sex, wachawi huchukua misukule ya kiume na kuipeleka kwa ya kike ikafanye mapenzi,baada ya miezi tisa vitoto huzaliwa na siku hiyo hiyo vinaenda kuwekwa kwenye moto maalumu kama tunavochomaga nyama choma ila tofauti ni kwamba kuna chombo cha kukinga mafuta ya mtoto mchanga,mafuta hayo jamaa alikuwa anaona wanakuja binadamu wa kawaida ambao alisikia wakiongea ni wafanya biashara wakubwa wanaenda kujipaka mwilini ili kuvutia biashara zao na yanagombaniwa haya mafuta licha ya kuuzwa bei mbaya
unaweza kujiuliza mbona wachawi bado tu hawajamkata jamaa ulimi ? wazazi wake walikuwa wanaenda kwa waganga hivo wachawi wakawa wanasahau na siku wakikumbuka inatokea tu kitu sababu zoezi linashindikana,mpaka hapo ni jamaa tu ndiye alikuwa na ulimi
NB
wazazi wa jamaa walifanikiwa kumtorosha Gamboshi na hii ni true story nilikuwa hadi na kipande cha copy ya gazeti